Bila kupewa promo na Diamond Platinumz, Alikiba si chochote wala si lolote

Umeandika uongo wa Hali ya juu Sana, danganya watoto wa juzi kati Ila sisi tuliokuepo tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 pindi alikiba anatoka niseme tu wazi Alikiba hakuwahi kua msanii mkubwa wa kusifiwa na kuimbwa kama ilivotokea baada ya yeye kushindanishwa na Diamond na bila hivo hakuna ambaye angekua anamtaja hata!

Alikiba ni msanii mzuri huo ndo ukweli Ila kabla ya ujio wa Chibu hakuwahi kua kwenye trending kiasi hicho kama unabisha turudi miaka hiyo lini Alikiba alikua staa namba moja hapa bongo kabla ya diamond???

Ngoja nikukumbushe kitu kuanzia miaka ya 2000/10 alikiba hata asingeweza kutajwa katika wasanii watatu Bora wanafanya poa hapo walikuepo MB Doggy na Matonya ndo walitawala soko mwishoni mwishoni ndo akaja Marlow....

Lakini hicho kipindi Alikiba alikuepo na ndo alikua anatoa Ngoma nzuri Sana sasa jiulize ilikuaje akawa anachukuliwa kama msanii mzuri wa kawaida Ila baada ya lile bifu lake na diamond nazani ilikua 2014 hivo ndipo Alikiba alipata umaarufu ambao hata yeye mwenyewe hua anashangaa [emoji28]

Kama angekua Bora kiasi hicho basi angekuaga msanii Bora namba moja enzi zile Diamond hajatoka....

Kama kuna mtu kafaidika na ujio wa diamond basi ni Alikiba... Na hii ilisababishwa na chuki Tu za watu flani Kwa Diamond baada ya kuona jamaa anaanza kua mkubwa kuliko walivotaka...
 
Unajua kujenga hoja
 
Hapa ada wazazi wako wangeinywea bia
 
Ulitaka awe mkubwa namna gani Mtu anayechipukia?
Hakujawahi kuwa na Kitu kinachoitwa msanii "namba moja", na hakitakuja tokea. Kwani kila mtu ana masikio yake na analist yake.Ila kunaweza kuwepo Kundi la wasanii wenye wafuasi na mashabiki wengi.
Alikiba amekuwepo kwenye hili Kundi toka anaanza mpaka kesho.
Alikiba anamtegemea Mondi? Na mpo serious?
So ni Mondi aliandika Mac Muga, Single boy etc, mapenzi yanarun dunia etc?

Kama Cinderella haikuwa hit iliyosumbua tuambie basi ni ngoma ipi iliyosumbua.
Kama Alikiba wa Nakshi Nakshi na Mac Muga sio top tier, tuambie basi hao waliokuwa zaidi yake ni wangapi na ni kina nani.
 
Wewe unamzungumza Alikiba wa zamani uko wakati jamaa anazungumzia Alikiba baada ya kupumzika miaka 3 hivi nazani anazungumzia wa kuanzia 2014 n.k alivyorudi kwenye game ni ngumu kuelewana kati yenu
 
Wewe unamzungumza Alikiba wa zamani uko wakati jamaa anazungumzia Alikiba baada ya kupumzika miaka 3 hivi nazani anazungumzia wa kuanzia 2014 n.k alivyorudi kwenye game ni ngumu kuelewana kati yenu
Kwanini asimpe promo Ferouz, au Mwanae Dudu Baya why Alikiba?
Promo ingemsaidia sana Queen darlin au Lavalava.
 
Kwanini asimpe promo Ferouz, au Mwanae Dudu Baya why Alikiba?
Promo ingemsaidia sana Queen darlin au Lavalava.
Hajasema Alikiba ni msanii mbaya,ila anachozungumzia kwa kiasi kikubwa kiba amerudi kwenye game baada ya kushindanishwa na diamond maana baada ya kiba kupumzika msanii aliyekuwa kinara ni Diamond ila baada yakuja na promo ya bifu na diamond ikamfanya atengeneze attention na watu kumfuatilia
 
If alitoboa bila promo wakati anaanza sidhani kama anamtegemea mtu ili abaki relative.
Kama ni bifu na kushindanishwa, Angekuwa Mkubwa Bell 9, Dimpoz, na Bob junior. Maana hao wote walikuwa na Bifu na Mond na Halikuwasaidia chochote.
 
If alitoboa bila promo wakati anaanza sidhani kama anamtegemea mtu ili abaki relative.
Kama ni bifu na kushindanishwa, Angekuwa Mkubwa Bell 9, Dimpoz, na Bob junior. Maana hao wote walikuwa na Bifu na Mond na Halikuwasaidia chochote.
Wote hao uliowataja walifanya vizuri ila walidrop baada kutojihusisha na diamond kabisa kwenye ushindani. Ukitaka kujua hilo angalia kwa Harmonize pia. Alikiba unayemzungumzia wewe ni wa zamani nadhani wewe ni mwenga ndio alikuwa top ila baada ya kupumzika soko lake likadrop akarudi kupitia mgongo wa Diamond ambapo alikuwa yupo top kama unakubumbu vizuri ndio team za music zikaanza kuzaliwa na clouds media waliipromote sana hii bifu
 
Aisee kama ulikuwa upo kwenye mawazo yangu.

Hii mada ndio nilipanga niianzishe baada ya reply ya huyo jamaa.

Kwa kifupi Ali Kiba ameanza kutoka kwenye 2005 kama sio 2006 .

Miaka ya 2005 kushuka chini ,Juma Nature ndiye msanii aliyesumbua sana wakiwema akina Ferooz na crew nzima ya Daz nundaz kiujumla ,akina Dully Sykes ,Blue nk

2005-2008 hapa tunawapata akina Matonya ,Marlow ,Mb dog ,Z Anto,Noorah ,Suma lee nk
Ally Kiba alikuwepo ila hakuwa mkubwa kihivyo japo nyimbo zake baadhi zilifanya poa na akapotea kabisa

2009 -2010 hapa ilikuwa Diamond Platinumz anatoka toka pamoja na Bell 9.

2010- Hapa Diamond ,Rich Mavoko nk.

Ally Kiba anakuja kuibuka 2013 huko tena kupitia Diamond maana kipindi hicho wameshamshindanisha na wengi lakini wote walishindwa kufua dafu (Mf belle 9, rich Mavoko nk)
Kwa hiyo Kiba anakuja kuibuka kwa kupitia tu mgongo wa Diamond kama ilivyo hivi sasa walivyotaka kumshindanisha Diamond na Chino Kid.

Kiufupi Kiba bila Diamond hatoboi
 
Pia dulyskes alikuwa juu ya alikiba .hebu think
 
Jaribu na wewe uone mambo yalivyo magumu. Acha tu!!!
 
Hizo ngoma kipindi zinatoka kulikuwa na ngoma nyingine kali kuzidi hizo.
Mfano Bembeleza, Binti Kiziwi, Vaileth, Mbayuwayu, Mpenzi Jini, Si uliniambia nk.
 
chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…