Bila umakini itachukuwa muda mrefu na inaweza ikawa mrefu sana kwa upinzani kuiondoa CCM madarakani

Bila umakini itachukuwa muda mrefu na inaweza ikawa mrefu sana kwa upinzani kuiondoa CCM madarakani

Gerald .M Magembe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2013
Posts
2,495
Reaction score
1,803
Wana Bodi leo ninakuja na uzi fikirishi kwa kupinga dhana ya kuiondoa madarakani kiuwepese wepesi na kimzaha mzaha bila kuwa na strategic Movement ambayo itakuwa na proper focus ya kitu gani kinatakiwa kufanyika kuweza kufikia hilo lengo.

Kwanza upinzani bado wengi wao hawajatambua kuwa CCM ni chama bora katika Africa, na haya sio maneneno ya WanaCCM , Ni maelezo yanayo tolewa na wachambuzi wakubwa wa masuala ya kisiasa Duniani ambao wamepata nafasi yya kui study CCM.

Upinzani unataka kuiondoa CCM kwa uanaharakati bila kuimarisha vyama vya upinzani na kuwa na mikakati ya utekelezaji.

CCM ndio chama pekee Afrika ambacho ni Political Party na ni Political Movement kwa wakati mmoja. Kwa misingi hiyo ni chama kinachoweza kujibadili badili kufuatana na wakati na kiwango cha upinzani wanao kumbana nao.

Baada ya uchaguzi mkuu wa 2020, CCM ndio kitakuwa chama chenye wabunge vijana kuliko chama chocho Duniani, sababu asili mia 80% ya wabunge watakuwa ni vijana ikiwa na maana wabunge wake watakuwa chini ya ya Umri wa miaka 40. ( soma kwa umakini jedwali la wabunge waliopitishwa na CCM kugombea)

Kitakuwa chama chenye kila character, kutoka kila pembe ya nchi, kila dini, profession mbali mbali, uzoefu wa kutenda kazi wa viwango mbali mbali, Aghalabu kuwa na ndugu wawili katika uongozi labda Mama Kikwete na Ridhi moko, Kitakuwa na wabunge asili mia 25% ya au kizazi cha pili au cha tatu cha wafia chama. Kizazi ambacho kiko tayari kwa lolote kwa chama chao.

Kitakuwa na hazina ya uongozi wa kila namna katika ngazi karibu zote za utendaji na uwakilishi. Wa wana CCM walio kitumikia chama kwa muda mrefu zamani na wanao aminika.

Chama kilicho undwa kwa ubora kina kila uwezekano wa kuleta viongozi bora.

Jee upinzani unakuwa na tafakuri ya kina hili, tusichangie kwa Utopolo, tujitahidi kuweza kudurusu kila ukweli ambao tunaweza kuubadili kuwa ngao japo kwao wao wataona kama ni silaha. Kuchukulia upinzani utashinda utashinda bila kuwa na fact ndio mwanzo wa kupotea. Jua nguvu za adui yako na utaweza kumshinda kwa kuwa utatumia silaha ambazo zitavunja nguvu zake.

Kuna hali ya kujidanganya kuwa upinzani ndio wenye akili bora na waliofanikiwa. HII SIO KWELI KABISA, TUJITAHIDI KUSOMA KILA HATUA YA KIUONGOZI NA UCHAGUZI.

Ninaona kampeni nzoto na michango inayofanywa huku Kilimanjaro katika uchaguzi huu, na msishangae kwa lolote lile ndio maana Mwamba yupo kimya kazi ni kubwa na sio lele mama.

Nawasilisha nisiwachoshe.
 
Mkuu huwezi kuwaambia chadomo humu wakakulewa! , walishaziba masikio ! Wao wanaamini TL wao atakua Rais wa nchi hii sijui kwa mikakati ipi ! Majimboni wapo hoi bin taaban!
 
As long as wewe ni verified user, lazima uandike ujinga! Sijasoma na siwezi kwa sababu ukiandika ukweli wake , unafuatwa, lazima uandike utopolo
 
Acha uwoga mkuu. Hakuna strategy ama movements zozote ndani ya ccm zaidi ya kutegemea vyombo vya dola na uchafuzi wa uchaguzi.

Uzi wako na vitisho vyako kwamba Kuna kampeni za maana zinafanywa Kilimanjaro, vingekuwa na maana kama ccm wasingekuwa wanaliogopa sanduku la kura.
 
Back
Top Bottom