'Bilionea' Chenge akimbia waandishi

'Bilionea' Chenge akimbia waandishi

Udaku kidogo - Kuna mtu ametizama vizuri hilo koti na shati ya chenge? Mnafikiri sh. ngapi???? That gives you a hint kwa nini bilioni za madafu anaita vijisenti!!!!!!

Tundu Lisu alisuggest kitu kimoja wiki hii hawa jamaa inabidi tuanze kuwazomea kila waendapo!!!!!!!
 
Huyo jamaa ana kiburi na dharau kubwa, mimi daima huwa siwashangai watu kama hao mimi namshangaa aliyewachagua. Labda slogan ya maisha bora kwa kila mtanzania hatukuielewa vizuri,inabidi tuwatafute hawa watanzania na tuwajue ni kina nani labda ndo kina chenge?
 
Huyu mzee kwa kweli sijui anawataka nini watanzania, Nadhani anatawataka watanzania lawama, siku watanzania wakianza vijimambo vyao tusisikie wakilalama, wavumilie.Naomba wajiandae
 
Huyu mzee kwa kweli sijui anawataka nini watanzania, Nadhani anatawataka watanzania lawama, siku watanzania wakianza vijimambo vyao tusisikie wakilalama, wavumilie.Naomba wajiandae

Amezioea kiburi huyo. Alipotajwa kwenye list of shame pamoja na kukiri kuwa yeye ni mkurugenzi TANGOLD aliwaambia pia waandishi "SIWEZI KUJIBU UTUMBO"; sasa aliosema utumbo umeanza kumwekea sisimizi tumboni sasa anakimbia tu!

Asha
 
JAMANI huyu chenge si ndie aliyehusika na kuigawa TTCL kwa management ya wazungu huyu???si ndio huyu aliyekuwa anaitetea hiyo kampuni ya sasktel kuwa ni bora wakati ni wachemshaji tu??

TTCL huduma zinazorota...,sasa nimejua kwa nini..,atakuwa alipewa cha kwake..,akahifadhi ofshore..,then ali-force wadhungu wake waje!!au mnasemaje hapa?!

Huyu jamaa hajafanya deal moja hii nchi jamani..,hao wachunguzaji waanzie mbali wasianze juzijuzi tu!!
 
Hakika hili la Chenge linashangaza na kuaibisha sana! Hivi wakuu mwajua kuwa Tanzania iko katika kundi ambalo UN imelitaja kama nchi 50 masikini zaidi duniani, kundi moja na Afghanistan, Somalia, Timor mashariki, Comoro, DRC nk. Katika EAC, ni Kenya pekee haiko katika kundi hilo, lakini sisi wengine tumeingia kwa kuwaendekeza mafisadi kama Chenge!

Hebu angalia Tz ilivyo masikini wa kutupwa kwa vigezo mbalimbali vinavyotumika:
Kwa kutumia kigezo cha Purchasing Power Parity (PPP), orodha ya nchi 10 masikini zaidi duniani (kuanzia na iliyokithiri) ni:

Ten Poorest Countries (based on 2004 PPP GNP per capita in international$)

Sierra Leone ... $550
Malawi ... $630
Burundi ... $660
Tanzania ... $670
Democratic Republic of Congo ... $680
Guinea-Bissau ... $690
Republic of Congo ... $740
Ethiopia ... $750
Niger ... $780
Republic of Yemen ... $810

Source: World Bank, World Development Indicators 2004.

Hiyo inaonesha Tz ni ya 4 duniani katika umasikini uliokithiri. Ukitumia kigezo tofauti cha Human Development Index, Tz bado ni masikini mno, ni ya 151 kati ya nchi 173, na iko kwenye kundi lenye lowest levels of human development. Ukitumia kigezo cha GDP peke yake (bila kujali hiyo GDP inaweza kununua nini kwa matumizi Tz), Tz inakuwa nchi ya 11 katika masikini waliokithiri, ikitangukiwa tu na Nepal kwenye orodha hiyo, ambako ya kwanza ni Ethiopia!

Lakini je, hivi kweli sisi ni masikini kiasi hicho au ndio huu umasikini wa kujitakia (kwa kujinyamazia), hatuna zahanati vijijini lakini pesa zimekwibwa ziko Jersey, Uswisi nk "zinapumzika" tu na kuzungushwa kwenye mabiashara ya wazungu?

Alisema Nyerere: "Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotusababisha tunonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi" Mimi nadhani tunaihitaji hamasa hii sasa kwa ajili ya mapinduzi ya kweli.
 
Hao waandishi nao waoga, si wangemkata mtama halafu wapige kelele za mwizi mwizi mwizi,

mama,
hii comment imenifanya nicheke mwenyewe hapa nilipo.Umenikumbusha vibaka wanochomwa moto kariakoo na kwingine. Niongezee...wangenyofoa taili la gari lake wakamvisha kisha watafute petrol na kibiriti vilipo,maake kwa mtindo wa kulindana huyu jamaa na mafisadi wengine hawatakaa wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
 
Nahisi TANZANIA kuna MABILIONEA wengi mno sema wanajulikana wachache
 
Back
Top Bottom