Bilionea wa Ubelgiji atuma bilioni 1 kwa mpenzi wake, Mahakama yataifisha

Bilionea wa Ubelgiji atuma bilioni 1 kwa mpenzi wake, Mahakama yataifisha

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1685053533627.png

Mahakama kuu Nchini Kenya imeiruhusu Serikali ya Nchi hiyo kutaifisha zawadi ya pesa za Kenya milioni 102 milioni (TSH. Bilioni 1.74) iliyotumwa kutoka Ubelgiji na Bilionea aitwae Marc De Mesel kwenda Kenya kwa Mpenzi wake ambaye ni Felista Nyamathira Njoroge (23) baada ya kubainika kuwa huenda kiasi hicho cha pesa kilitokana na utakatishaji fedha.

Jaji Esther Maina aliamuru kutaifishwa kwa fedha hizo kwasababu chanzo chake kutoka kwa Bilionea Marc hakikuwekwa wazi kama ilivyotakiwa na kusema kutokana na kukosekana kwa taarifa za chanzo cha fedha hizo huenda zimetokana na utakatishaji fedha hivyo akaunti za Benki zichukuliwe kwa Serikali.

Nyamathira ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi Nairobi aligonga vichwa vya habari mwaka 2021 alipofichua kuwa Polisi wameishikilia zawadi ya pesa aliyotumwa na Mpenzi wake aliyepo Ubelgiji.

Vyombo vya Habari Kenya vimeripoti kwamba hii sio mara ya kwanza kwa Tajiri huyo wa Ubelgiji kutuma pesa nyingi Kenya kwani aliwatumia Wanawake wengine watatu jumla ya pesa za kenya milioni 257 ambazo ni zaidi ya Bilioni nne kwa pesa za Tanzania ambapo Mwanamke mmoja Jane Wangui Kago alitumiwa milioni 49 za Kenya, Serah Wambui shilingi milioni 100 na Tabby Wambuku Kago milioni 108.
 
Sasa kwanini mahakama imetumia neno " huenda"

Hii ina maanisha kuwa imeacha kuthibitisha pasipo shaka. Je judge angetumiwa yeye hizo hela angependa zichukuliwe tuu.

Chukulia dada wa watu anajituma kwa mpenzi wake kwenye tendo halafu juhudi zake zinazimwa na mahakama kwa neno la huenda.

Wampe maua yake
 
Ni aibu kubwa sana kwa taifa la Kenya na huo ni uporaji mchana kweupe

Huyo jamaa ni investor na kwenye tweeter yake ameandika pamoja na girlfriends sio girlfriend
Na anatoa msaada kwa masikini na marafiki
Inakuwaje waibe hela zake
Kweli kabisa ndugu yangu; kazi ya serikali ilikuwa ni kukata income tax kwenye pesa hizo ambazo zingeaminika kuwa ni income kwe huyu binti na kumwachia kilicho chake. Lakini wao wanachukua kila kitu ambayo siyo utaratibu wa serikali.
 
Kweli kabisa ndugu yangu; kazi ya serikali ilikuwa ni kukata income tax kwenye pesa hizo ambazo zingeamika kuwa nia income kwe huyu binti na kumwachia kilicho chake. Lakini wao wanachukua kila kitu ambayo siyo utaratibu wa serikali.
Majizi tu hayo
Haya wamechukua watagawana wao
Ila laiti wangepewa wote waliotumiwa nina uhakika wangefanya miradi mingi na kuajiri masikini kibao wenye uhitaji na kuwasaidia wengine

Africans tuna shida sana
 
Back
Top Bottom