Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
BILA SHERIA ZA DINI HAYA YANGEFANYIKA, JE BADO UNAAMINI SHERIA ZILIONDOLEWA?
Kwa Mkono wa, Robert Heriel.
Moja ya vipengele nyeti katika Utamaduni ni Dini.
Dini ni utamaduni unaojifungamanisha na masuala ya miungu kulingana na jamii husika. Kila jamii mungu wake, ikiwa ni hivyo mungu huyo ametoa utaratibu wake, utaratibu huo ndio huitwa Dini. Yaani taratibu au kanuni au njia za kumfikia mungu wa jamii husika.
Elimu ya tamaduni ni muhimu Sana. Mtu yeyote anayeelezea habari za Dini anapaswa awe na elimu isiyo na Shaka ya masuala ya tamaduni. Ni sharti mtu anapoeleza habari za Dini aelewe na amueleweshe msikilizaji habari za utamaduni wa jamii husika yenye mungu huyo. Hata hivyo Taikon anafahamu kuwa dunia inajamii nyingi kumaanisha inamiungu mingi vilevile, ingawaje IPO miungu inaingiliana kimfanano na kiutamaduni Kama ilivyo Kwa baadhi ya jamii kukaribiana kimila na kidesturi.
Leo sitaandkka Sana, nimeandika haya ili kuweka mambo Sawa baada ya kuona upotoshaji unazidi kuwa mkubwa ndani ya jamii.
Kuna tofauti kubwa ya Miiko na Dini, miiko ni mapokeo ambayo kila jamii hujiundia kulingana na sababu mbalimbali.
Miiko haiingiliani na Masuala ya sheria za miungu ingawaje zipo jamii zimeweza kuchukua sehemu ya sheria za miungu na kuiweka kwenye miiko.
Pia zipo jamii huchukua miiko na kuifanya kuwa kama sheria za miungu Jambo ambalo sio sahihi.
Mfano, ni mwiko Kwa jamii nyingi za binadamu Kwa mwanamke kuongoza au kuhusika na mambo ya utawala.
Jamii za mashariki ya Kati kama Wayahudi na waarabu MWIKO huu umedumu Kwa miaka mingi. Sio ajabu mwiko huu uliingizwa kwenye Sheria za miungu(dini) kuwa mwanamke asiongoze au asipewe nafasi ya kuendesha Ibada. Ila kimsingi sheria nyingi za miungu haielezi hivyo.
Miiko inabadilika kulingana na nyakati lakini sheria za miungu haibadiliki kulingana na nyakati. Sheria za miungu haibadiliki.
Miungu yenye sheria za kubadilika wanakosa sifa ya kuitwa mungu kwani sifa kuu ya mungu ni kutokubadilika kwani aliumba mwanzo akiwa mwisho, hivyo anajua mwisho kabla ya Mwanzo.
Watu wanaosema sheria za miungu iliondolewa ni watu wanaojaribu Kueleza kuwa wanauelewa mdogo WA mambo ya elimu ya Dini. Au wanafanya hivyo makusudi Kwa maslahi Yao wenyewe. Nani ajuaye!
Pasipo sheria ya Dini(sheria za miungu); haya yangefanyika pasipo shida yoyote:
1. Wanadamu wangekulana nyama na wala isingekuwa tatizo.
Mtu anayesema sheria za miungu imefutwa anajaribu Kueleza kuwa anaouwezo wa Kula nyama ya mtu/binadamu mwenzake.
2. Kufanya mapenzi na Mama au Baba yako, au mtoto wako.
Mtu anayesema sheria imefutwa anajaribu Kueleza kuwa anaouwezo wa kutoka na Mama yake mzazi, au Baba yake mzazi, au anauwezo WA kulala na Mwanaume mwenzake, au mwanamke mwenzake kimapenzi.
Anajaribu Kueleza kuwa Anauwezo kuwa kumlawiti mtoto wake wankumzaa pasipo shida yoyote.
Kufanya mapenzi na Mama au Baba Mkwe.
Kufanya mapenzi na mume au mke WA mtoto wako.
3. Kufanya ngono WA wanyama.
4. Kuua tuu mtu unavyojisikia
5. Kuiba, kudhulumu, kufisadi miongoni mwa mambo mengine.
Jambo moja la uhakika ni kuwa moja ya vitu ambavyo miungu haiviwezi kuviondoa ni sheria.
Kuondoa sheria ni kumuondoa huyo mungu mwenyewe kwani mungu ndio hiyo sheria.
ukisikia mungu kajiua basi ndio kaondoa sheria. Sheria ndio mungu mwenyewe, ndio utambulisho wa miungu.
Kusema sheria zimeondolewa ni kusema mungu kaondolewa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Kibiti, Pwani