Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Zaidi ya Sh bilioni 10 zimetumika kujenga Kiwanda cha Chaki kinachomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu. Mradi huo uliotarajiwa kuwa miongoni mwa miradi ya kimkakati ya kuongeza mapato ya halmashauri, kuzalisha ajira na kuchochea uchumi wa eneo hilo, bado haujaanza uzalishaji licha ya ujenzi wake kukamilika na kufanyiwa majaribio.
Kwa muda mrefu sasa, wananchi wa Maswa wameendelea kusubiri kuona kiwanda hicho kikianza kufanya kazi, lakini matarajio hayo yameendelea kufifia huku majengo na mitambo vikisubiri kuanza kutumika.
Kwa mujibu wa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, changamoto kubwa iliyopo si ujenzi wa kiwanda bali ni ukosefu wa mtaji wa kuanzisha uzalishaji. Halmashauri inaeleza kuwa tayari iliwasilisha ombi serikalini la kupatiwa fedha za mtaji, lakini hadi sasa fedha hizo hazijatolewa.