Bila kujirudi, Kassim Majaliwa atapigwa chini!

Bila kujirudi, Kassim Majaliwa atapigwa chini!

Tanzania sasa inapitia wakati muhimu sana. Sasa hivi kuna watu wachache ndiyo wameshikilia fungua za amani na katiba ya nchi yetu. Watu hao ni Rais Samia, Kinana, Mbowe, Rais Mwinyi, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Lissu na Zitto. Hawa ndiyo watu muhimu kwenye Katiba yetu ijayo

Waziri Mkuu Majaliwa ana matatizo mawili makubwa

1. Kitendo cha kuengua mpinzani wake wa uchaguzi ili apite bila kupigwa inaonesha alikuwa anapenda ule mfumo na hii imemfanya kutokuaminika kabisa na wapinzani

2. Kitendo cha kukubali hadharani kwamba alikuwa anawatumia wakina Sabaya kule kwa Mbowe kumemwaribia sana.

Kwa mwenendo wa sasa Rais Samia pamoja na Mwinyi wanahitaji viongozi wa upinzani ili waweze kupeleka taifa mbele.

Waziri mkuu bila kutafuta njia ya kutubu na kusema wazi kabadilika itabidi atolewe kwa manufaa ya umma.

Hivyo anaweza kutafutia issue kama Spika Ndugai au tu Rais kufanya mabadiliko ya kawaida au anaweza kutubu na kujirudi kitu ambacho hajafanya mpapa sasa.

Mbowe kwa sasa ana nguvu kuliko Majaliwa. Na akiweka kichwa ngumu na kujifanya ni mzalendo yatamkuta ya Ndugai.

Namshauri awahi haraka sana kuweka msimamo wake wazi bila hivyo atapigwa chini kwani hatakuwa anasaidia nchi au chama
Serikali nzima ya ccm imenufaika na mfumo wa kupita bila kupingwa,aliouanzisha Shetani Jiwe.
Hakuna msafi ccm,ila kama wanataka kumtoa kafara Majaliwa Ili kujisafisha mbele ya jamii,haitoshi,ccm ni saratani ndani ya nchi,dawa ni kuichoma kwa mionzi
 
Mkuu Kamundu , sio Waziri Mkuu aliyeengua bali wabunge waheshimiwa sana, wapinzani hujiengua ili wapite bila kupingwa, na hii ni kwa mawaziri wakuu wote na senior ministers kama Mwandosya.

Sii kweli, Sabaya alikuwa anatumiwa na the status quo yote.

Sii kweli, ila imetokea tuu wote ni waungwana, JPM crushed the opposition and wiped it off na bado Tanzania ikapaa!.

Not necessarily, Tanzania viongozi wetu wapo at the pleasure of the president na sio kuwajibika kwa umma. Baada ya PM Majaliwa kusema alichokisema kumhusu JPM, and what happened thereafter, tungekuwa na utamaduni wa kuwajibika, he shouldn't be there by now!. Hivyo usimpangie Samia!.

Kwa vile hatuna utamaduni wa viongozi kutubu, hana sababu ya kutubu kwa yeyote, hata Spika JYN, kule kutubu ndiko kumeponza, angekauka tuu kwasababu rais hana mamlaka kumuondoa Spika, Jaji Mkuu au CAG!.

Hapa unachanganya nguvu ya powers, popularity, umaarufu na umashuhuri, Mbowe ana nguvu gani?. He is somebody kama Mwenyekiti wa Chadema lakini hana nguvu yoyote nje ya Chadema!. As an opposition leader ni kweli Mbowe commands much respect lakini you can't compare na PM!.

Atapigwa chini na nani kwa kosa gani?. Kama Mama amemkubali, ni amemkubali, subirini tuu 2025 amalize kipindi chake kwa amani. Tusitake kumpangia Mama kazi!.
P

Hivi tujiulize waziri mkuu kwenda jimboni Hai baada ya uchafuzi wa 2020 na kusema tulikuwa tinawatumia hawa akiimanisha Sabaya alikuwa na maana gani? Alisema bila kujua wakati ule Magu atatutoka.

Mpinzani wa Majaliwa aliletewa mizengwe na jina lake kutolewa na sio kweli alijitoa kwa heshima. Saaa kuna sababu gani sasa ya chama kumweka mgombea ambaye tena aje kujitoa sasa mchakato wa kutafuta mgombea kwenye jimbo ulikuwa wa nini hasa?
 
Serikali nzima ya ccm imenufaika na mfumo wa kupita bila kupingwa,aliouanzisha Shetani Jiwe.
Hakuna msafi ccm,ila kama wanataka kumtoa kafara Majaliwa Ili kujisafisha mbele ya jamii,haitoshi,ccm ni saratani ndani ya nchi,dawa ni kuichoma kwa mionzi

Tofauti ni kwa kiti chake ni ngumu kumuhusisha kwenye majadiliano huko mbele. Katika mambo waliokubaliana kwa mujibu wa Mbowe ni kusema maovu yaliyoyekea kwa uwazi sasa je Majaliwa yuko tayari?
 
H
Hivi tujiulize waziri mkuu kwenda jimboni Hai baada ya uchafuzi wa 2020 na kusema tulikuwa tinawatumia hawa akiimanisha Sabaya alikuwa na maana gani? Alisema bila kujua wakati ule Magu atatutoka.
Kuna things that the government people does which goes without saying kuhusu nafasi za ma DCs na ma RCs, enzi za PM Pinda, niliwahi kusema kitu kuhusu hili PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong! hivyo usimtwishe PM pekee jukumu hili, it's a system. Wakati DC Sabaya anakabidhiwa kuwa DC wa Hai, alikabidhiwa some extra duty fulani which he did it vizuri na kufanikisha!, ndio maana aliposhitakiwa yeye tuu nikauliza why him alone wakati kuna wengine wengi who did the same, hivyo nikatoa angalizo Life After Life: Je, wajua Magufuli huko alipo anayaona yote? Je, tuendeleze 'double standards' ya 'cherry picking' au tuiachie Karma iwashughulikie?
P
 
Kati ya maboresho ya JF ninayopendekeza, ni mkimuita member humu muongo:, unaweka na uongo wake kisha unaweka ukweli wako.
P
Mbowe hawezi kumtumikia Samia kama mwenyekiti wa CCM.
Anamtumikia kama Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzania, na Rais Samia pia anamtumikia Mbowe kama Mwenyekiti wa Chadema Taifa.
Huo ndio ukweli dhidi ya uongo wako!

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Elimu ya uraia inahitajika sana!, mazungumzo ya maridhiano ni kati ya vyama CCM na Chadema, na sio Chadema na serikali!. Mbowe anapo ongea na Samia, ni Samia Mwenyekiti wa CCM na sio Samia rais wa JMT!. Ni mazungumzo ya kichama na sio ya kiserikali!.
P
 
Huyo toka aseme uongo akiwa msikitini kule Njombe nimemdharau sana
Ulitaka aseme Magufuli anaumwa? Mbona hata Samia hakusema ukweli alisema Rais anaumwa vimafua tu ila mbona hamsemi Samia muongo na kumdharau?
 
Chadema wanataka waliokuwa Kwa magufuli wote watoke Yani wanaona apo watakuwa wamechukuwa nchi, chuki mbaya sana
Nafikiri kuna kitu hujakifahamu, sio watu wote waliokuwa na Magufuli walifurahia ubabe, ukandamizaji na uvunjifu wa katiba alikuwa akiufanya. Ndio maana unaona mabadiliko yanaanzia CCM yenyewe. Na wala sio CHADEMA, hakuna kinachoweza kufanyka bila CCM hebu elewa hili. Sasa ndio sababu Rais wetu alisema atabadili viongozi ambao haendani na yeye kwenye mkutano wa CCM tulia utajua pole pole.
 
Hata ndani ya CCM na serikali kuna wasio taka vita/vifo/mateso kwa vyama pinzani wanataka siasa za ushindani ambazo ni kioo chao cha kujitazama na kujirekebisha.
 
Ulitaka aseme Magufuli anaumwa? Mbona hata Samia hakusema ukweli alisema Rais anaumwa vimafua tu ila mbona hamsemi Samia muongo na kumdharau?
Hayo ya Magufuli unayasema wewe sijui mlielezana nini naye huyo mpaka kiwi nyeusi kichwani.
 
Enyi WANAFIKI,

Ni nani alitewaambia Kassim Majaliwa hawezi kubadilika na kuepuka mfumo kandamizi?

Changamoto tulizopitia ni za kimfumo, Si za Kassim binafsi.

Kama sa100 ameweza badilika, Kassim aweza badilika pia akiwa Waziri mkuu.

KAMBA, mwigu, napena na wahuni wengine kama hawajaondoshwa, hayupo Bado wa kupoint FINGERS Kwa KASSIM MAJALIWA.

Aamen
 
Hayo ya Magufuli unayasema wewe sijui mlielezana nini naye huyo mpaka kiwi nyeusi kichwani.
Siyasemi mimi bali wale wanaosema Majaliwa ni muongo, na huo uongo wenyewe ndio huo wa kusema Magufuli mzima kumbe anaumwa.
 
Enyi WANAFIKI,

Ni nani alitewaambia Kassim Majaliwa hawezi kubadilika na kuepuka mfumo kandamizi?

Changamoto tulizopitia ni za kimfumo, Si za Kassim binafsi.

Kama sa100 ameweza badilika, Kassim aweza badilika pia akiwa Waziri mkuu.

KAMBA, mwigu, napena na wahuni wengine kama hawajaondoshwa, hayupo Bado wa kupoint FINGERS Kwa KASSIM MAJALIWA.

Aamen
Kwani Samia alikuaje hadi useme kabadilika?
 
Tanzania sasa inapitia wakati muhimu sana. Sasa hivi kuna watu wachache ndiyo wameshikilia fungua za amani na katiba ya nchi yetu. Watu hao ni Rais Samia, Kinana, Mbowe, Rais Mwinyi, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Lissu na Zitto. Hawa ndiyo watu muhimu kwenye Katiba yetu ijayo

Waziri Mkuu Majaliwa ana matatizo mawili makubwa

1. Kitendo cha kuengua mpinzani wake wa uchaguzi ili apite bila kupigwa inaonesha alikuwa anapenda ule mfumo na hii imemfanya kutokuaminika kabisa na wapinzani

2. Kitendo cha kukubali hadharani kwamba alikuwa anawatumia wakina Sabaya kule kwa Mbowe kumemwaribia sana.

Kwa mwenendo wa sasa Rais Samia pamoja na Mwinyi wanahitaji viongozi wa upinzani ili waweze kupeleka taifa mbele.

Waziri mkuu bila kutafuta njia ya kutubu na kusema wazi kabadilika itabidi atolewe kwa manufaa ya umma.

Hivyo anaweza kutafutia issue kama Spika Ndugai au tu Rais kufanya mabadiliko ya kawaida au anaweza kutubu na kujirudi kitu ambacho hajafanya mpapa sasa.

Mbowe kwa sasa ana nguvu kuliko Majaliwa. Na akiweka kichwa ngumu na kujifanya ni mzalendo yatamkuta ya Ndugai.

Namshauri awahi haraka sana kuweka msimamo wake wazi bila hivyo atapigwa chini kwani hatakuwa anasaidia nchi au chama
Kamundu! Bila shaka wewe ni mmojawao unaotumika au kujipigia debe. Be objective not subjective. Unakumbusha mambo yaliyopita ili iweje? Mh.Waziri Mkuu hana kosa gani hapo mgombea kama aliingia mitini? Leta ushahidi sio kutumiwa na wapenda madaraka. Mungu akusaidie uache chuki binafsi
 
Back
Top Bottom