Bilionea Lugumi kuhudhuria ‘Kikao cha Wanaume’ April 2, 2026

Bilionea Lugumi kuhudhuria ‘Kikao cha Wanaume’ April 2, 2026

Kiingilio 50,000/-
Hio hela Bora nikanywe bia na kuchoma Kilo 2 za nyama manyoko
Watakaoenda watageuzwa fursa,inabidi wajue wao ndiyo watazidi kumtajirisha!

Eti bilionea awaite walala hoi akajadili nao changamoto zao na wamsikilize akiwaambia alifanya fanyaje hata akafanikiwa.
 
Niliona tangazo lao!

Ni fursa ya networking na socialization kwa vijana

Ila wawe waangalifu, wasije kugeuzwa wao ndiyo fursa
 
Nend huwa ni vizuri sana wanzungumzia sana masuala ya uchumi na maisha ningekuwa na kaclip cha mfano ningekuwekea
bora hata wangeitisha kikao kikiwahusu vijana wa dar es salamu. Kuliko kuwaalika mataita wote kikaoni. Kiingilio 50k si mchezo mzee
 
Kikao maalum kwa ajili ya wanaume kitafanyika April 2, Mlimani City na kimeandaliwa na @prophetipm kikilenga kuwakutanisha wanaume watu wazima pamoja na vijana ili kujadili masuala muhimu yanayohusu maisha, maadili na juhudi za kujiletea maendeleo binafsi.

Miongoni mwa wazungumzaji ni mfanyabiashara bilionea @lugumisaidi ambaye anatajwa kuwa mfano wa mafanikio kwa vijana wengi nchini Tanzania na barani Afrika. Uwepo wake unatarajiwa kuleta hamasa kubwa kutokana na safari yake ya maisha na mafanikio aliyoyapata kupitia juhudi, nidhamu na uthubutu katika shughuli za kibiashara na kijamii.

Akieleza sababu za kumualika @lugumisaidi kuwa mzungumzaji, @prophetipm amesema “Sababu ya kumualika Lugumi ni upendo wangu kwake, ana upendo , hajivuni lakini pia ana ushawishi Tanzania kwa namna anavyoishi , anasaidia watu , anahudumia yatima, nikaona vijana wengi wa Tanzania wanatamani kufanikiwa sasa yeye anayo mengi ya kuwa-inspire vijana, wanaume wa Afrika kujifunza namna ya kupambana, naamini maneno atakayozungumza machache yataenda kubadilisha maisha ya watu, watakuwa na morali mpya kwenda kufanya kazi kujifuma kupambana katika maisha”

Aidha, waandaaji wa kikao hicho wanaamini kuwa ujumbe utakaotolewa na wazungumzaji, hususan Lugumi, utaweza kuwajengea washiriki morali mpya ya kufanya kazi kwa bidii, kujitegemea na kupambana ili kufikia ndoto zao. Wanatarajia kuwa mafunzo na ushauri vitakavyotolewa vitachangia kubadili mitazamo ya wanaume na vijana wengi na kuwahamasisha kuwa watu wenye maadili mema na mchango chanya katika maendeleo ya jamii. 💼✨📣
Vipi Anko T atashiriki????
 
Back
Top Bottom