Bila U-Sri Lanka ama kuchapana kamwe Katiba Mpya iliyo bora haitapatikana

Bila U-Sri Lanka ama kuchapana kamwe Katiba Mpya iliyo bora haitapatikana

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Katiba bora ni ile inayotoa fursa sawa kwa vyama vya siasa na raia wake kwa ujumla na yenye kumuwajibisha kila anayeikiuka.

Hapa nchini kuna vuguvugu la kutaka kuandikwa kwa katiba mpya. Lakini katiba itakayoandikwa kwa mazingira na mwenendo tulionao sasa itakuwa siyo bora.

Itakuwa siyo bora kwa sababu hakuna mashinikizo kutoka ndani ya dhamira za viongozi na jamii kwa ujumla ya kutunga katiba bora.

Nijuavyo mm umma ukiamka toka usingizini, ukaanza kudai haki za kikatiba mpk kupelekea mapinduzi kama yale ya Sri Lanka, ama machafuko ya kuchapana kama yale ya Kenya, hapo ndipo katiba bora itaandikwa.

Kitakachofanyika sasa itakuwa ni kuandika katiba ambayo kwa vyovyote vile itakifanya chama tawala kiendelee kuneemeka kwa mamlaka ya kidola. Siyo rahisi kuruhusu Neema hii iondolewe na katiba mpya.
 
Uko sahihi kabisa, hii katiba ya kupatikana katika mazingira ya kukimbeleza chama kilichoko madarakani kwa sababu za kihistoria, na wizi wa kura, ni kupotezeana muda.

Ndio maana wanaweza kuongea kwa jeuri kwa kusema kuwa iwapo katiba hii haifuatwi, tuna uhakika gani katiba hiyo mpya itafuatwa? Wanasema kwa jeuri kuwa wananchi hawataki katiba mpya bali maendeleo!

Mambo mengi ya msingi yaliyomo kwenye rasimu ya Warioba, ambayo ni maoni halali ya wananchi, vifungu vingi vimeondolewa maana havina maslahi kwa chama kilichoko madarakani kwa sababu za kihistoria.

Kwa vyovyote vile katiba mpya itaingiza vifungu vya kukilinda chama tawala na mianya yake ya kubaki madarakani kwa shuruti.

Kama tunataka kweli katiba mpya ya wananchi ni aidha yatokee machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi au ya aina nyingine.
 
Uko sahihi kabisa, hii katiba ya kupatikana katika mazingira ya kukimbeleza chama kilichoko madarakani kwa sababu za kihistoria, na wizi wa kura, ni kupotezeana muda...
Tunakokwenda yote yanawezekana, kama watesi wa wananchi au watesi wa wapinzani ndio wanaonwa wenye utumishi wa kutukuka tutegemee nini 🤔
 
Tinakokwenda yote yanawezekana,kama watesi wa wananchi au watesi wa wapinzani ndio wanaonwa wenye utumishi wa kutukuka tutegemee nini 🤔

Kwasasa bado wananchi ni waoga, lakini itafika point kitaeleweka. Wangalau wanajeshi majasiri kama wapo wanaweza kutukwamua kwa sasa.
 
Miaka 10 iliyopita ilitakiwa Wananchi waonekane waelewa kwa kukataa kina Magufuli na kuchagua kina Zitto, Halima Mdee, Dr Slaa, Kafulila n.k ambao leo nyie nyie mnawaona hawafai kwa kuwa ni wabinafsi,n.k
Waelewa ambao maamuzi yoyote ya viongozi hata ya hovyo yanapita na hawathubutu kupinga zaidi ya kulalamika? Tufanye ni waelewa, lakini waliojaa ukondoo mwingi.
 
Miaka 10 iliyopita ilitakiwa Wananchi waonekane waelewa kwa kukataa kina Magufuli na kuchagua kina Zitto, Halima Mdee, Dr Slaa, Kafulila n.k ambao leo nyie nyie mnawaona hawafai kwa kuwa ni wabinafsi,n.k

Kwani viongozi wa nchi hii wanachaguliwa na wananchi? Ingekua viongozi wa nchi hii wanachaguliwa na wananchi, CCM isingekuwa madarakani leo hii.
 
Hii mada ni kama vile muanzishaji na wanao comment ni mtu mmoja mwenye IDs tofauti. Upuuzi mtupu.
 
Siku vyombo vya ulinzi na usalama vitakapokuwa upande wa wananchi siku hiyo hiyo katiba inakuwa imeandikwa.
 
hivi Chama ambacho ndani ya miaka michache kimesalitiwa na Wagombea Urais wawili ( Slaa na Lowassa)

Makamu Mwenyekiti (Prof Safari)

Makatibu wakuu watatu ( Slaa, Kaburu na Mashinji)

Mwenyekiti wa Bavicha Taifa ( Patrobas)

Mwenyekiti na Katibu wa Bawacha ( Mdee na Hanje)

Wabunge kadhaa na Madiwani kadhaa

bado kitalaumu kwa kutopewa nchi ?

kama wana sifa ya kununulika si hatare

Yaan Makamu mwenyekiti kasaliti, Mgombea urais kasaliti, Katibu na Naibu wamesaliti, Bavicha wamesaliti, Bawacha wamesaliti

yaan safu yote wamesaliti kasoro mwenyekiti yeye kaamua kulamba asali bila ya kuisaliti waziwazi
Kwani viongozi wa nchi hii wanachaguliwa na wananchi? Ingekua viongozi wa nchi hii wanachaguliwa na wananchi, CCM isingekuwa madarakani leo hii.
 
hivi Chama ambacho ndani ya miaka michache kimesalitiwa na Wagombea Urais wawili ( Slaa na Lowassa)

Makamu Mwenyekiti (Prof Safari)...
Kama hao COVID 19 ni mtaji wakisiasa Kwa chama Dola kijiandae vilevile kusalitiwa. Hakuna urafiki wa kudumu kisiasa isipokuwa masilahi ya kudumu.Hao viwavi na wazalendo ndani ya chama Dola watatumika kuiangusha CCM.
 
hivi Chama ambacho ndani ya miaka michache kimesalitiwa na Wagombea Urais wawili ( Slaa na Lowassa)

Makamu Mwenyekiti (Prof Safari)....
Hahaha. Vijana washanyweshwa maji ya uchawa, kamwe hawawezi kukuelewa, japo wanafahamu vizuri kuwa mwenyekiti wao amelamba asali wazi wazi tena mchana kweupee.
 
Tunaandika KATIBA mpya bila maandamano.

Nchi hii usifananishe na hizo ulotaja, hii ni ya kipekee.

RASIMU alosimamia Judge WARIOBA irudi mezani mjadala uanzie hapo.

Arudishwe Mzee wetu Kwa Tume amalizie KAZI aliyoianza.

Ameeeen
 
hivi Chama ambacho ndani ya miaka michache kimesalitiwa na Wagombea Urais wawili ( Slaa na Lowassa)

Makamu Mwenyekiti (Prof Safari)...

Wataacha kusaliti wakati hawakuwa na uwezo wa kuvumilia mateso hadi mwisho? Wanasaliti lakini hawaondoki na wafuasi.

Inshort wao hawakuwa mabadiliko bali sehemu tu ya wataka mabadiliko. Ni juu yako kujiuliza kwanini nguvu kubwa ya dola imetumika kuhakikisha inawapata baadhi ya hao watu toka chama chenye ushawishi wa kweli kwa wananchi?
 
Tunaandika KATIBA mpya bila maandamano.

Nchi hii usifananishe na hizo ulotaja, hii ni ya kipekee.

RASIMU alosimamia Judge WARIOBA irudi mezani mjadala uanzie hapo.

Arudishwe Mzee wetu Kwa Tume amalizie KAZI aliyoianza.

Ameeeen
Katiba uchwara itaandikwa, na wala siyo katiba bora
 
Katiba uchwara itaandikwa, na wala siyo katiba bora
Kundi dogo tu la walokiteka chama kile kilichoanzishwa ktk msingi wa mwl Nyerere ndo wazito sababu ya kuhofia kupokwa madaraka.

Sheria zote na hila kandamizi hazitozuia kusudi la Mungu juu ya Tanzania kutimia.

Ninaiona Tanzania nzuri, TAJIRI, kimbilio la mataifa mengi siku Si nyingi. Naipenda Nchi yangu TANZANIA.

Ameeeen.
 
Walamba asali watatembeza virungu na risasi zinazopinda kona na kuwatupa mabwe pande kwenye viroba
 
Back
Top Bottom