Hakika hili la Chenge linashangaza na kuaibisha sana! Hivi wakuu mwajua kuwa Tanzania iko katika kundi ambalo UN imelitaja kama nchi 50 masikini zaidi duniani, kundi moja na Afghanistan, Somalia, Timor mashariki, Comoro, DRC nk. Katika EAC, ni Kenya pekee haiko katika kundi hilo, lakini sisi wengine tumeingia kwa kuwaendekeza mafisadi kama Chenge!
Hebu angalia Tz ilivyo masikini wa kutupwa kwa vigezo mbalimbali vinavyotumika:
Kwa kutumia kigezo cha Purchasing Power Parity (PPP), orodha ya nchi 10 masikini zaidi duniani (kuanzia na iliyokithiri) ni:
Ten Poorest Countries (based on 2004 PPP GNP per capita in international$)
Sierra Leone ... $550
Malawi ... $630
Burundi ... $660
Tanzania ... $670
Democratic Republic of Congo ... $680
Guinea-Bissau ... $690
Republic of Congo ... $740
Ethiopia ... $750
Niger ... $780
Republic of Yemen ... $810
Source: World Bank, World Development Indicators 2004.
Hiyo inaonesha Tz ni ya 4 duniani katika umasikini uliokithiri. Ukitumia kigezo tofauti cha Human Development Index, Tz bado ni masikini mno, ni ya 151 kati ya nchi 173, na iko kwenye kundi lenye lowest levels of human development. Ukitumia kigezo cha GDP peke yake (bila kujali hiyo GDP inaweza kununua nini kwa matumizi Tz), Tz inakuwa nchi ya 11 katika masikini waliokithiri, ikitangukiwa tu na Nepal kwenye orodha hiyo, ambako ya kwanza ni Ethiopia!
Lakini je, hivi kweli sisi ni masikini kiasi hicho au ndio huu umasikini wa kujitakia (kwa kujinyamazia), hatuna zahanati vijijini lakini pesa zimekwibwa ziko Jersey, Uswisi nk "zinapumzika" tu na kuzungushwa kwenye mabiashara ya wazungu?
Alisema Nyerere: "Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotusababisha tunonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi" Mimi nadhani tunaihitaji hamasa hii sasa kwa ajili ya mapinduzi ya kweli.