Bilionea wa Kirusi akutwa akiwa amefariki dunia ndani ya hoteli Zanzibar

Bilionea wa Kirusi akutwa akiwa amefariki dunia ndani ya hoteli Zanzibar

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Mambo ndiyo kama hivi wadau!

==========

Bilionea wa Kirusi, Igor Sosin amefariki kwenye mapumziko mjini Zanzibar akiwa na mwanae wa kike, Taisia pamoja na mwanamke ambae hajafahamika. Hii ni miaka mitano tangu mtoto wake wa kiume, Egor alipomnyonga mke wake wa pili na waya wa simu mwaka 2015.

Mwanae Egor hakupata kesi kwa kumuua mama yake baada ya kugundulika na ugonjwa ambao haukusemwa wa akili. Alikubali kumuua kwenye hoteli ya Kazan akidai alitaka kulitoa shetani ndani ya mama yake. Baadae aliachiliwa kwenye hospitali ya akili baada ya kufanikiwa kutibiwa ugonjwa huo.

Inasemwa kuwa amemtaliki mke wake wa tatu na chanzo cha kifo bado hakijajulikana. Miezi kadhaa iliyopita, bilionea huyo wa Kirusi alipona Covid19. Polisi mjini Zanzibar wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho kwenye hoteli ya Park Hyatt na mwili wake ulipelekwa hospitali ya Mnazi mmoja kujua chanzo cha kifo chake.

RPC wa Mjini Magharib, Awadhi Juma Haji amesema ofisi yake bado haijapokea taarifa kutoka hospitali hivyo hawezi kusema nini hasa kilimuua bilionea huyo. Mwili wake utasafirishwa kwenda nchini kwake kwani taratibu zote zimekamilika.


Sonin.jpg
 
Watakaomsogelea wahakikishe wamevaa barakoa, Covid haiogopi maombi.
Duh,kwa hiyo unataka kusema hata binti wa kizanzibar tayari ana covid 19? Maana alikuwa analala na marehemu bilionea. Au unaleta hisia za kiChadema?
 
Tujifukize tena? Maombi yanafanya nini sasa?
 
Poleni sana!

Hapa makamanda wa Ufipa watajifanya wajuaji kupita maelezo!

Hapa mifuasi ya chama fulani itakuwa inafanya jitihada zote kufunika funika ili ugonjwa fulani usiwe ni chanzo cha kifo hata kama ndiwo.

Alaumiwe sana dobi Ila, kaniki ni rangi yake!

Apumzike kwa amani mtalii huyu. Yeye ni shahidi mwaminifu.
 
Back
Top Bottom