Bilioni 2 ni nyingi ila ndogo kwa Simba, Next time mfanye 5 kwenda mbele

Bilioni 2 ni nyingi ila ndogo kwa Simba, Next time mfanye 5 kwenda mbele

Simba imepanda thamani, ni pesa ndogo sana.
Simba.imesambaa.nchi nzima wana uwezo wa chini kuuza jezi laki tano acha na vitu vingine kama kofia, bendera na bidhaz nyingine.
Kama kila jezi ni 20000 mauzo ni Bilioni 10 ukiondoa gharama nyingine wanapata si chini ya bilioni 5....
Ndilo swali langu
 
Mtazamo wako ni finyu sana.
Haujaainisha kwa miaka ya nyuma Simba walikuwa wakiingiza kiasi gani kwa mauzo ya "MERCHANDISE" zake...
Mkuu, hatupaswi kufungwa na mtizamo wa nyuma ikiwa tunaizungumzia Simba iliyomaliza nafasi ya kwanza kwenye group lenye timu kama Al ahly na As Vita.

Simba imekuwa kubwa sana kuanzia kwenye matokeo hadi nje ya uwanja.

Twende kwenye hoja.

Simba hii ya sahizi inayoingia robo fainali unadhani katika kipindi cha miaka miwili itauza chini ya pisi za jezi milioni moja?

Hapo ni jezi tuu, sijazungumzia vitu kama bendera, Madera, vipeperushi, mipira n.k

Nikukumbushe tuu kila msimu klabu za mpira huja na jezi zenye muundo mpya kwaajili ya biashara, kwa hiyo ndani ya miaka miwili watauza jezi za aina mbili tofauti kwa wateja wale wale.

Suala la kuwa na wataalam w biashara sio hoja, Simba inaweza ikawa ina wataalam wa biashara wenye maslahi binafsi, maana kibiashara ni wazi Simb imepigwa
 
Kwani kuna ulazima wa kuandika THREAD kwa jambo ulijui?
 
Hongera sana Simba na Vunja bei kwa makubaliano ya kihistoria mlioingia hii leo, kiukweli Simba imepiga hatua ukilinganisha na ilipokuwepo...
Yani jinsi ulivyopiga hayo mahesabu nakufananisha na mkulima wa matikiti kwenye mtandao....

Vunja Bei ataingia gharama za

1. Uzalishaji wa jezi
2. Usambazaji wa jezi
3. Kulipa wasambazaji
4. Kuwalipa simba bilioni 1 kwa mwaka yani 2 kwa miaka miwili...
5. Alipe kodi...

Baada ya hapo ndio anaanza kutafuta faida....

Kumbuka mkataba uliopita simba alikuwa anapata milioni 100 leo imefika bilioni 2 anakuja mtu anasema haitoshi bila hata kusubiri wajaribu hiyo risk....
 
Mtazamo wako ni finyu sana.
Haujaainisha kwa miaka ya nyuma Simba walikuwa wakiingiza kiasi gani kwa mauzo ya "MERCHANDISE" zake...
Hawa Simba wakishanyolewa club bingwa ndio kwisha habari yao nani atataka kununua jezi jekundu, hii business ina risk balaa is all about mood swing.
 
Hongera sana Simba na Vunja bei kwa makubaliano ya kihistoria mlioingia hii leo, kiukweli Simba imepiga hatua ukilinganisha na ilipokuwepo.

Twende kwenye facts sasa....
Kwa kuanzia sio mbaya, ukitegemea miaka ya nyuma simba alikuwa anapata 100M, after hiyo miaka miwili nategemea deal litakalosainiwa litakuwa kubwa zaidi ya hili la 2B
 
VB kajua kucheza na akili za mchezo na atapiga faida sana tu
 
Back
Top Bottom