Bilioni 2 zatengwa kwa wananchi watakaovamiwa na wanyama pori

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Serikali imesema imetenga shilingi bilioni mbili katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya kifuta jasho kwa wananchi wote watakaovamiwa na wanyama pori.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mary Masanja amesema hayo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Namtumbo Mhe.Vita Kawawa aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kufidia wananchi wanaoshambuliwa na wanyama pori ikiwemo Tembo.

Mhe. Masanja amesema serikali itatoa fidia kwa wananchi wote watakaovamiwa na wanyama kulingana na uharibifu utakaojitokeza.

Chanzo: ITV
 
Na wake watakaokatwa shingo na na kunyongwa na maji kana kule mbeya watafidiwa? Maana maji ya mito siku hizi no makali sana,yanakata watu vichwa.
 
Hiyo ni hela ya kula tu wamejitengea
 
Serikali imesema imetenga shilingi bilioni mbili katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya kifuta jasho kwa wananchi wote watakaovamiwa na wanyama pori.
🤣 tunaomba vigezo ili ku qualify kwenye malipo, nataka nikaswage tembo selous waje shambani kwangu Kisakitu
 
Serikali imesema imetenga shilingi bilioni mbili katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya kifuta jasho kwa wananchi wote watakaovamiwa na wanyama pori.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Mary Masanja amesema hayo bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Namtumbo Mhe.Vita Kawawa aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kufidia wananchi wanaoshambuliwa na wanyama pori ikiwemo Tembo.

Mhe. Masanja amesema serikali itatoa fidia kwa wananchi wote watakaovamiwa na wanyama kulingana na uharibifu utakaojitokeza.

Chanzo: ITV
Mimi naona kama walitakiwa wafanye the opposite. Badala ya kutenga fedha hizo kuja kufidia watu watakaouliwa na tembo, wangezitumia katika kuimarisha mkakati wa kuhakikisha kuwa wanyama pori hawasogelei kabisa makazi ya binadamu milele.
 
Back
Top Bottom