Pre GE2025 Bila kujali wasiojulikana, Tundu Lissu aendelea na Mikutano yake Vijijini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Huu hapa ni Mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Kinyeto, Jimbo la Singida Kaskazini, uliofanyika leo saa 3 asubuhi .Ikumbukwe kwamba Lissu amekwisha toa angalizo la kufuatiliwa na kikundi cha Wasiojulikana, ambako tayari kishawashitaki kwa umma.

Pia soma Kuelekea 2025 - Ushauri kwa Tundu Lissu: Omba ulinzi kabla ya kuendelea na michakato



Chadema inaendelea na Ratiba zake bila kujali vijana Wajinga waliosambazwa mitandaoni kwa Ujira duni ili kuizushia uongo.

====

Pia soma: DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali
 
Vijana wajinga ni kama akina Mashambwa?
 
akiulizwa maswali asipanic, fursa ya maswali kaitoa mwenyewe halafu yanamkera 🤣🐒
 
Naona watu wamejaa knoma kuja kusikiliza nondo kutoka kwa mwamba Lissu, vp hakuna picha ya juu ili tuone umati vizuri kama hii 👇 ya mkutano wa Chadema ila jukwaa la juu ina picha ya Mwinyi wa CCM.?

 
JPM alisingiziwa mabaya mengi sana na Chadema

..mbinu za uongo na ukatili za Magufuli zilikuwa za hali ya chini, au za kijinga.

..hali hiyo ndio ilisababisha lawama za matukio yote mabaya ya serikali zielekezwe kwake.

..watangulizi wake serikali ilipokosea lawama zilienda kwa Waziri Mkuu, au Waziri wa sekta husika.
 
N miaka mitatu sasa JPM hayupo ila bado wasiojulikana wapo na wengine wanamfatilia Lissu, vp anayeendeleza haya mambo n nani au ni JPM akiwa mfu.?
 
N miaka mitatu sasa JPM hayupo ila bado wasiojulikana wapo na wengine wanamfatilia Lissu, vp anayeendeleza haya mambo n nani au ni JPM akiwa mfu.?

..Rais Samia Suluhu amebadilisha mbinu za kushindana na wapinzani.

..mpaka sasa hivi hajatumia mabavu na ukatili kama alivyokuwa akifanya Magufuli.

..kasoro kubwa ninayoiona kwa Rais Samia ni kushindwa kuwachukulia hatua wote waliohusika na matendo ya kikatili na kikandamizaji wakati wa utawala wa Magufuli.

..kwamba Samia hajachukua hatua za kisheria inatia wasiwasi kwamba iko siku na yeye atakuja kuwatumia walewale waliotumika na Magufuli kutenda uovu.
 
JPM alisingiziwa mabaya mengi sana na Chadema

..ujinga wa Magufuli ni kama tukio la Mo Dewji kutekwa halafu akaachiwa karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani.

..ujinga mwingine ni tukio la ofisi ya mkosoaji wake, Fatma Karume, iliyoko karibu na makao makuu ya jeshi, kushambuliwa kwa bomu na wahusika kufanikiwa kutoroka.
 
Kwahy hayo yote yakijirudia sasa hv kama ambavyo yanajirudia kwa Lissu mtasema mhusika n nani.?
 
Kwahy wale waliokuwa wanafanya maovu kwa amri ya JPM, sasa hv wanafanya kwa amri ya nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…