Tetesi: Bilioni 1.9 zaibwa CHADEMA, Wingu zito latanda. Wabunge wagoma kuchangia chama

Tetesi: Bilioni 1.9 zaibwa CHADEMA, Wingu zito latanda. Wabunge wagoma kuchangia chama

Status
Not open for further replies.

ALWATAN KIZIGO

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
539
Reaction score
644
Kuwa mpinzani ni sawa na kuvaa nguo nyeupe , DOA likigusa tuuuu ni balaaa .Ni kweli wakuu fedha zimepigwa, zaidi ya 1.9 Bilioni.

Wakuu ni hivi jumla ya Tsh 1.9 Bilioni, Zimekwapuliwa kwenye account ya Chama, (CHADEMA) Miezi kadhaa iliyopita.

Toka jana Chama kimeshindwa kujenga hoja kabisa juu ya ukwapuliwaji wa hizo fedha, John Mrema amejenga hoja dhaifu kuwahi kutokea, kwa kusema kuwa chama kinachafuliwa kwa kuwa tunaelekea uchaguzi mkuu. Hii ni hoja dhaifu kweli kweli

Ipo hivi, Kwa kawaida wabunge wa viti maalumu CHADEMA huchangia 1, 560, 000 kwa mwezi,

Na wabunge wa majimbo huchangia 520, 000 kila mwezi

Katibu mkuu Dr. Vincent Mashinji, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Mweka hazina ndio waweka sahihi kwenye hiyo account. (signatories)

Ni takribani ya miezi 5 sasa wabunge hawaendelei kuchanga fedha hizo (wamegoma) baada ya kubaini kuwa fedha hizo zimekwapuliwa na kupelekwa kusiko julikana

Kama mimi muongo aje mbunge yeyote aseme yeye kama ndani ya hii miezi 5 amechanga zile fedha za wabunge zilizokuwa zinachangwa kila mwezi. Na kama haziendelei kuchangwa kuna nini nyuma ya pazia?

Jiulizeni kwa nini wabunge sasa hawachangi fedha hizo?.... Why hawachangi?... Kuna nini nyuma ya pazia?... Aje mbunge hata mmoja aliyechangia mwezi huu au mwezi uliopita.

Jana Mayor wa ubungo kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter badala ya kujenga hoja, anapiga picha magari ya chama, na kudai hakuna fedha zilizo kwapuliwa, anataka kusema kuwa fedha za michango ya wabunge ile imetumika kununua magari?

Fedha za Ruzuku zilifanya nini? .... Leteni ushahidi kwa nini hawaendelee kuchanga fedha kama ilivyo kuwa awali?

Jana Joseph Selasini akijibu hoja hiyo ameweza kukubali kuwa ni kweli Wabunge hawaendelei kuchanga kwa takribani ya mezi 5 kwa kile alicho kieleza kuwa spika amegoma kuwakata.

Mjiulize kwa nini Ndugai amegoma kuwakata?... Kama ameshindwa kuwakata na nyie mpo safi na hakuna upotevu wa hizo fedha za wabunge kutoka account ya ECO Bank, mmeshindwa kuitisha kikao kutafuta njia mbadala ya wabunge kuendelea kuchanga?...Why mnakwepa vikao?

Nimalize kwa kusema, Hao wanaotetea kwamba Fedha zimetumika kununua magari au pikipiki. Je wanajua wanachokifanya? Hawaoni kama wanazidi kukichafua chama?

Haya wabunge njooni sasa, uwanja ni wenu, semeni ni lini mmechanga hizo fedha?

Yani CHADEMA ya sasa haina maana kabisa muda wa kufanyika kwa uchaguzi kwa mujibu wa kalenda ya Chama umeshapita na Mbowe hataki kabisa kuitisha uchaguzi labda kwa sababu anahofia madudu yake kubainika.
 
kama ni kweli , hiyo bil 1.9 iliyopotea CHADEMA wangekuwa wana dola ingepotea tril 1.9
Ten percent au sio?
CCM WEZI NA CHADEMA PIA WEZI? NCHI YA WEZI NA WABINAFSI?

Tuachane na wanasiasa kama kweli wote wakwapuaji kisha apatikane mwanamapinduzi asie na chama afanye yake tukomboe nchi hakuna namna sasa!
 
Huna akili kweli.badala upige kelele mumewenu magufuli aonyeshe zile 1.9tilion mnahangaika nabilion 1 yawabunge
 
  • Thanks
Reactions: PNC
nyie mnacheza na mpiga disco ?mnafikiri kaja kushangaa magorofa chadema? anakula ruzuku na michango ndiyo hiyo kisha piga nyie endeleeni kupiga picha magari ya miaka kumi iliyopita mwenzenu anakula hela na hakuna uchaguzi mwenyekiti wa maisha
 
Sasa kama Ndugai hawakati si unaona kabisba yuko nyuma ya huu mchezo?

Yeye kinamhusu nini kuibiwa au kukwapuliwa hela ndani ya chadema?

Kwanini asiendelee na utaratibu wake Wa kukata kama ilivyokua awali? Au kuna wabunge Wa Chadema waliomlalamikia kuhusu suala hilo?

Kua usitukate hela maana hatuoni au haturidhishwi na matumizi yake? Yaani ni kama unavyotoa sadaka na kuondoka, kuibiwa haikuhusu

Ndugai aache kusambaza na kuvumisha usanii wake Wa kutaka wenzao Chadema washindwe hata kujiendesha, hivyo kuipa ccm kushinda uchaguzi bila kupingwa na kutuletea maboya!
 
Ungetueleza kwanza kuhusu wizi wa 1.5 tln ambao watu wanfungwa midomo wasiuzungumzie
 
Sasa kama ndugai hawakati si unaona kabisa yuko nyuma ya huu mchezo? Yeye kinamhusu nini kuibiwa au kukwapuliwa hela ndani ya chadema? Kwanini asiendelee na utaratibu wake Wa kukata kama ilivyokua awali? Au kuna wabunge Wa chadema waliomlalamikia kuhusu suala hilo? Kua usitukate hela maana hatuoni au haturidhishwi na matumizi yake? Yaani ni kama unavyotoa sadaka na kuondoka, kuibiwa haikuhusu, Ndugai aache kusambaza na kuvumisha usanii wake Wa kutaka wenzao chadema washindwe hata kujiendesha, hivyo kuipa ccm kushinda uchaguzi bila kupingwa na kutuletea maboya!
Mbona hoja yako dhaifu Sana hi.Kama ndugai hawakati Hakuna tatizo si ina maana pesa wanabaki nazo wenyewe SI wazipeleke wenyewe.mfano mimi unatakiwa unikate laki moja kwenye mshahara wangu ili ziende chadema hujanikata Mimi SI nizipeleke.Mleta mada Yuko sahihi wamegoma kuchangia wangekuwa haeajagoma hizo pesa wangezipeleka wrnyewe kwa cash au kuagiza benki zao wa transfer hiyo michango toka kwenye akaunti zao ziende akaunti ya chadema.Wamegoma
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom