Siyo kweli...
Cc:
Mahondaw
Hili ni kweli maana hata vibaka, wezi, majambazi wengi wamejificha ktk shughuli ya boda boda, mchana anasukuma chuma, usiku anakaba.
Baadhi yao baada ya kupata/kutosheka na pesa za boda huacha hiyo tabia ya wizi/ukabaji na wengine hawaachi bali wanapumzika tu, wakikosa pesa kwa siku kadhaa wanaingia mzigoni.
Bodaboda ni aina ya ajira ya kipuuzi kwa nchi ya Tanzania, inafuga na kuwalea wajinga na wapumbavu wasiojali maisha yao na maisha ya watu wengine.
Inawezekana vipi mtu hajali usalama wake anaendesha chombo kwa speed kubwa as if ana spair ya maisha?, huyu huyu hajali maisha ya wapita njia/waendesha vyombo vya moto njiani, yeye anajali kukimbia tu.
Kuna namna hawa watu wa boda boda ilitakiwa kabla ya kujiingiza humo, wapimwe akili, wapewe shule ya usalama wa kuendesha vyombo vya moto, mafunzo marefu yenye vikwazo vigumu kwa wazembe.
Tutaendelea kuwafuga majizi na majambazi tusipobadili huu mfumo