Bilionea wa Kirusi akutwa akiwa amefariki dunia ndani ya hoteli Zanzibar

Bilionea wa Kirusi akutwa akiwa amefariki dunia ndani ya hoteli Zanzibar

Hapa mifuasi ya chama fulani itakuwa inafanya jitihada zote kufunika funika ili ugonjwa fulani usiwe ni chanzo cha kifo hata kama ndiwo.

Alaumiwe sana dobi Ila, kaniki ni rangi yake!

Apumzike kwa amani mtalii huyu. Yeye ni shahidi mwaminifu.
Hata kama ni corona kakuambia nani kaipata ZNZ. Inawezekana katoka nayo kwao. Kafia kwenye kinena cha mtoto wa kizenj, jaza mwenyewe.
 
Wengi wamesema itakuwa ni kutokana na matumizi ya vidonge vya kuongeza nguvu aina ya Viagra lakini taarifa kamili hii hapa.

UNGUJA.
Bilionea wa Russia, Igor Sosin amekutwa amefariki katika chumba cha hoteli ya Park Hyatt iliyopo mtaa wa Mji Mkongwe mjini Unguja.

View attachment 1659420

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji alithibitisha kutokea kwa kifo cha bilionea huyo kuwa kilitokea usiku wa Desemba 23.

Kwa mujibu wa kamanda huyo siku ya kifo chake, Sosin alikuwa na mwanamke wa kizanzibari aitwaye Arafa Ramadhan Mpondo (23), mkazi wa Fuoni ambaye anadaiwa kuwa ni mpenzi wake aliyempata kwa njia ya mtandao.

Alisema baada ya kuhojiwa Arafa alieleza kuwa saa 5:45 usiku alimuona marehemu hayuko vizuri lakini akaamua kulala naye hadi asubuhi.

Kulipokucha alimuamsha lakini hakuamka, ndipo alipotoa taarifa kwa uongozi wa hoteli kwa ajili ya hatua zaidi.

Kamanda alieleza kuwa mwili wa marehemu alipelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja na majira ya saa 5:51 usiku kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Akizungumza kuhusu mwanamke huyo, Kamanda Awadh alisema bado anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano huku wakisubiri majibu ya uchunguzi wa kidaktari ingawa hadi sasa imebainika kuwa bilionea huyo alikufa kifo cha kawaida.

Msemaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Hassan Mcha Makame, alisema mwili wa marehemu umetolewa damu kwa uchunguzi wa kimaabara na tayari mwili huo umekabidhiwa kwa familia yake na wameshafirisha kwenda nchini kwao.

KUTOKA UINGEREZA.
Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeripoti kuhusu kifo cha bilionea huyo likieleza kuwa mapema mwaka huu aliugua na kupona ugonjwa wa corona na alipanga kusherehekea mwaka mpya akiwa visiwani Zanzibar.

Bilionea huyo anayeaminika kuwa na utajiri unaokadiriwa kuwa Dola18 bilioni (Sh41.5 trilioni), alitambulika kuwa mapenzi ya kuzunguka na boti baharini na kucheza mpira wa tenisi.

Wakati wa uhai wake bilionea huyu aliweka wazi kuwa anapenda kuishi maisha ya kifahari na starehe ilikuwa na nafasi kubwa kwenye maisha yake.
Sosin anatambulika kama mwanzilishi wa kampuni za Starik Hottabych na Modi baada ya kuanguka kwa mfumo wa kijamaa nchini humo.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Sosin amekutwa na umauti akiwa kwenye mchakato wa kutalikiana na mkewe wa tatu aitwaye Inna.
Kifo cha Sosin ni mwendelezo wa habari za kuhuzunisha zinazohusisha family hiyo kwani hivi karibuni mtoto wake wa kiume, Egor, akiwa na umri wa miaka 19, inasemekana alimuua mama yake kwa waya kumkaba na waya wa simu.




SOURCE: Mwananchi
wanawake sio poa aisee
mtu analala na mtu mwenye utajiri wa b 18 akipewa posho apo
anafungua kamradi kake anaanza na yeye kuwa motivation speaker😛😛😛😛
 
Corona.

Zanzibar sasa hivi wamejaa warusi waliokimbia kwao kwa sababu ya corona kwa kigezo cha kuja kutalii.
Acha uongo.
Hawajakimbia kwao.

Wamekuja kwa sababu destinations zao nyingi zimefungwa au zina restriction nyingi. Kama uturuki Na Egypt
 
Vumbi la Congo ndio limemuua. Huyo binti alibanwa na plaizi atasema alimfanya nn huyo mzee kabla ya kulala naye

mkuu, kwanini wambane dada wa watu ? alikuwa kwenye utafutaji kama watu wengine tu, ukute labda hata wamekutana Badoo huko
sioni kama anapaswa huko dada kubanwa wakati jamaa mwenyewe ndiye kafata utamu, hiyo james Bond anaiita occupational hazard
 
Back
Top Bottom