Bila kodi, mikopo wala tozo Serikali kutekeleza miradi ya Tsh 25T

Nchi kama Norway imeweza kuwa tajiri kwa kutumia fedha za rasilimali ya mafuta kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Sisi tuna madini na gesi, kwa nini fedha zinazopatikana huko zisielekezwe katika kufadhili miradi mikubwa na maendeleo ya nchi?
 
Naomba tu niwe mkweli,
Kazi anazofanya huyu mama ni kubwa sana ila hazipewi airtime ya Kutosha kama ilivyokuwa wakati wa Mwendazake ila huyu mama anafanya makubwa
 
Nchi kama Norway imeweza kuwa tajiri kwa kutumia fedha za rasilimali ya mafuta kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Sisi tuna madini na gesi, kwa nini fedha zinazopatikana huko zisielekezwe katika kufadhili miradi mikubwa na maendeleo ya nchi?
Nakubaliana na wewe,
Kama Taifa tunahitaji kutumia Rasilimali zetu,
Tatizo hatuna mtaji wa kuzifikia,
MFANO mradi wa LNG unahitaji zaidi ya 46T tunazipataje?
 
Ndg yangu Balthazar
Hiyo ni typinge error hizo ni US$37million
 
Tunaweza kuchukua mazuri ya PPP ya Mkapa tukachanganya na PPP hii ya mama Samia huenda tukapata kitu Bora kabisa,
Mimi nashauri PPP iwe kwenye miradi mipya tu hii ya Zamani iachwe Serikali ipambane nayo
 
PPP haitumii pesa ya Serikali inatumia pesa za Private ndio maana tunasema Serikali itajenga miradi bila kodi Toka kwa.wananchi

Acheni stori za uongo. Kama serikali haitoi pesa yoyote ila ujenzi unafanyika na Private Sector, mchango wa serikali ni upi?. PPP ni kwamba serikali inatoa kiasi na private sector kiasi.
 
Basi tumpongeze kwa hili alilofanikiwa kwanza,

Hilo la ulinzi ni suala mtambuka na wanaofanya hivyo ni watu wabaya

Amefanikiwa kwenye Nini? Kuomba wawekezaji wa Trillioni 25?. Maana unaongea kana kwamba zimeshapatikana.
 
Acheni stori za uongo. Kama serikali haitoi pesa yoyote ila ujenzi unafanyika na Private Sector, mchango wa serikali ni upi?. PPP ni kwamba serikali inatoa kiasi na private sector kiasi.
Mchango wa Serikali ni Ardhi inayomiliki
 
Mkuu sijui kama Kuna nchi hasa za Dunia ya tatu watu hawatekani,

Kutekana kumebeba mambo mengi na maswali mengi kuliko majibu

Raia anashushwa kwenye basi mchana, polisi wanaambiwa wanapuuza. Kesho yake anauawa , halafu Rais anakuja kudai kifo ni kifo
 
Uko maeneo gani tuonane kamanda ili uamini haina haja ya kubishana

Jitahidi kupambana na suspicion. Huwezi kumsifia mtu kiasi hicho Tena kwenye thread yako Kama sio wewe ndio muhusika. Elezea anachofanya basi, ukianza sifa nyingi moja Kwa moja tunakichukulia ni wewe Kafulila unajipromoti.
 
Serikali haitumii mtaji wake ila wa sekta binafsi nadhani ndio maana ya hii sentesi

Hapo ndio kwenye kigugumizi. Serikali haitoi pesa kwenye mradi, ila sekta binafsi. Na sekta binafsi wakishajenga wanapataje faida. Maana unaongea kana kwamba wanajenga Bure.
 
Kafulila tunataka vitendo sio stori na kujipromoti
 
Raia anashushwa kwenye basi mchana, polisi wanaambiwa wanapuuza. Kesho yake anauawa , halafu Rais anakuja kudai kifo ni kifo
Sijui kama Kuna mtu anaushahidi wowote, Mimi binafsi siungi mkono utekaji na kuuana watu.
Lakini wakati mwingine yaweza kuwa pia ni watu wabaya tu wanaharibu taswira ya nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…