Bila kodi, mikopo wala tozo Serikali kutekeleza miradi ya Tsh 25T

Hapo ndio kwenye kigugumizi. Serikali haitoi pesa kwenye mradi, ila sekta binafsi. Na sekta binafsi wakishajenga wanapataje faida. Maana unaongea kana kwamba wanajenga Bure.
Private lazima wapate faida,
Lakini mwisho wa siku Serikali itanufaika hasa kwa watu wake kupata huduma mbalimbali za kijamiii
 
Hiyo Ardhi Ina thamani sawa na gharama za mradi. Kumbuka Private Sector wanafanya biashara na serikali haifanyi biashara
Ardhi na sehemu ilipo ni mtaji mkubwa, mfano hapo DDC ukitangaza mnada wa 15bn hukosi,
 
Jitahidi kupambana na suspicion. Huwezi kumsifia mtu kiasi hicho Tena kwenye thread yako Kama sio wewe ndio muhusika. Elezea anachofanya basi, ukianza sifa nyingi moja Kwa moja tunakichukulia ni wewe Kafulila unajipromoti.
Sijawahi sifa za Kafulila ila sifa za anachokifanya tu
 
Nchi kama Norway imeweza kuwa tajiri kwa kutumia fedha za rasilimali ya mafuta kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Sisi tuna madini na gesi, kwa nini fedha zinazopatikana huko zisielekezwe katika kufadhili miradi mikubwa na maendeleo ya nchi?
Nakubaliana na hii hoja yako lakini Tanzania sio Norway tunamambo mengi ya tofauti hivyo tujipe muda na sisi.
 
Acheni stori za uongo. Kama serikali haitoi pesa yoyote ila ujenzi unafanyika na Private Sector, mchango wa serikali ni upi?. PPP ni kwamba serikali inatoa kiasi na private sector kiasi.
Hapana ni private ndio wanatoa kila kitu isipokuwa ardhi
 
Tatizo la CCM story nyingi Vitendo kisoda
 
PPP iongezewe ulinzi hasa kuajiri wazalendo
 
Kama unaamini tskwimu za ccm, insbidi upimwe kichwa milembe, tilioni 25!, makusanyo yetu kwa, mwaka ni tilioni 20,matumizi tilioni 45,tunahitaji tilioni 25 za, kukopa, sasa unapata wapi 25 za miradi?
 
Sawaa Personal wa Kafulila a.k.a jina alilopewa na yule Mwanasheria MKuu
 
Kama unaamini tskwimu za ccm, insbidi upimwe kichwa milembe, tilioni 25!, makusanyo yetu kwa, mwaka ni tilioni 20,matumizi tilioni 45,tunahitaji tilioni 25 za, kukopa, sasa unapata wapi 25 za miradi?
Hahaha
 
Daah wewe jamaa na hii ID DAAAH
 
Kwa kuuza nchi , hiyo inawezekana, lakini madhara yake hata vitukuu, vyake wataonja machungu ya kuuza nchi.
 
Kama unaamini tskwimu za ccm, insbidi upimwe kichwa milembe, tilioni 25!, makusanyo yetu kwa, mwaka ni tilioni 20,matumizi tilioni 45,tunahitaji tilioni 25 za, kukopa, sasa unapata wapi 25 za miradi?
Siumeambiwa itatokea sekta binafsi
 
Nakubaliana na hii hoja yako lakini Tanzania sio Norway tunamambo mengi ya tofauti hivyo tujipe muda na sisi.
Haishinfikaninkuwa hivyo ila naona nchi imewekwa kwenye misingi ya kutegemea pesa za walipa kodi pamoja na misaada ili kuiendesha bajeti. Ila miradi mikubwa ya madini ipo kunufaisha wageni na watu wachache
 
Nakubaliana na wewe,
Kama Taifa tunahitaji kutumia Rasilimali zetu,
Tatizo hatuna mtaji wa kuzifikia,
MFANO mradi wa LNG unahitaji zaidi ya 46T tunazipataje?
Tuna resources nyingi kama madini ya dhahabu, almadi pamoja na makaa ya mawe, achilia mbali madini mengine na hata mafuta. Badala ya kukopa kufadhili miradi ya maendeleo uwepo mpango mkakati wa kuhakikisha mapato ya rasilimali inaelekezwa kufadhili LNG pamoja na vitega uchumi vingine ili kuiwezesha nchi kujitegemea. Najua kuna watakaosema kuwa inaweza sababisha vikwazo ila zipo njia za kuepuka vikwazo hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…