Bilionea wa Kirusi akutwa akiwa amefariki dunia ndani ya hoteli Zanzibar

Bilionea wa Kirusi akutwa akiwa amefariki dunia ndani ya hoteli Zanzibar

Umepata wapi mamlaka ya kutangaza habari ya vivo vya watalii wanaokuja kutalii ndani ya nchi yetu, wewe utakua umetumwa na mabeberu
Haka kajamaa si kalikuwa kamati ya kuleta habari za vifo vya Covid19, au umeshakasahau? 😂😂
 
Wengi wamesema itakuwa ni kutokana na matumizi ya vidonge vya kuongeza nguvu aina ya Viagra lakini taarifa kamili hii hapa.

UNGUJA.
Bilionea wa Russia, Igor Sosin amekutwa amefariki katika chumba cha hoteli ya Park Hyatt iliyopo mtaa wa Mji Mkongwe mjini Unguja.

zanzibarpic-data.jpg


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji alithibitisha kutokea kwa kifo cha bilionea huyo kuwa kilitokea usiku wa Desemba 23.

Kwa mujibu wa kamanda huyo siku ya kifo chake, Sosin alikuwa na mwanamke wa kizanzibari aitwaye Arafa Ramadhan Mpondo (23), mkazi wa Fuoni ambaye anadaiwa kuwa ni mpenzi wake aliyempata kwa njia ya mtandao.

Alisema baada ya kuhojiwa Arafa alieleza kuwa saa 5:45 usiku alimuona marehemu hayuko vizuri lakini akaamua kulala naye hadi asubuhi.

Kulipokucha alimuamsha lakini hakuamka, ndipo alipotoa taarifa kwa uongozi wa hoteli kwa ajili ya hatua zaidi.

Kamanda alieleza kuwa mwili wa marehemu alipelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja na majira ya saa 5:51 usiku kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Akizungumza kuhusu mwanamke huyo, Kamanda Awadh alisema bado anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano huku wakisubiri majibu ya uchunguzi wa kidaktari ingawa hadi sasa imebainika kuwa bilionea huyo alikufa kifo cha kawaida.

Msemaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Hassan Mcha Makame, alisema mwili wa marehemu umetolewa damu kwa uchunguzi wa kimaabara na tayari mwili huo umekabidhiwa kwa familia yake na wameshafirisha kwenda nchini kwao.

KUTOKA UINGEREZA.
Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeripoti kuhusu kifo cha bilionea huyo likieleza kuwa mapema mwaka huu aliugua na kupona ugonjwa wa corona na alipanga kusherehekea mwaka mpya akiwa visiwani Zanzibar.

Bilionea huyo anayeaminika kuwa na utajiri unaokadiriwa kuwa Dola18 bilioni (Sh41.5 trilioni), alitambulika kuwa mapenzi ya kuzunguka na boti baharini na kucheza mpira wa tenisi.

Wakati wa uhai wake bilionea huyu aliweka wazi kuwa anapenda kuishi maisha ya kifahari na starehe ilikuwa na nafasi kubwa kwenye maisha yake.
Sosin anatambulika kama mwanzilishi wa kampuni za Starik Hottabych na Modi baada ya kuanguka kwa mfumo wa kijamaa nchini humo.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, Sosin amekutwa na umauti akiwa kwenye mchakato wa kutalikiana na mkewe wa tatu aitwaye Inna.
Kifo cha Sosin ni mwendelezo wa habari za kuhuzunisha zinazohusisha family hiyo kwani hivi karibuni mtoto wake wa kiume, Egor, akiwa na umri wa miaka 19, inasemekana alimuua mama yake kwa waya kumkaba na waya wa simu.




SOURCE: Mwananchi
 
Aisee gone too soon

Hako kabinti kazi ipo mpaka uchunguzi uishe atakuwa ameshakaa selo takribani mwezi 1 na siku kadhaa
 
Akili yangu imewaza hivi....

Ni wakati muafaka sasa wa Zanzibar kujenga hispitali moja nzuri ambayo itakuwa kivutio kwa watalii na kuwahakikishia watapata huduma kama wako ughaibuni wakiwa vakesheni huko Zanzibar na wakipatwa na ugonjwa ghafla maana helabya matibabu pia itabaki Zanzibar.

Sijui nimeeleweka...!! Maana nimejaribu kufupisha sababu huwa nna maelezo marefuuuu.
Yaani hiyo hospitali iwe ni uwekezaji na ni sehemu ya utalii ambayo itahudumia watalii hata wazawa wakiweza kumudu gharama mradi huduma ziwe za hali ya juu na vifaa viwe bora na imara.

Happy Boxing Day.
 
Aisee gone too soon

Hako kabinti kazi ipo mpaka uchunguzi uishe atakuwa ameshakaa selo takribani mwezi 1 na siku kadhaa
Hujaona Kamanda ameshaweka dondoo kuwa Inaonekana Jamaa amekufa kifo cha Kawaida?

Arafa atakaa ndani Kwa muda labda Kwa ajili tu ya usalama wake.
 
Zenj daily ndege za kutoka Urusi zinamwaga wazungu, wanakimbia Covid kwao, wanaileta bongo..Wabongo Covid ipo tujihadhari.
 
Back
Top Bottom