Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Clip yake nimeiona twitter(Darmpya Blog on twitter), imenifurahisha mno na huyu inaonyesha ni muongeaji mzuri sana.Akiingia Bungeni, itakuwa ni shida(watu wataomba muongozo wa kiti mwanzo, mwisho).
Anakwambia: Akili kichwani, pesa mfukoni, Yesu moyoni.
Msikilizeni hapa kwenye hii clip akihojiwa:
Waliojipa kazi ya kuia CHADEMA wamefeli kwa asilimia 100, kwani watia nia ni wengi nchi nzima akiwemo huyu aliewatosa watu wa chama cha kijani akaona aje ajaribu kugombea kupitia CHADEMA,huku akidai yeye hana njaa.
Siku zinaenda kasi sana...sasa hivi huyu bilionea kawachefua makamandaSalary Slip,
Sasa huyu ndio sio tapeli ila Gwajima siku hizi tapeli, makamanda bana [emoji1787][emoji1787]
ha ha ...duh..mmefikia wapi na bilionea?Katika kuaanda michakato ya kuwatafuta na hatimaye kufanikiwa kuwapika makada vijana na kuwa viongozi mahiri hapa nchini, basi CDM inastahili kongole zake. Kitu kama hicho ambacho alikifanya Mwl. Nyerere katika kipindi cha ile CCM iliyokuwa na agenda za kisiasa zenye kubebwa na hoja makini.
Si hii CCM ama UVCCM ya sasa, wote ni wale wale, kumejaa wababaishaji toka viongozi Taifa mpaka mashinani. Wote hutegemea tu mbeleko ya dola ktk kukabiliana na washindani wengine wa kisiasa pasipo kulimudu vyema jukwaa la kisiasa kama njia ya kujenga hoja shindani.
Hata hapa ndani ya jukwaa hili, utakuta mtu anaanzisha uzi wenye maudhui mazuri kwa ajili ya mijadala pevu, lkn wana Lumumba aka Buku 7 wao huja na kauli nyepesi nyepezi na tena zenye maudhui kama njia yao pekee ya kutaka kuleta uharibifu ktk hoja iliyotolewa, kwa malengo ya kumtoa mtoa hoja kwenye reli.
Hii ndiyo njia pekee iliyobaki kwa wao kukwepa kujibu hoja kinzani. Tunapoelekea kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, hoja mezani itakuwa ni kwa namna gani CCM ilitekeleza ilani Yao iliyopita ya uchaguzi. Ilikuwa ni kwa maendeleo ya vitu ama ya watu, hapo hakuna ujanja ktk hili, si TAKUKURU ama Jeshi la Polisi litawasaidia ktk hili.
Niliyaona haya mapema sana.Huyu shila sio wa kumwamini sana,niwashauri chadema kuwa makini,ccm inaweka mapandikizi ili baadae yajitoe uchaguzi kuvuruga chama,huyu shila ni rafiki mkubwa sana wa bashite.
Kwani na huyu nae kasema Pengo kala maharage gani sijui, au na yeye kasema misikiti ote ataigeuza sunday shool au nae kala kondoo?Huyu hajachanganya dini na siasa wandugu? Mbona naona comment nyingi tofauti na alivyotangaza nia Gwajima? Tuache unafki kwenye nyeusi tuseme nyeusi haijalishi ni upande gan!
Angalau wewe unajielewa kuliko haya kina salary slipBahati mbaya huwezi kukumbatia pesa halafu ukabaki na Yesu, hawa watu wanaonesha jinsi walivyo watafutaji, nawasikitikia sana hao waumini wao, naona msimu wa fursa kwao umewadia.