Bila Neymar Jr, PSG anamtoa Real Madrid mapema tu!!

Mchochezi

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Posts
10,962
Reaction score
7,830
Mechi ya kwanza tatizo lilikuwa na utoto wa Neymar Jr kupiga chenga zisizo na faida kwenye timu naa kuigharimu timu yake. Ila kwa leo kwa kuwa hayupo, nina imani asilimia 90, nafasi yake akipangwa winga machachari Angel Di Maria, halafu asaidiane na Mbappe na Edinson Cavani basi leo Bingwa Mtetezi Madrid anatolewa mapema tu.

Pale kwenye idara ya kiungo kuna umuhimu wa kuanza kwa mkongwe Thiago Motta kama kiungo mkabaji ili kutoa fursa kwa Kiungo mshambulizi Marco Verratti kusogea mbele akishirikiana na bwana mdogo Adrien Rabiot.

Pia Mwalimu Unai Emery ili anogeshe furaha ya Ushindi leo hana budi kumpa nafasi kiongozi na nahodha Thiago Silva asaidieane na Marquinhos, hakika Real Madrid atakufa mapema tu tena 3-0.


Tukutane Saa 4:45 Usiku kwa majira ya Afrika Mashariki na Kati!!
 


Daaah mbinu za ukweli kabisa hizi,lakini tatizo CR7 lazima avizie afunge angalau kimoja ndio shida itakapoanzia hapo.
 
Tatizo ni Real inafungika ila haikwepeki, nyavu zako watagusa tu, mechi itaisha kwa Madrid kusonga kwa advantage ya away goals.
 
FT RMADRID 2-0

[HASHTAG]#STAKEURGFRIEND[/HASHTAG]
 
UNGEPENDA TIMU ZA NCHINI KWAKO KAMA HIVI LOH
 
Katika mafanikio ya PSG 2017/2018 Huwezi kumtoa Neymar watu wakakuelewa,PSG kupoteza mechi ya kwanza ilikuwa ni uzembe wa defense kujiamini kupita kiasi na kufanya makosa ya kijinga.Neymar ni kweli hakucheza vizuri mechi ya kwanza,ila siyo Guarantee kwamba hata Leo atacheza hivyo hivyo,Wachezaji wote wakubwa duniani siyo kila mechi huwa wanacheza vizuri,Siyo CR7 wala Messi wote kuna mechi huwa wanacheza vyongo utadhani hawapo uwanjani.Neymar bado ni mchezaji wa kutegemewa PSG.Tizama statistics zake hapo chini then unambie unaweza vipi kusema asipkuwepo timu ina uhakika wa kushinda.Labda tuongee kinazi.
https://www.whoscored.com/Players/50835/Show/Neymar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…