Mechi ya kwanza tatizo lilikuwa na utoto wa
Neymar Jr kupiga chenga zisizo na faida kwenye timu naa kuigharimu timu yake. Ila kwa leo kwa kuwa hayupo, nina imani asilimia 90, nafasi yake akipangwa winga machachari
Angel Di Maria, halafu asaidiane na
Mbappe na
Edinson Cavani basi leo Bingwa Mtetezi Madrid anatolewa mapema tu.
Pale kwenye idara ya kiungo kuna umuhimu wa kuanza kwa mkongwe
Thiago Motta kama kiungo mkabaji ili kutoa fursa kwa Kiungo mshambulizi
Marco Verratti kusogea mbele akishirikiana na bwana mdogo
Adrien Rabiot.
Pia Mwalimu
Unai Emery ili anogeshe furaha ya Ushindi leo hana budi kumpa nafasi kiongozi na nahodha
Thiago Silva asaidieane na
Marquinhos, hakika Real Madrid atakufa mapema tu tena
3-0.
Tukutane
Saa 4:45 Usiku kwa majira ya Afrika Mashariki na Kati!!