Bila malaria wazungu wangetuangamiza na kukaa Afrika

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Kila sehemu walikoenda, lengo kuu la wazungu ilikuwa na kuanzisha makazi napya na kuangamiza jamii ya hapo.

Wamewaangamiza wa Aborigines wa Australia hadi wamebaki wa kuhesabu. Huko Amerika wamewaangamiza Wahindi Wekundu na leo Wahindi Wekundu ni wa kuhesabu hapa na pale.

Walitumia magonjwa na silaha. Mfano , huko Amerika kulikuwa hakuna mahonjwa kama typhoid, ndui, magonjwa fulani ya zinaa nk. Walivyoingia wakapeleka ndui, typhoid nk. Wahindi Wekundu walikufa kama kumbikumbi. Leo asilimia kubwa ya bara lile ni wazungu.

Kwetu Afrika walikuwa na lengo hilohilo lakini walishindwa sababu ya magonjwa ya kitropiki, hasa Malaria. Muafrika amejenga kinga ya malaria miaka na miaka lakini mzungu ilimuua kirahisi sana. Wale waliojaribu kuweka makazi ya kudumu walishindwa sababu ya malaria.

Nafikiri tuna sababu ya kuushukuru huu ugonjwa.
 
Hivi wanavokuja kutalii wakiamua kuleta maradhi hatari zaidi ya hiyo malaria watashindwa?

Usiendelee kutuaminisha hicho inachotaka tuamini
 
Hivi kwani walisema wameshindwa kuiangamiza malaria?
 
Wazungu hawajaisha bado tunao wazungu weusi wanaotutesa kila kukicha kwa pesa zetu wenyewe
 
Kila sehemu walikoenda, lengo kuu la wazungu ilikuwa na kuanzisha makazi napya na kuangamiza jamii ya hapo.

Wamewaangamiza wa Aborigines wa Australia hadi wamebaki wa kuhesabu. Huko Amerika wamewaangamiza Wahindi Wekundu na leo Wahindi Wekundu ni wa kuhesabu hapa na pale.

Walitumia magonjwa na silaha. Mfano , huko Amerika kulikuwa hakuna mahonjwa kama typhoid, ndui, magonjwa fulani ya zinaa nk. Walivyoingia wakapeleka ndui, typhoid nk. Wahindi Wekundu walikufa kama kumbikumbi. Leo asilimia kubwa ya bara lile ni wazungu.

Kwetu Afrika walikuwa na lengo hilohilo lakini walishindwa sababu ya magonjwa ya kitropiki, hasa Malaria. Muafrika amejenga kinga ya malaria miaka na miaka lakini mzungu ilimuua kirahisi sana. Wale waliojaribu kuweka makazi ya kudumu walishindwa sababu ya malaria.

Nafikiri tuna sababu ya kuushukuru huu ugonjwa.
Hoja mfu, za kinyonge, zisizo na mashiko,za woga, udhaifu,unafiki,ukosefu wa deep thinking n.k na ndo maana miaka na miaka waafrika hatuendelei sababu ya kuendelea kuwa na fikra kama hizi.
 
Back
Top Bottom