Bilionea Gautam Adani ambaye Kafulila anataka kumpa shirika la TANESCO ashitakiwa kwa utapeli huko Marekani

Namaanisha ela ambayo andani alikuwa anaenda kuiwekeza airport kenya ni kubwa kuliko ambaya DP kawekeza bandari yetu. Andani alikuwa ainvest $1.85 billion hizi ni zaidi ya tilioni 3 za kibongo huku DP wakiweza $250 milioni na wakisema kuwa wanaweza kuongeza hadi 1 bilioni.
 
Kwa Mujibu wa Taarifa za Habari za Ulimwengu, serikali ya Kenya imefuta rasmi mikataba Yote na kampuni hii, Hisa za kampuni hii zimeshuka Leo kwa zaidi ya asilimia 20 huko NY SEM, Hofu imeingia pia kwa wachangiaji wa kampuni juu ya hatma ya Kampuni hiyo siku za Usoni, huku ikiwa imewekeza Kenya Tanzania na Morocco, madalali wa Tanzania ikiwemo huyu aliyeenda India hivi karibuni nadhani hawatafanya mabadiliko yoyote! Kwa sababu amekua mpiga debe mkuu! Kenya haijajali kuwa ni miaka 30 ya uwekezaji kwenye Airports ambao ulilalamikiwa sana na wakenya!
Hapa kwetu tunampigia debe aingie kwenye umeme! Kama alihonga huko duniani logically hapa amehonga pia mana Rushwa imekua order of the day!
 
Bandari wameisha mpa ndio hizo PPP tunazo zikosoa na kuonyesha kushindwa kwa Sirikali kufanya wanachotakiwa kufanya, kukusanya Kodi na kuzitumia vizuri.
 
Niliwahi kusema, huyu KAFULILA atakuwa bilionea na hii PPP.
Hapa mali zetu ni zinadalaliwa
Yani yupo a few yard kuwa multibillionaire. Akifanikisha hio dili moja tu lazma alambe mzigo level za Billion 100 au zaidi.
 
Nimewaambia huyu Bwana mdogo Kafulila hajui ngoma anayoicheza amejiunga CCM amekuwa mjinga tofauti na huko nyuma alipokuwa na Akili.kuna mtu aliwahi kumwita Kafulila tumbili inawezekana akawa tumbili kweli.
 
UREFU WA KAMBA UNAZINGATIWA MKUU.
 
Tumbili kama Tumbili ukiona amekomalia kitu ujue ana mgao wake tayari.
 
Niliwahi kusema, huyu KAFULILA atakuwa bilionea na hii PPP.
Hapa mali zetu ni zinadalaliwa
Lucas Mwashambwa aione kwenye file! Wakiambiwa wanavimbisha magego tu! Wababe wa Dunia wamefanya upelelezi na kugundua kwamba jamaa anahonga Ili kupata fursa! Na Kenya wanejiridhisha wamemtimua bila kujali miaka 30 ya mkataba! Sisi hapa kwetu tunatunga Sheria zinazojenga mazingira tukiwafukuza watushtaki tuwalipe! Haya Yuko bandarini na DP world na ni tapeli, kwa mujibu wa habari za kuaminika, watu wameanza kuchomoa fedha zao kwenye Hisa Leo. Pale NY ameporomoka thamani kwa 20% Leo tu je kesho, je akiamza kupanda mahakamani?
 
Machawa ni maadui wengine wa taifa hili.
 
Kama kuna rushwa ya huyu Gabacholi basi Tumbili anamfanyia kazi mtu (si bure)
 
Machawa ni maadui wengine wa taifa hili.
Pale wanapopewa nafasi ya Kuongea wao tu, hutumia nafasi hizo kuaminisha na kuhubiri Yale yasiyofaa kwa kuyafanya yanafaa Ili kukidhi mahitaji Yao!

Hujieguza mahakama kwa kuhoji, "uko wapi ushahidi" wakipewa taarifa sahihi hukimbilia Nenda mahakamani, huku walikua wameweka bunge na mahakama mifukoni mwao. Sauti zikizidi huchagua njia ya haramu ya kuteka na kuua. Lust for money and power.
Awali nilijua tu Kafulila ni dalali Ndio mana anatumia nguvu nyingi kuhubiri PPP, Kwa maslahi binafsi kuwanufaisha mabepari wachachen na watu walioko katika circle yake.

Jiulize kama Stiegelrs Gorger inazalisha umeme wa kutosheleza na upo wa ziada., zile ahadi umeme utashuka bei Ili kuongeza unafuu wa maisha uko wapi? Kama mradi ulijengwa kwa fedha zetu kwanini sisi tusiwe wa kwanza kufaidika? Kilichotokea ni kupanda kwa gharama za umeme kimya kimya!

Na kama haitoshi, sasa hivi wanataka kutuzoesha utaratibu wa kukatika umeme Ili kuhalalisha kuwapa matapeli tenda ya kusimamia usambazaji ikiwemo kujenga miundombinu na gharama kuongezeka kwenye upatikanaji wa huduma ya umeme ikiwemo gharama za kuunganishwa!

Ukiangalia MWENYEKITI wao anahangaika na kampeni za nishati safi Kwa ajili ya kulinda afya na mazingira. Cha kushangaza utadhani hajui kwamba gharama za gesi ya kutumia majumbani Bado ni kubwa. Gharama za kuunganisha umeme pamoja na units ni kubwa. Badala kumshauri aangalia swala la kisera ikiwemo tax exemption kwenye gas na vifaa vyake pamoja na gharama za umeme, wao humsifia tu kisa ameongea majukwaani nyumbani na kwa wajomba! Hawa watu ni goons
 
Nchi hii ukiwaza na kutathmin mambo mengi karoho kanauma.
Ni dhahiri viongozi madaraka yamewalevya, wanatuona sisi kama punguani fulani hivi walikuwa wanakata buku buku kwenye umeme kila mwezi, sasa hivi wameipandisha kimya kimya ni buku jero.

Kuna mambo ya kiwaki mengi kupitiliza.
 
Kenya alishavurumishwa ila Shamba la Bibi atasitawi. Sijui ni nani ametuloga Yarabi.
 
Kwanza fahamu mijadala hufanywa na wenye akili, ukishaona watu mijadala mikubwa ni mwenge, kumbukizi za Vifo, may mosi, siku ya ukimwi, siku ya wanawake hapo ujue Pana tatizo kubwa sana
Hii comment yko inatakiwa iwekewe bango...
 
Hili tukio la kushitakiwa bilionea Adani liwe onyo kwa kafulila na PPP yake. Muhimu tuwaze nchi kuweza kuendesha yenyewe yale mashirika tuliamua lazima yawe chini ya umiliki wa umma. Tumekua tunaonya hukuna wajomba duniani. Tumeona hatua rais Ruto amechukua kuwatosa Adani group. Rushwa kwa vigogo ni hatari maana tunajipeleka wenyewe kupigwa kiuchumi huku kukiwa na matokeo hasi kiuchumi kwa umma wa wananchi wetu.
Kwanza tutambue sisi ni nchi huru. Tunapoteza uhuru wetu kwa kujiaminisha kwa wageni kuhusu mustakabali wetu kiuchumi. Lazima tuwe na aina ya uongozi wa taifa wenye ujasiri maarifa na maono sahihi kwa kesho ya taifa letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…