Tz shamba la bibiRamadhan Semtawa
- NI MARA TATU YA WIZI WA EPA;
- DCI MANUMBA ASEMA TAARIFA ZINAFANYIWA KAZI
WATU wasiofahamika wameghushi nyaraka za malipo na kuiba zaidi ya Sh300 bilioni katika benki tatu kubwa nchini na kusababisha mtikisiko mkubwa katika sekta ya fedha, uchunguzi umeonyesha.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu, kwa njia ya mtandao wa kompyuta na kuhusisha wezi wa kimataifa ndani na nje ya nchi.
Tukio hilo ambalo ni kubwa kuwahi kutikisa sekta ya fedha nchini tangu uhuru mwaka 1961, limetokea katika kipindi cha takribani miaka miwili tangu serikali ianzishe kitengo maalumu cha Intelejensia cha kufuatilia Mzunguko wa Fedha chafu (FIU).
Licha ya kuwepo FIU, ambayo iliundwa pamoja na Sheria ya Kupambana na Fedha Chafu ya mwaka 2007, uchunguzi wa Mwananchi, umebaini kutokea wizi huo mkubwa katika benki hizo.
Uchunguzi huo umebaini kwamba, taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo ambazo ni mara tatu ya zile za EPA zilizoibwa katika Benki Kuu Tanzania (BoT), zilihamishwa kwa njia ya kompyuta kwa kughushi malipo kwenda kwa wahusika wa mtandao huo katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako Polisi wa Kimataifa wa nchini na wenzao wanahaha kuzichunguza.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, alithibitisha kuwepo taarifa za uhalifu huo, lakini akaweka bayana, hakuna ushahidi wa kiwango maalumu kilichoibwa hadi sasa.
"Hizo taarifa zipo zinafanyiwa kazi, ila haijathibitika ni kiasi gani cha fedha kimeibwa na benki zipi hasa, kwa hiyo kusema ni Sh300 bilioni au zaidi ya hapo, si sahihi hakuna uthibitisho wowote," alifafanua DCI Kamishna Manumba.
DCI Manumba aliongeza kwamba, baada ya uchunguzi kukamilika polisi itatoa taarifa za kina, sahihi na kwa wakati kwa wananchi na kusisitiza, "Kwa sasa ngoja tufanye kazi."
Hata hivyo, DCI Manumba alionya na kuzitaka benki na watu wengine kuwa makini katika kuangalia usalama wa mali na fedha katika kipindi chote.
"Unajua, mambo ya uhalifu sisi tunajitahidi kukabiliana nayo lakini bado wengine wanaendelea kwa kutumia mbinu mbalimbali. Kwa mfano tunazuia watu wasibakwe, lakini wanabakwa, hii yote inaonyesha umuhimu wa watu kuwa makini," alifafanua DCI Manumba.
Gavana wa Benki Kuu (BoT) Profesa Benno Ndulu, alipoulizwa kuhusu sakata hilo alisema yuko nje ya nchi kikazi.
"Niko Sweden kikazi, halafu hapa siwezi kukusikia vizuri wala kuzungumza vema kwani kuna shughuli ambayo nimehudhuria," alisema Profesa Ndulu, ambaye taasisi kuu ya fedha ya nchi ina wajibu wa kusimamia benki na taasisi zote za fedha nchini.
Baadhi ya maofisa wa benki hizo ambazo majina yake tunayahifadhi, wamethibitisha kukumbwa na uhalifu huo mkubwa na kwamba wameacha suala hilo mikononi mwa vyombo vya dola.
"Ni kweli kuna vitenfo vya kughushi vimetokea katika benki yetu, lakini hilo hatuwezi kulizungumzia kwa kina kwasababu liko mikononi mwa vyombo vya dola. Polisi wanaweza kulizungumzia hilo," alifafanua ofisa kutoka moja ya benki iliyoibiwa kiasi kikubwa cha fedha karibu Sh100 bilioni.
Wakati DCI Kamishna Manumba, Gavana Ndulu na maofisa wa benki wakizungumzia hayo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, hadi sasa taarifa za awali zinaonyesha mpango huo mchafu umeanzia ndani ya benki kwa kuhusisha baadhi ya watu ambao ni wanamtandao na wezi wenzao nje ya nchi.
Mwananchi imebaini kwamba, hadi sasa Idara ya Interpol Tanzania kwa kushirikiana na wenzao wa nje wanafanya uchunguzi huo wa kina katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo zilikwenda.
Katika uchunguzi huo, Mwananchi imebaini kwamba baada ya mpango huo kufanywa nchini fedha hizo zinaonyesha zilihamishwa kwa njia hiyo ya kughushi kwenda nchi hizo.
Vyanzo hivyo vya habari za kiuchunguzi, zilifafanua kwamba baadhi ya watu katika mabenki hayo ambao wanafahamu mzunguko wa fedha ikiwemo malipo ya ndani na nje, wamepanga njama hizo na kughushi malipo kwa kushirikiana na mtandao mkubwa wa wezi wenzao wa nje ya mabenki ndani na nje.
Habari hizo za kiuchunguzi, zinaonyesha kwamba wizi huo umetikisa mabenki hayo kiuchumi huku duru za kiusalama zikisema vyombo vya usalama vimekuwa makini kuangalia fedha hizo zimeingia mikononi mwa watu gani.
Mwananchi imebaini kwamba, kiasi hicho kikubwa cha fedha kinaweza kuweka usalama wa taifa hatarini endapo kitakuwa kimeingia kwenye mikono ya watu ambao wana nia mbaya na nchi.
"Ni kiasi kikubwa cha fedha, kama kitakuwa kimeingia kwenye mikono ya watu hatari wanaweza kuhatarisha usalama wa nchi, bilioni 300 si kitu kidogo," kilisema chanzo kimoja kutoka moja ya vyombo vya usalama.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, kitisho kingine kinachoangaliwa hadi sasa ni iwapo fedha hizo zimeibwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba kwa ajili ya kundi fulani ikiwemo mafisadi kutaka kuzitumia kutimiza malengo yao.
"Tunaangalia pia, maana inawezekana ni mafisadi wakubwa ambao wanajua mzunguko wa fedha ndiyo wamekula njama na kutaka kuhujumu nchi kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu," kilifafanua chanzo hicho.
Ingawa haijathibitika, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kuliibuka ufisadi mkubwa katika BoT ambao zaidi ya Sh 133 bilioni ziliibwa.
Wapo bize wanachungulia JF tunaandika nini badala ya kulinda uchumi wa nchi
Si uzito wa kujifunza bali ni madhara yatokanayo na mabenki yote makubwa kutotaka kuajiri wa Tanzania na hasa ambao hawajasoma au kufanya kazi nje. Uongozi wa juu wa mabaenki ni kutoka nje hivyo wao kudhani kuwa watu huku wamelala na kuleta technolojia zilizokwisha muda wake nje hapa basi watalizwa zaidi. Nilishangaa kuona benki moja ina ATM zilizopakwa rangi ukiwa mchunguzi utajua zimetunika, sijui nazo zinapata baraka ya 'new technology'?Haya ni madhara ya kutumia technology bila kwanza kuweka wataalamu [waaminifu] wa kutosha kwenye mabenki, sheria, polisi na utawala.
Historia inatuambia tuko wazito mno kujifunza, matukio kama haya yatatokea mara nyingi tu huko mbeleni.
Whatch this space!
Ndugu wananchi,
Nashukuru sana kwa ufala na ujinga wenu na umbumbumbu na uzoba milonao unaonifanya mimi na wajanja wenzangu tuishi kwa raha mustarehe.
Kwanza pamoja na kuwa tuliiba hela nyingi wakati wa uchaguzi wa majuzi, mlitushindisha kwa kishindo maana nyie ni mafala na vipofu msioona! Hata mlipoambiwa na wale ambao hawakupata mgao hamkuonyesha kukerwa na tulipoona mko hivyo, tukasitisha hata majadiliano. Sasa tumeamua kuchota za kutosha tuwapikieni na pilau maana mungu wa wajinga kama nyie ni matumbo yenu. Mkishakula mtatupa tu kura zenu kama kawa tumalizie kabisa kilichosalia humo.
Ahsanteni kwa kunisikiza,
mbaff zenu,
Wenu Rawofia Serpentina,
President, Nchitata!
Mi SIJASEMA MWENZIO 😕ukweli wa mambo mi siami kama ni wezi tu hizo pesa zitakuwa zauchaguzi,why kila uchaguzi ukikaribia pesa nyingi sana zinapotea,kwa mtindo huu hii nchi kuendelea itakuwa ndoto
wakati habari za wizi wa kimafia wa sh300 bilioni zikiwa zimeistua serikali, watu kumi wamekamatwa kwa tuhuma za wizi mwingine wa aina hiyo uliohusisha sh360 milioni za benki moja nchini.
Kukamatwa kwa watu hao kumetokea siku moja baada ya gazeti la mwananchi kuripoti wizi huo mkubwa unaotumia teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta ambao ulifanyika kwenye benki nne kubwa nchini, taarifa iliyofanya mamlaka ya mapato (tra) kuanza uchunguzi.
Mbali na taarifa za kukamatwa kwa watu hao, vyombo vya habari pia vimeripoti kukamatwa kwa mfanyabiashara mmoja aliyekuwa akifanya jaribio la kuiba kimafia sh221 milioni kutoka benki ya nbc.
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ambazo zilithibitishwa na msemaji wa jeshi la polisi, kamishna msaidizi abdallah msika zinasema watu hao walikamatwa kati ya februari na machi, katika msako wa jeshi hilo kwenye mikoa ya dar es salaam, shinyanga na zanzibar.
Kukamatwa kwa watu hao kumetokea wakati benki zimekuwa zikihaha kubadili na kuboresha mifumo yake ya kuchukua na kutoa fedha kwa njia ya elektroniki kwa lengo la kukabiliana na uhalifu uliokithiri unaofanywa na watu walio ndani na nje ya nchi.
Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao, mssika alisema watano kati yao ni wafanyakazi wa benki hiyo (jina tunalo kwa sababu za kimaadili) na wengine ni kutoka nje ya benki hiyo na kuongeza: "hadi sasa uchunguzi bado unaendelea.
"wote wanatuhumiwa kwa wizi huohuo wa mtandao... Baada ya kufanyika uchunguzi walibainika kuwa ni sehemu ya mtandao ambaon inatuhumiwa unahusika kwenye wizi huo."
kwa mujibu wa taarifa hizo zilizothibitishwa na mssika, wizi huo ulifanyika katika kipindi cha kuanzia januari lakini ulibainika kati ya februari na ndipo uchunguzi ukaanza.
Msika alifafanua kuwa baada ya kufanyika uchunguzi ilibainika kiasi hicho cha fedha kilihamishwa kutoka tawi moja jijini dar es salaam na kupelekwa tawi jingine la mkoani shinyanga.
Alisema baada ya kuhamishiwa tawi la shinyanga, fedha hizo zilianza kuingizwa kwenye akaunti mbalimbali za wahusika ndipo baadhi yao waliponaswa.
"fedha zilitoka tawi la dar es salaam na kupelekwa tawi la shinyanga, baada ya kufika shinyanga zilianza kuingizwa kwenye akaunti mbalimbali za watuhumiwa... Tayari hao kumi wamekamatwa kuhusika na tukio hilo," alifafanua msemaji huyo wa polisi.
Kuhusu kiasi cha fedha, alisema hadi sasa zimepatikana sh319.5 milioni kati ya sh360 milioni zilizoibwa na kwamba juhudi za kusaka nyingine na watuhumiwa zinaendelea.
Mssika aliongeza kwamba baada ya watuhumiwa wengine kukamatwa, watajumuishwa katika kesi inayowakabili watu hao kumi walio mikononi mwa polisi.
Katika hatua nyingine, mssika alisema jeshi la polisi limetaka benki yoyote ambayo imekumbwa na tuhuma za wizi huo wa mtandao ziwasilishe taarifa zao polisi.
Mssika, ambaye alilirudia kauli ya mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai (dci), kamishna robert manumba kuhusu taarifa za wizi mkubwa katika mabenki matatu, alisema hadi sasa hawajapata taarifa hizo kuhusu kiwango kilichoibwa na benki husika.
Wizi wa mtandao umekuwa ukikua kwa kasi nchini kutokana na matukio yaliyozikumba benki na tayari kuna kesi mbalimbali zinazohusisha wafanyabiashara wa morogoro, walioba zaidi ya sh1 bilioni katika moja ya benki nchini.
Lakini vyombo vya usalama ikiwemo polisi na mamlaka za serikali zimekuwa zikijaribu kufunika uhalifu huo.
Juzi wataalamu wa kubaini uhalifu wa kughushi kutoka afrika kusini walikuwa jijini dar es salaam kuangalia wizi mkubwa katika moja ya benki kati ya tatu zilizokumbwa na wizi huo wa kimafia wa sh300 bilioni.
Benki hiyo ambayo inatajwa kuwa iliibiwa kiasi hicho kikubwa cha fedha, kwa sasa imeanza kurekebisha mfumo wake wa usalama wa fedha, hali ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa kwa wateja wake kwa takriban wiki nne sasa.
Tayari maafisa wadogo wanne wa benki hiyo wameshaondolewa katika nafasi zao kwa ajili ya kupisha uchunguzi zaidi kubaini uhalifu huo na mtandao wake.
Uchunguzi wa wizi huo unahusisha pia maafisa waandamizi ambao wanatuhumiwa kuwa wanaweza kushirikiana na mtandao wa wahalifu wa kughushi kufanikisha wizi huo wa kimafia.
Mwaka 2005/2006 benki kuu (bot) iliibiwa zaidi ya sh133 bilioni katika akaunti moja ya malipo ya madeni ya nje (epa) baada ya watu kughushi nyaraka zilizoonyesha kuwa walirithishwa madeni na makampuni ya nne na hivyo kujivunia mabilioni ya fedha.
Hadi sasa, wafanyabiashara kadhaa pamoja na wafanyakazi wa bot wameshafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kula njama na kuiba fedha hizo,
hata hivyo, baadhi ya walioiba hawakufikishwa mahakamani baada ya rais jakaya kikwete kutoa msamaha kwa wale ambao wangezirudisha kabla ya novemba mosi mwaka 2008.
Mbali na waliorejesha kiasi cha sh70 bilioni, waliokwapua kiasi cha sh40 bilioni pia hawajafikishwa mahakamani kutokana na wizi huo kuhusisha makampuni mengine yaliyo nje ya nchi na hivyo uchunguzi kuhitaji nguvu kubwa zaidi kuweza kuwabaini wahusika.
Source: Mwananchi