Mchochezi
JF-Expert Member
- Feb 29, 2012
- 10,962
- 7,830
Mechi ya kwanza tatizo lilikuwa na utoto wa Neymar Jr kupiga chenga zisizo na faida kwenye timu naa kuigharimu timu yake. Ila kwa leo kwa kuwa hayupo, nina imani asilimia 90, nafasi yake akipangwa winga machachari Angel Di Maria, halafu asaidiane na Mbappe na Edinson Cavani basi leo Bingwa Mtetezi Madrid anatolewa mapema tu.
Pale kwenye idara ya kiungo kuna umuhimu wa kuanza kwa mkongwe Thiago Motta kama kiungo mkabaji ili kutoa fursa kwa Kiungo mshambulizi Marco Verratti kusogea mbele akishirikiana na bwana mdogo Adrien Rabiot.
Pia Mwalimu Unai Emery ili anogeshe furaha ya Ushindi leo hana budi kumpa nafasi kiongozi na nahodha Thiago Silva asaidieane na Marquinhos, hakika Real Madrid atakufa mapema tu tena 3-0.
Tukutane Saa 4:45 Usiku kwa majira ya Afrika Mashariki na Kati!!