Pre GE2025 Bila kura za Kanda ya Ziwa, CCM inaweza kubaki madarakani?

Pre GE2025 Bila kura za Kanda ya Ziwa, CCM inaweza kubaki madarakani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Biteko ana influence gani nje ya jimbo lake. Nani alimjua Biteko kanda ya ziwa, Shibuda alikuwa anajulikana kanda ya ziwa kushinda Biteko.

Shibuda alipokatwa CCM aliweza kulitetea jimbo lake nje ya CCM. Mwambie Biteko atoke CCM uone kama ana ushawishi wa kutetea jimbo lake nje ya CCM.

Hao watu hawana impact yeyote ndani ya CCM na watanzania wala hawana ubaguzi kwenye kura za taifa.

Magufuli hakuwa anapendwa kanda ya ziwa tu, bali Tanzania nzima.

Mengine ni kujijaza ujinga tu, kanda ya ziwa kama mikoa mingine aihitaji baraża la mawaziri lililojaa wasukuma kufanya maamuzi.

Kwanza ni kuwa dharau na kuwapa label ya ukabila ambayo haipo huko.

Ujakutana na wasukuma waliokuwa serikalini enzi za Magufuli (hawataki, hata kumsikia).

Mafisadi hayana dini, wala ukabila; na wananchi hawana dini wala ukabila kwenye maamuzi yao zaidi ya imani tu na mtu wakuwatatulia shida zao.

Mengine ni ujinga mtupu mnaojijaza vichwani kwenu tofauti na fikra za watanzania.
🌤️🙋‍♂️🎯✍️👍👏👊🤝👌🙏
 
Baada ya kifo cha Magufuli na Samia Suluhu Hassan kuanza kuachana na yule aliyemtengeneza, kumekuwa na juhudi za makusudi kwake na chama cha Mapinduzi kushikilia dola. Hata hivyo, wawili hawa wanajua kuwa bila ya kura za Kanda ya Ziwa, hakuna anayeweza kushika madaraka nchini.

Tokana na utendaji na ushawishi aliokuwa nao Magufuli, yeyote anayejitahidi kumweka kapuni ataishia mwenyewe. Kuepuka balaa hili, Samia alipinda katiba na kumteau Dotto Biteko kuwa naibu waziri mkuu cheo ambacho ni upotezaji wa fedha za umma mbali na kutokuwamo kwenye katiba.

Janja ya pili ni kumpa Stephen Wasira umakamu mwenyekiti wa CCM mbali na kuteua mawaziri kama Innocent Bashungwa na Stagomera Tax wanaotoka mikoa ya Mwanza na Kagera wakati Biteko anatoka Geita. Kwa vile mkoa wa Mara mmoja wa mikoa ya Kanda ya Ziwa haukuwa na waziri. Hivyo, wameamua kumpa umakamu mwenyekiti Wasira ili kuirubuni mikoa husika isiwapige kibuti.

Je hii janja itafanikiwa na kuiwezesha CCM kuendelea kushika dola mbali na uchakachuaji wa uchaguzi? Je hii janja itaepusha mgawanyiko ndani ya chama baada ya magwiji kama Makamba na Kinana kuonekana kujiweka mbali nayo?

Je janja hii itazima hasira za wale waliokuwa wakimuunga mkono Magufli walioutupwa nje ya ulaji?
Je bila Kanda ya Ziwa, ccm inaweza kuendelea kushikilia dola?

Je bila Kanda ya Ziwa, Samia anaweza kuwa rais tena baada ya kuupata kwa mkono wa Mungu?
Karibuni tujadili na kudadavua pamoja.
Kanda ya ziwa insonwspiga kura wangapi, weka namba hapa otherwise ni bla bla.
 
Mkuu ndio maana mnafeli mitihani kwa kutoelewa kilichoandikwa, wapi pameandikwa Magufuli ndie aliyemtengeneza huyo unayemsema? rudia tena kusoma ndio utajua aliyeandika anamaanisha mtu huyo uliyemuandika na sio Magu! Unakurupuka na mambo ya ukabila wakati hata andiko hujalielewa.
usi mind mkuu ukiona mkurupuko wowote au hasira yoyote juu ya hili andko jua n mccm tu uyo
 
Labda kama sijaelewa ni makamba yupi huyo uliyeandika "Magwiji kama Makamba"

Yaani gwiji wa siasa za Tanzania awe Makamba ni yupi yule bwana mdogo au mzee wa kutengwa?.
 
Kwa uchaguzi halisi kabisa ambao mshindi anapatikana kwa kura halali toka kwa wapiga kura hakuna chama kinaweza kutoboa bila kuungwa mkono na kanda ya ziwa. Lakini CCM hii haitegemei tena kura kujitangaza kuwa imeshinda ushindi wa kishindo kwa 99%. CCM siyo chama cha siasa tena bali ni chama dola. Kwa Tume hii na sheria hizi na Katiba hii inayotoa kinga kwa wezi wa kura kwa ibara inayosema mgombea wa Urais akishatangazwa na mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi kuwa ameshinda hakuna mamlaka yoyote inayoweza kuhoji ni dhahiri CCM haiwezi kuondoka madarakani kwa njia ya sanduku la kura.
 
Baada ya kifo cha Magufuli na Samia Suluhu Hassan kuanza kuachana na yule aliyemtengeneza, kumekuwa na juhudi za makusudi kwake na chama cha Mapinduzi kushikilia dola. Hata hivyo, wawili hawa wanajua kuwa bila ya kura za Kanda ya Ziwa, hakuna anayeweza kushika madaraka nchini.

Tokana na utendaji na ushawishi aliokuwa nao Magufuli, yeyote anayejitahidi kumweka kapuni ataishia mwenyewe. Kuepuka balaa hili, Samia alipinda katiba na kumteau Dotto Biteko kuwa naibu waziri mkuu cheo ambacho ni upotezaji wa fedha za umma mbali na kutokuwamo kwenye katiba.

Janja ya pili ni kumpa Stephen Wasira umakamu mwenyekiti wa CCM mbali na kuteua mawaziri kama Innocent Bashungwa na Stagomera Tax wanaotoka mikoa ya Mwanza na Kagera wakati Biteko anatoka Geita. Kwa vile mkoa wa Mara mmoja wa mikoa ya Kanda ya Ziwa haukuwa na waziri. Hivyo, wameamua kumpa umakamu mwenyekiti Wasira ili kuirubuni mikoa husika isiwapige kibuti.

Je hii janja itafanikiwa na kuiwezesha CCM kuendelea kushika dola mbali na uchakachuaji wa uchaguzi? Je hii janja itaepusha mgawanyiko ndani ya chama baada ya magwiji kama Makamba na Kinana kuonekana kujiweka mbali nayo?

Je janja hii itazima hasira za wale waliokuwa wakimuunga mkono Magufli walioutupwa nje ya ulaji?
Je bila Kanda ya Ziwa, ccm inaweza kuendelea kushikilia dola?

Je bila Kanda ya Ziwa, Samia anaweza kuwa rais tena baada ya kuupata kwa mkono wa Mungu?
Karibuni tujadili na kudadavua pamoja.
Acha ukabila na ukanda hautakusaidia lolote.
 
Acha ukabila na ukanda hautakusaidia lolote.
Acha unafiki kujifanya hakuna ukabila wakati upo. Mlizoea kumtuhumu Magufuli kupendela kanda ya ziwa sawa na ambavyo Samia sasa anapendelea Visiwani. Mnadhani hatuoni?
 
Back
Top Bottom