TANZIA Bilionea Mustafa Sabodo afariki dunia

Yani aliwapa hela cdm ya kuchimba visima? Leta hiyo taarifa ilipo.

Au sikiliza hapa useme ni wapi sabodo alitamka hivyo

View: https://youtu.be/ggLBDDb2MJc?si=31g4vmV_sg8nichS

View: https://twitter.com/kigogo2014/status/1461967536124317698

Rudisheni hela za mzee wa watu.
 
Unaniwekea story mlizotunga wenyewe? Nimekuwekea video ta itv sabodo mwenyewe akiongea na mbowe akishukuru wewe unaniletea vyanzo vya watu kama wewe.
 
Nimepokea taarifa, mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo amefariki Dunia. Sabodo ametokea mkoani Lindi na alijenga shule maarufu kule pia alifadhili chama cha upinzani cha Chadema

======

Mustafa Sabodo alizaliwa mwaka 1942 mkoani Lindi na alipata kusema ametoka kwenye familia yenye utajiri wa imani na fedha.

"Mimi nimetoka kwenye familia ya Uislamu wa Kihindi wa Gujarati Khoja, nilijitahidi kupambana dhidi ya umaskini nikiwa na matarajio ya kuwa tajiri na ninamshukuru Mungu nimekuwa hapa nilipo,"alisema.

Licha ya kupooza sehemu ya mwili wake mwaka 2000, Sabodo aliendelea kufanya kile anachotaka ikiwemo kusimamia miradi yake na ya jamii kuhakikisha inafanikiwa ikiwemo kuchimbia visima zaidi ya 280 nchini.

Licha ya kutoka kwenye familia ya utajiri baadaye alifilisika na akapambana dhidi ya kufilisika huko kwa kuweka matarajio ya kuwa tajiri na baadae akawa.

ELIMU
Kielimu, Sabodo alisoma Shule ya Sekondari ya Lindi na baadaye alihitimu ngazi ya cheti kwenye Chuo cha Cambridge.

Baadaye alihitimu Chuo cha Edinburg nchini Uingereza mwaka 1965 ambapo alisoma sheria ya biashara na usimamizi wa mifuko ya fedha.

Baadaye aliishi nje ya Tanzania kwa kufanya kazi ya ushauri wa kimataifa na kurejea nchini mwaka 1996 na kuwekeza.

MOYO WA KUJITOLEA
Mwaka 2003 Sabodo alitoa udhamini wa uchezeshaji wa bahati nasibu ya mfuko wa Mwalimu J.K Nyerere wenye thamani ya Sh 100 milioni.

Wazo la kuanzishwa kwa mfuko huo wa Mwalimu Nyerere lilikuwa la Sabodo, pia alichangia Sh 1.3 bilioni katika kuufanikisha.

Pia Sabodo amechangia miradi mbalimbali ikiwemo kutoa kiasi cha Sh 5 bilioni kwa ajili ya kuchangia chuo cha ualimu cha elimu ya juu cha Mtwara, alichangia Sh 965 milioni kwa ajili ya upanuzi wa majengo ya hospitali ya Shree Hindu Mandal, mradi wa Khoja Shia-aheri Sh 1.6 bilioni.

Sabodo licha ya kuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), alitoa Sh 100 milioni kwa ajili ya kukipongeza chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa ajili ya ushindi wa kiti cha Ubungo alichoshinda Joshua Nasari wa jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha wakati huo.

Pia alitoa baskeli 100 na kuahidi kuchimba visima vitano katika jimbo hilo.

======

KSI Jamaat of Dar es Salaam, Tanzania

Death Announcement

‎إِنَّا للهِ وَإِنَّـا إِلَيْهِ رَاجِعون
”Surely we belong to Allah and to Him shall we return”.

It is with sadness that we share the news of demise of MUSTAFA RAJABALI JAFFER (SABODO) has passed away in Dar Es Salaam.

More Details To Follow...

Kafan - Dafan Committee
Mzee moyo wa CSR rest in peace tabasamu huku ukiwa kwenye safari ya milele 🙏🙏🙏
 
Rip sabodo tutakukumbuka daima
 
Bilionea Mustafa Sabodo amefariki lkn maumivu yamebakia kwa wengine.

Alikuwa ni bilionea mwenye huruma Kwa jamii ya watanzania.

Alijenga mashule na alikuwa pia ni muumini wa siasa zenye usawa na mpenda haki.
Nakumbuka alitoa pesa ijengwe ofisi mkaenda kupanga lile banda kuku pale ufipa!
 
Back
Top Bottom