Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
BILIONI 1.3 KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KIJIJI CHA KUMUBUGA, NGARA
Serikali imetenga Shilingi Bilioni Moja na Milioni Miatatu (Bilioni 1.3) ili kutatua changamoto ya tatizo la Maji katika Kijiji cha Kumubuga Kata ya Nyamagoma wilayani Ngara mkoani Kagera
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nyamagoma alipofanya ziara ya kikazi ya kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi wa Jimbo lake
Akiwasilisha changamoto mbalimbali za Kata hiyo kwa Mbunge wa Jimbo la Ngara, Diwani wa Kata ya Nyamagoma Mhe. Laurent John Msongalele Amesema kuwa Mbunge Mhe. Ndaisaba George Ruhoro amefanya kazi kubwa ya kuwaletea Maendeleo wananchi
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilayani Ngara mkoani Kagera Bi.Anastazia Amos amesema wananchi wajiandae Kujiandikisha katika Daftari la Makazi ili kupata sifa ya kuwachagua viongozi wao wa Serikali za mitaa.