Bila Magufuli tungesalimika magonjwa na chanjo zinazoendelea duniani?

Bila Magufuli tungesalimika magonjwa na chanjo zinazoendelea duniani?

Dokta Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2022
Posts
1,370
Reaction score
3,152
Bila ungangari wa kile chuma, tusingesalimika na maigizo yanayoendelea duniani ya magonjwa na machanjo ya ajabu ajabu.

Mara corona, mara sijui monkeypox, mara nini!

Kwa misingi ile ya ungangari aliyoiweka, hata aliyemfuatia anaogopa kufanya jambo la kipuuzi kwa kuhofia kusutwa na wananchi waliozielewa zile falsafa.

Yale machanjo siku hizi siyasikii, sijui wameyafukia wapi?

Wakati wa corona, Kila mtu alijificha uvunguni akichungulia kwenye kitobo akihofia kunyukwa na mabeberu, lakini yule mzee hakuogopa lolote licha ya kushambuliwa kila kona na vibaraka waliopewa vibiskuti.

Najua kuna wale vinyamkera wachache wasio na elimu watakuja hapa kumwaga mitusi bila tafakuri.

Nchi ilisalimika kwenye vifungo vya lockdowns na machanjo ya hovyo hovyo kwa sababu ya Magufuli.

Mpaka sasa tunaenda vizuri kwa sababu ya misingi hiyo ya UTAMBUZI.

Machanjo yamepotelea kusikojulikana.

Uzalendo. Uthubutu. Uhodari.
 
Misimamo yake imetusaidia kutoathirika sana, Hofu inaua zaidi kuliko hali halisi. Wale ukipingana nao lazima wakumalize. Wao ndio upanga duniani iendaje.
Ishu ya corona ilikuwa ni kutest mitambo ya 666.
Wewe na marehemu magufuli mna walau chanjo 12
 
Mleta mada acha upunguani wako na ujinga ulipitiliza!
Unajua tulipoteza ndugu zetu wengi kwa ujinga na ulimbukeni wa huyu mtu wenu?
Unajua tungelichukua hatua kama wenzetu tusingepoteza watu wengi kiasi kile?
Unajua kuna nyumba watoto wamebaki yatima kwa ugonjwa ule?
Halafu bila aibu unasema eti 'bila kile chuma' sasa 'chuma' chenu kimeliwa na kutu! pambaf!
 
Nilipoteza ndugu zangu walichelewa kupata j&j kisa mtu alikua ana wadanganya wafukize na kutukana masister kanisani walio vaa barakoa. Sasa mtu kavaa barakoa hata kama kunge kua hamna ugonjwa wewe ina kuhusu namna gani?
Hata akina Ben Mkapa, Agustino Mahiga, John Kijazi, Lwakatare, Ndassa, Maalim Seif ni hiyo hiyo COVID 19 ndiyo iliyowaua.

Jamii ya Kitanzania ilivyo illiterate eti wanampongeza kwa uzembe huu! Serious??
 
Back
Top Bottom