figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,132
- 64,416
Jana nimekutana na balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe, Suzan S. Kaganda hazina ya Taifa.
Baada ya kumsikiliza vizuri, nimeamini kumbe Nchi yetu bado ina Wazalendo. Tatizo Wazalendo CCM hawataki wakae karibu na Wananchi. Mfano Balozi Polepole alipelekwa Cuba, Balozi Suzan kapelekwa and Zimbabwe.
Polisi wanaongoonzwa wa Wambura🤣🤣🤣 Wakati tuna Polisi Msomi huko Zimbabwe.
Kwanini Samia hataki kumpa Ukuu wa Polisi? Kwanini anang'ang'ania wakina Wambura wasio na elimu ya wasio jali utu.
Kama angekuwa Suzan, 29.10.2025 Watu waaingekufa.
Nakumbuka ndo alizuia jaribio la Nape Nauye kutekwa Dar. Es Salaam. Siku nape Nnauye anatishiwa Bastola, Suzan Ndo aliingilia kati japo tu hawasemi.
Sisi tulikuwa tunamsubiri Nape aje kuongea na Wanahabari, Tukasikia Nje ya Geti anapiga Kelele kwamba "Nisaidieni Natekwa'. Tulikuwa Oyster bay mbele kwenye Ukimbi wa Protea Hotel mbele ya kanisa la RC. Maulid Kitenge akazuia.. Lakini hawakuacha.. Hadi alipokuja Suzan, kipindi hicho alikuwa ndo Bosi wa Polisi Kinondoni.
Aliwauliza Swali dogo.. Alisema nanukuu, "Tuna taarifa za Nape Nnauye kuja kufanya Mkutano hapa, Mbona hatuna taarifa za ninyi kuja kumkamata? Wale wasiojulikana wakawaka Gari wakaondoka. Tangia hapo namheshimu.
Nape akamuambia Suzan, Dhahabu haiwi dhahabu hadi ipite kwenye moto, na Mbegu haioti hadi ifukiwe ioze. Bila Kaganda kuwa IGP tusikubali Maridhiano.
Hii ni Dibaji
Katikati ni dada wa taifa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan S. Kaganda, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Hakimiliki na Haki Shirikishi, Bi. Maureen Fondo na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Utafutaji na Uchunguzi, Bw. Said Ramadhan
Sasa jana Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. Suzan S. Kaganda, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Shirika la Kikanda la Haki Miliki Afrika (African Regional Intellectual Property Organization – ARIPO) lenye ofisi zake mjini Harare, Zimbambwe.
Wawakilishi hao ni Mkuu wa Kitengo cha Hakimiliki na Haki Shirikishi, Bi. Maureen Fondo pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Utafutaji na Uchunguzi, Bw. Said Ramadhan, ambao wote ni raia wa Tanzania wanaofanyakazi katika taasisi hiyo ya kikanda. Mimi wallinikuta pale nimeenda kufuatilia mambo yangu kwa Boss Kaganda.
Wawakilishi hao walifika Ubalozini kwa lengo la kujitambulisha kwa Mheshimiwa Balozi Kaganda pamoja na kulitambulisha shirika hilo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku na kuimarisha ushirikiano wa kikazi.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Balozi Kaganda aliwapongeza kwa mchango wao katika shirika hilo, akisisitiza kuwa uwepo wao unasaidia kuitangaza Tanzania kimataifa pamoja na kuhakikisha maslahi ya nchi yanalindwa na kupewa kipaumbele katika taasisi na mashirika ya kimataifa yanayoshughulikia masuala ya haki miliki na ubunifu.
Aidha, wawakilishi hao waliishukuru Ofisi ya Ubalozi kwa ushirikiano mzuri, wakieleza kuwa shirika hilo lilianzishwa kufuatia makubaliano yaliyofikiwa mwaka 1976 katika mji wa Lusaka, kupitia Makubaliano ya Lusaka ya tarehe 9 Desemba 1976.
Waliongeza kuwa taasisi hiyo inalenga kusimamia na kuratibu masuala ya haki miliki na ubunifu kwa nchi 22 wanachama, ikiwemo Tanzania, kwa lengo la kuhamasisha ubunifu, kulinda haki za wabunifu na kuchochea maendeleo ya kiuchumi barani Afrika.