Bilioni 300 zaibiwa kimafia Dar...

Bilioni 300 zaibiwa kimafia Dar...

wizi bongo unatokea kutokana na mchanyiko wa mambo, hasira ya wafanyakazi juu ya viongozi wao ambao ni wezi, kuajiriwa kwa kutoa rushwa hivyo mwajiria kutaka kurudisha kilicho chake, mishahara midogo, kuajiri watu bila kufuata uwezo wa mtu, hivyo uwezekano wa kuwa mwaminifu upo mdogo.
 
  • NI MARA TATU YA WIZI WA EPA;
  • DCI MANUMBA ASEMA TAARIFA ZINAFANYIWA KAZI
Ramadhan Semtawa

WATU wasiofahamika wameghushi nyaraka za malipo na kuiba zaidi ya Sh300 bilioni katika benki tatu kubwa nchini na kusababisha mtikisiko mkubwa katika sekta ya fedha, uchunguzi umeonyesha.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu, kwa njia ya mtandao wa kompyuta na kuhusisha wezi wa kimataifa ndani na nje ya nchi.

Tukio hilo ambalo ni kubwa kuwahi kutikisa sekta ya fedha nchini tangu uhuru mwaka 1961, limetokea katika kipindi cha takribani miaka miwili tangu serikali ianzishe kitengo maalumu cha Intelejensia cha kufuatilia Mzunguko wa Fedha chafu (FIU).

Licha ya kuwepo FIU, ambayo iliundwa pamoja na Sheria ya Kupambana na Fedha Chafu ya mwaka 2007, uchunguzi wa Mwananchi, umebaini kutokea wizi huo mkubwa katika benki hizo.

Uchunguzi huo umebaini kwamba, taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo ambazo ni mara tatu ya zile za EPA zilizoibwa katika Benki Kuu Tanzania (BoT), zilihamishwa kwa njia ya kompyuta kwa kughushi malipo kwenda kwa wahusika wa mtandao huo katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako Polisi wa Kimataifa wa nchini na wenzao wanahaha kuzichunguza.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, alithibitisha kuwepo taarifa za uhalifu huo, lakini akaweka bayana, hakuna ushahidi wa kiwango maalumu kilichoibwa hadi sasa.

"Hizo taarifa zipo zinafanyiwa kazi, ila haijathibitika ni kiasi gani cha fedha kimeibwa na benki zipi hasa, kwa hiyo kusema ni Sh300 bilioni au zaidi ya hapo, si sahihi hakuna uthibitisho wowote," alifafanua DCI Kamishna Manumba.

DCI Manumba aliongeza kwamba, baada ya uchunguzi kukamilika polisi itatoa taarifa za kina, sahihi na kwa wakati kwa wananchi na kusisitiza, "Kwa sasa ngoja tufanye kazi."

Hata hivyo, DCI Manumba alionya na kuzitaka benki na watu wengine kuwa makini katika kuangalia usalama wa mali na fedha katika kipindi chote.

"Unajua, mambo ya uhalifu sisi tunajitahidi kukabiliana nayo lakini bado wengine wanaendelea kwa kutumia mbinu mbalimbali. Kwa mfano tunazuia watu wasibakwe, lakini wanabakwa, hii yote inaonyesha umuhimu wa watu kuwa makini," alifafanua DCI Manumba.

Gavana wa Benki Kuu (BoT) Profesa Benno Ndulu, alipoulizwa kuhusu sakata hilo alisema yuko nje ya nchi kikazi.

"Niko Sweden kikazi, halafu hapa siwezi kukusikia vizuri wala kuzungumza vema kwani kuna shughuli ambayo nimehudhuria," alisema Profesa Ndulu, ambaye taasisi kuu ya fedha ya nchi ina wajibu wa kusimamia benki na taasisi zote za fedha nchini.

Baadhi ya maofisa wa benki hizo ambazo majina yake tunayahifadhi, wamethibitisha kukumbwa na uhalifu huo mkubwa na kwamba wameacha suala hilo mikononi mwa vyombo vya dola.

"Ni kweli kuna vitenfo vya kughushi vimetokea katika benki yetu, lakini hilo hatuwezi kulizungumzia kwa kina kwasababu liko mikononi mwa vyombo vya dola. Polisi wanaweza kulizungumzia hilo," alifafanua ofisa kutoka moja ya benki iliyoibiwa kiasi kikubwa cha fedha karibu Sh100 bilioni.

Wakati DCI Kamishna Manumba, Gavana Ndulu na maofisa wa benki wakizungumzia hayo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, hadi sasa taarifa za awali zinaonyesha mpango huo mchafu umeanzia ndani ya benki kwa kuhusisha baadhi ya watu ambao ni wanamtandao na wezi wenzao nje ya nchi.

Mwananchi imebaini kwamba, hadi sasa Idara ya Interpol Tanzania kwa kushirikiana na wenzao wa nje wanafanya uchunguzi huo wa kina katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo zilikwenda.

Katika uchunguzi huo, Mwananchi imebaini kwamba baada ya mpango huo kufanywa nchini fedha hizo zinaonyesha zilihamishwa kwa njia hiyo ya kughushi kwenda nchi hizo.

Vyanzo hivyo vya habari za kiuchunguzi, zilifafanua kwamba baadhi ya watu katika mabenki hayo ambao wanafahamu mzunguko wa fedha ikiwemo malipo ya ndani na nje, wamepanga njama hizo na kughushi malipo kwa kushirikiana na mtandao mkubwa wa wezi wenzao wa nje ya mabenki ndani na nje.

Habari hizo za kiuchunguzi, zinaonyesha kwamba wizi huo umetikisa mabenki hayo kiuchumi huku duru za kiusalama zikisema vyombo vya usalama vimekuwa makini kuangalia fedha hizo zimeingia mikononi mwa watu gani.

Mwananchi imebaini kwamba, kiasi hicho kikubwa cha fedha kinaweza kuweka usalama wa taifa hatarini endapo kitakuwa kimeingia kwenye mikono ya watu ambao wana nia mbaya na nchi.

"Ni kiasi kikubwa cha fedha, kama kitakuwa kimeingia kwenye mikono ya watu hatari wanaweza kuhatarisha usalama wa nchi, bilioni 300 si kitu kidogo," kilisema chanzo kimoja kutoka moja ya vyombo vya usalama.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kitisho kingine kinachoangaliwa hadi sasa ni iwapo fedha hizo zimeibwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba kwa ajili ya kundi fulani ikiwemo mafisadi kutaka kuzitumia kutimiza malengo yao.

"Tunaangalia pia, maana inawezekana ni mafisadi wakubwa ambao wanajua mzunguko wa fedha ndiyo wamekula njama na kutaka kuhujumu nchi kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu," kilifafanua chanzo hicho.

Ingawa haijathibitika, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kuliibuka ufisadi mkubwa katika BoT ambao zaidi ya Sh 133 bilioni ziliibwa.
Tz shamba la bibi
 
MSEMAJI wa Jeshi la Polisi Kamanda Msika
Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi nchini limesema halina taarifa za wizi wa shilingi Bilioni 300 zinazodaiwa kuibwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kutoka katika mabenki mbalimbali yaliyounganishwa na mtandao huo hapa nchini.

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, amesema leo kuwa taarifa zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na wizi huo hazijafikishwa Polisi.

Kamanda Mssika amesema kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kamishna Robert Manumba, aliyedaiwa kukaririwa na chombo hicho cha habari, amesema kuwa hana taarifa ya tukio la wizi wa shilingi Bilioni 300.

Kamishna Manumba amesema kuwa mawasiliano kati yake yeye na Mwandishi wa taarifa hiyo kwa upande wake binafsi yalihusu tukio la wizi wa fedha katika benki ya NMB Tawi la Bank House Jijini Dar es Salaam ambapo mwanzoni mwa mwezi Februari mwaka huu, Jeshi la Polisi lilibaini kuibwa kwa shilingi milioni 360 kwa njia ya mtandao wa kompyuta fedha ambazo zilihamishiwa katika tawi moja wapo la benki hiyo lililopo mkoani Shinyanga.

Kamanda Mssika amefafanua kuwa, mara baada ya fedha hizo kufika Mkoani Shinyanga, zilitawanywa kutoka katika tawi hilo na kupelekwa kwa njia ya mtandao wa kompyuta kwenda katika akaunti mbalimbali za watu binafsi kwenye matawi mengine ya benki hiyo katika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Kutokana na wizi huo Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Benki ya NMB limeshafanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 319 kati ya shilingi milioni 360 zilizoibwa na kwamba tayari baadhi ya watuhumiwa waliohusika katika wizi huo wakiwemo watumishi watano wa benki wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu shitaka lao.

Hata hivyo Kamanda Mssika amesema kutokana na taarifa za kuibwa kwa shilingi bilioni 300, kama ilivyoandikwa, ametoa wito kwa Makampuni ama Taasisi za Kifedha zinazoweza kuwa zimefanyiwa hujuma hiyo ya wizi na iwapo rasimu zao za ndani kiuchunguzi zimekamilika, basi wawasiliane na Mkurugenzi wa makosa ya Jinai nchini Kamishna Robert Manumba, ili hatua za uchunguzi ipasavyo kwa kuvishirikisha vyombo vya dola ziweze kuchukuliwa haraka iwezekanavyo.

Source: http://bashir-nkoromo.blogspot.com/
 
Hold on inawezekana hawa jamaa walisikia habari za wizi wa majuzi wa mafia wa Kirusi walioiba mamilioni ya dola kwa kutumia credit cards sehemu mbalimbali duniani na miongoni mwao wakiwa tayari wamedakwa na FBI?
 
Wizi wa namna hii unasaidia uwekezaji wa wazalendo manake kwa mazingira ya kawaida mwananchi wa manzese kuwa bilionea ni ndoto njia za mkato zinakubalika sometimes manake wameuza unga kutoka bado sasa kwanini wasibuni nji mbadala.

Wenyewe wanajua mtajua na itachukua muda kuwagundua, naomba wawe wa TZ ili pesa ziwe na impact humu ndani. Kila mtu anataka kundesha vogel sasa wafanyeje manake kama siasa majina ni hayo hayo miaka nenda rudi, kwakuwa brain imetumika then wishing them good lucky.
 
Haya ni madhara ya kutumia technology bila kwanza kuweka wataalamu [waaminifu] wa kutosha kwenye mabenki, sheria, polisi na utawala.

Historia inatuambia tuko wazito mno kujifunza, matukio kama haya yatatokea mara nyingi tu huko mbeleni.

Whatch this space!
Si uzito wa kujifunza bali ni madhara yatokanayo na mabenki yote makubwa kutotaka kuajiri wa Tanzania na hasa ambao hawajasoma au kufanya kazi nje. Uongozi wa juu wa mabaenki ni kutoka nje hivyo wao kudhani kuwa watu huku wamelala na kuleta technolojia zilizokwisha muda wake nje hapa basi watalizwa zaidi. Nilishangaa kuona benki moja ina ATM zilizopakwa rangi ukiwa mchunguzi utajua zimetunika, sijui nazo zinapata baraka ya 'new technology'?
Viongozi wamabenki amkeni watu wanakimbia kasi ya ULAYA!!! Mkalage baho
 
Wizi wa bilioni 300 waitisha Mamlaka ya MapatoRamadhan Semtawa

WIZI wa zaidi ya Sh 300bilioni uliozikumba benki tatu kubwa nchini umezichanganya mamlaka za serikali na taasisi za fedha na tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imeanza uchunguzi kuona kama kuna athari zozote zinazoweza kusababishwa na ufisadi huo.

Wizi huo ambao kwa jumla ni zaidi ya makusanyo ya kodi kwa mwezi, umetikisa mabenki matatu makubwa (majina tunayo kwa sababu za kibiashara) kipindi ambacho tayari taasisi hizo zilipigwa na mawimbi ya mtikiso wa uchumi wa dunia.

Kamishna mkuu wa TRA, Harry Kitillya aliiambia Mwananchi ofisini kwake jana kuwa ingawa hadi jana mchana hakukuwa na taarifa za wizi wa fedha za kodi katika mabenki mbalimbali nchini, wamelazimika kufuatilia sakata hilo kwa karibu.

Kwa mujibu wa Kamishna Kitillya, fedha za kodi zinapokuwa ndani ya benki zikipotea benki husika ndiyo inawajibika na "lakini tumeona ni vema na sisi tuanze kufuatilia kwa karibu".

Mkuu huyo wa mamlaka ya mapato alifafanua kwamba kiutaratibu benki ambazo kuna akaunti ya TRA hupaswa kuingiza fedha za makusanyo ya kodi kwenda akaunti ya mamlaka hiyo iliyo BoT mara tisa kwa mwezi.

Alifafanua kuwa fedha hizo zinapaswa kuwekwa kwenye akaunti hiyo kila Jumatatu na Jumatano ya juma na mara moja kila mwisho wa mwezi.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, TRA italazimika kufanya uchunguzi kutokana na kuhofu kitisho kama kilichowahi kuikumba katika sakata la Sh 4.5 bilioni kutoka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), ambazo hazikulipwa na kuingia mifukoni mwa wajanja hadi mamlaka ilivyostuka na kuuliza uongozi wa kampuni hiyo ya simu.

"Tutachunguza kwa sababu kodi yetu kutoka TTCL iliingia mifukoni mwa wajanja hadi tulipoamua kuchunguza, inawezekana tukafikiri kila kitu ni salama lakini kumbe sivyo kwa hiyo tutachunguza," alisisitiza Kamishna Kitillya.

Alifafanua kuwa baada ya kuchunguza ilibainika TTCL ilikuwa imekwishalipa kodi hiyo, lakini wajanja wachache walishirikiana na watu wasio waaminifu na kuitia mfukoni.

Kwa mujibu wa mkuu huyo, TRA iko makini kuhakikisha mzunguko wa fedha zake za kodi uko salama na kuonya kwamba, haitasita kuwashughulikia watakaohusika na upotevu wa fedha za kodi ya nchi.

"Sisi tukiona mambo hayaendi vizuri tunachukua Takukuru tu wanashughulika, tuna imani kubwa na taasisi hii na hata katika lile sakata la TTCL tuliwachukua wao kulishughulikia, hatuna utani na fedha za kodi," alionya mkuu huyo.

Mtaalamu mmoja kutoka Wizara ya Fedha na Uchumi, alisema mabenki yaliyoibiwa kila moja inaweza kuwa na fedha kati ya Sh200 bilioni hadi Sh300 bilioni kutokana na kuwa na mtandao mkubwa wa wateja hadi nje ya nchi.

"Haya mabenki matatu ni makubwa, yote ni ya kigeni yana mtandao mkubwa wa wateja kutoka ndani na nje ya nchi, wanaweza kuwa na mtaji kwa sababu kuna makampuni makubwa ya nje yanaweka fedha zao," alisema ofisa huyo.

Kwa upande mwingine, ofisa huyo alifafanua kwamba ni rahisi kuweza kukamata kiasi cha fedha kilichoibwa na kuingizwa nchini Marekani kutokana na nchi hiyo kuwa na mfumo imara wa kuangalia mzunguuko wa fedha katika mabenki.

Aliweka bayana kwamba, mtu yeyote mgeni anayelipwa kuanzia dola 4,000 za Kimarekani huanza kufuatiliwa nyendo zake na benki hulamizika kuwa na maelezo ya kutosha kuhusu wapi fedha hizo zilitoka na zina uhusiano gani na mhusika.

"Kwa hiyo kama fedha hizi zimelipwa kwa mgeni, kabla ya kufanya hivyo benki itapaswa kuwa na melezo ya kutosha kuhusu anayelipwa na zilikotoka fedha hizo, wao huanza kutilia shaka fedha kuanzia dola kati ya 4,000 na kuendelea mbele," kilifafanua chanzo hicho.

Mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni mwa mwaka huu, mabenki matatu ambayo yana mtandao wa kimataifa yalikumbwa na tuhuma za wizi huo wa kisasa.

Wizi huo umefanyika takribani miaka miwili na nusu tangu serikali ianzishe kitengo cha Financial Intelligency Unit (FIU) ambacho kiliundwa sambamba na Sheria ya Kupambana na Fedha Chafu ya mwaka 2007.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini taarifa za awali za Polisi wa Kimataifa (Interpol) zinaonyesha fedha hizo zilihamishwa kwa njia ya kompyuta kwa kughushi malipo kwenda kwa wahusika wa mtandao huo katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani.

Alipoulizwa kuhusu sakata hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba alithibitisha kuwepo kwa taarifa za uhalifu huo lakini akaweka bayana, hakuna ushahidi wa kiwango maalumu kilichoibwa hadi sasa.

"Hizo taarifa zipo zinafanyiwa kazi lakini haijathibitika ni kiasi gani cha fedha kimeibwa na ni benki zipi hasa. Kwa hiyo kusema ni Sh300 bilioni au zaidi ya hapo, si sahihi... hakuna uthibitisho wowote," alifafanua Kamishna Manumba.

Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu alisema jana kuwa hana taarifa zozote za wizi wa fedha hizo na kwamba taasisi hiyo imeshtushwa na taarifa hizo, huku akisisitiza kuwa sekta ya fedha hapa nchini iko salama.

Gavana Ndulu alisema benki zimekuwa zinapata faida tena hakuna taarifa zozote zinazoonyesha kuwa kumefanyika wizi mkubwa namna hiyo katika benki za hapa nchini, huku akinukuu taarifa ya mabenki hayo ya mwezi Februari mwaka huu.

"Nitawauliza watu wa mabenki waniambie unawezaje ukatokea wizi mkubwa namna hiyo halafu regulator (msimamizi) asiwe na taarifa," alisema Ndulu.

Huku akilihakikishia gazeti hili kuwa ni vigumu sana katika sekta ya benki hapa nchini kuibiwa na kwamba kama kutakuwa na wizi huo basi hakuna taarifa zozote ambazo zimepelekwa rasmi ofisini kwake.

"Mfumo wa sasa wa TISS unaotumiwa na BoT na mabenki (TISS) hauna tatizo lolote maana mawasiliano yake yanaratibiwa na BoT," alisema Gavana Ndulu.

Gavana Ndulu alisema kwamba akiba (total deposit) iliyoko katika benki za hapa nchini mpaka mwishoni mwa mwaka jana ilikuwa Sh7.8 trilioni na fedha zilizokopeshwa kwenye sekta binafsi ni zaidi ya Sh4 trilioni.

Taarifa za ndani kutoka katika kitengo cha ufuatiliaji wa wizi mtandaoni cha Jeshi la Polisi zinasema kuwa kumekuwa na taarifa ambazo zinawahusisha wafanyakazi wa mabenki wenyewe katika wizi huo.

Ofisa mmoja wa kitengo hicho ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa madai kuwa si msemaji wa kitengo hicho, katika kesi ambazo wamekuwa wanazifanyia uchunguzi nyingi huwahusisha wafanyakazi wa benki husika.

"Tatizo hilo ni kubwa sana katika mabenki yetu hapa nchini…. na tatizo ni kwa wanaofanya hizo ‘transactions’ inabidi mabenki yafanye mabadiliko makubwa sana," alisema.

Aliongeza kuwa taarifa za wizi mkubwa unaotokea katika mabenki kupitia mtandao zinapatikana wakati fedha zimeshaibwa.

Naye mkurugenzi wa benki ya CRDB, Dk Charles Kimei alisema kumekuwa na tatizo katika kupata taarifa sahihi za hundi kutokana na benki moja kutaka kujiridhisha kutoka benki nyingine, lakini kitendo hicho kinakuwa kigumu.

"Nimeisikia taarifa hiyo ya mabenki kulizwa, lakini napenda kukuhakikishia kuwa sisi tuko salama kabisa hapa… na tutaendelea kuwa makini katika kusimamia masuala yote ya kibenki (transactions)," alisema Dk Kimei.

Alisema kinachoziponza benki nyingi ni kujaribu kufanya uhamisho wa fedha kwa haraka zaidi kupitia mtandao bila kijiridhisha kwanza, kama inavyoshauriwa na wataalamu wa masuala ya kibenki.

"Tumekuwa tunatukanwa sana kwamba tunafanya kazi taratibu sana… lakini siku zote tumekuwa tunawaambia wateja wetu kuwa usalama wa fedha zao ndio jambo kubwa kwetu na tunalisimamia siku zote," alisema Dk Kimei.

Aliongeza kuwa "sisi tuko radhi kutukanwa kuliko kuingia katika makosa ambayo yanaweza kuigharimu benki na kupoteza imani kwa wateja wetu ambao wamekuwa wakifurahia jinsi benki yetu ilivyo makini".

Alisema sekta za kibenki zinatakiwa kurudi katika njia zake za zamani kwa kuwa kama suala la usalama wa fedha halitaangaliwa mapema, kutakuwa na tatizo kubwa katika benki za hapa.

Tuhuma za wizi wa fedha katika mabenki kwa njia ya mtandao wa kompyuta zilianza kuripotiwa katika vyombo vya habari mwezi Septemba mwaka jana wakati gazeti la The East African liliporipoti kuwa benki ziliibiwa zaidi ya Sh100 bilioni. Hata hivyo, tokea wakati huo, ni watuhumiwa wachache tu ndio wamefikishwa mahakamani.

imeanza uchunguzi kuona kama kuna athari zozote zinazoweza kusababishwa na ufisadi huo.
Ni utani au? Nani aliyewahi kufukuzwa kazi kwasababu ya wizi wa hela TRA, NSSF, PPF n.k?
Hii nchi ina wenyewe?
 
Ndugu wananchi,
Nashukuru sana kwa ufala na ujinga wenu na umbumbumbu na uzoba milonao unaonifanya mimi na wajanja wenzangu tuishi kwa raha mustarehe.
Kwanza pamoja na kuwa tuliiba hela nyingi wakati wa uchaguzi wa majuzi, mlitushindisha kwa kishindo maana nyie ni mafala na vipofu msioona! Hata mlipoambiwa na wale ambao hawakupata mgao hamkuonyesha kukerwa na tulipoona mko hivyo, tukasitisha hata majadiliano. Sasa tumeamua kuchota za kutosha tuwapikieni na pilau maana mungu wa wajinga kama nyie ni matumbo yenu. Mkishakula mtatupa tu kura zenu kama kawa tumalizie kabisa kilichosalia humo.

Ahsanteni kwa kunisikiza,
mbaff zenu,

Wenu Rawofia Serpentina,
President, Nchitata!
 
mzee naona leo umeamua kuamsha hasira za wanachi.............. hahaha.............. nzuri sana mwalimu kilima cha sera.............
 
Ndugu wananchi,
Nashukuru sana kwa ufala na ujinga wenu na umbumbumbu na uzoba milonao unaonifanya mimi na wajanja wenzangu tuishi kwa raha mustarehe.
Kwanza pamoja na kuwa tuliiba hela nyingi wakati wa uchaguzi wa majuzi, mlitushindisha kwa kishindo maana nyie ni mafala na vipofu msioona! Hata mlipoambiwa na wale ambao hawakupata mgao hamkuonyesha kukerwa na tulipoona mko hivyo, tukasitisha hata majadiliano. Sasa tumeamua kuchota za kutosha tuwapikieni na pilau maana mungu wa wajinga kama nyie ni matumbo yenu. Mkishakula mtatupa tu kura zenu kama kawa tumalizie kabisa kilichosalia humo.

Ahsanteni kwa kunisikiza,
mbaff zenu,

Wenu Rawofia Serpentina,
President, Nchitata!

Sasa hizo ( Bilioni 300 zimeyeyuka) kivipi mbona hutufafanuli?na hao waliokula mbona hujawataja Unasema tu kimafumbo fumbo Mkuu President, Nchitata!? Mwaga Mtama kwenye njiwa Wengi.Na hao waliokula Wamo ndani ya Serikali, na Serikali imewachukulia hatuwa gani?au ndio hao hao walikuwemo ndani ya hiyo Serikali ndio walaji?nakuomba utufafanulie Mkuu President, Nchitata! Ama kweli Waswahili husema Wajinga ndio waliwao kazi kweli ipo hapa bongo.
 
NI MARA TATU YA WIZI WA EPA;DCI MANUMBA ASEMA TAARIFA ZINAFANYIWA KAZI
Ramadhan Semtawa

WATU wasiofahamika wameghushi nyaraka za malipo na kuiba zaidi ya Sh300 bilioni katika benki tatu kubwa nchini na kusababisha mtikisiko mkubwa katika sekta ya fedha, uchunguzi umeonyesha.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti hili, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu, kwa njia ya mtandao wa kompyuta na kuhusisha wezi wa kimataifa ndani na nje ya nchi.

Tukio hilo ambalo ni kubwa kuwahi kutikisa sekta ya fedha nchini tangu uhuru mwaka 1961, limetokea katika kipindi cha takribani miaka miwili tangu serikali ianzishe kitengo maalumu cha Intelejensia cha kufuatilia Mzunguko wa Fedha chafu (FIU).

Licha ya kuwepo FIU, ambayo iliundwa pamoja na Sheria ya Kupambana na Fedha Chafu ya mwaka 2007, uchunguzi wa Mwananchi, umebaini kutokea wizi huo mkubwa katika benki hizo.

Uchunguzi huo umebaini kwamba, taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo ambazo ni mara tatu ya zile za EPA zilizoibwa katika Benki Kuu Tanzania (BoT), zilihamishwa kwa njia ya kompyuta kwa kughushi malipo kwenda kwa wahusika wa mtandao huo katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako Polisi wa Kimataifa wa nchini na wenzao wanahaha kuzichunguza.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Manumba, alipoulizwa ofisini kwake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, alithibitisha kuwepo taarifa za uhalifu huo, lakini akaweka bayana, hakuna ushahidi wa kiwango maalumu kilichoibwa hadi sasa.

"Hizo taarifa zipo zinafanyiwa kazi, ila haijathibitika ni kiasi gani cha fedha kimeibwa na benki zipi hasa, kwa hiyo kusema ni Sh300 bilioni au zaidi ya hapo, si sahihi hakuna uthibitisho wowote," alifafanua DCI Kamishna Manumba.

DCI Manumba aliongeza kwamba, baada ya uchunguzi kukamilika polisi itatoa taarifa za kina, sahihi na kwa wakati kwa wananchi na kusisitiza, "Kwa sasa ngoja tufanye kazi."

Hata hivyo, DCI Manumba alionya na kuzitaka benki na watu wengine kuwa makini katika kuangalia usalama wa mali na fedha katika kipindi chote.

"Unajua, mambo ya uhalifu sisi tunajitahidi kukabiliana nayo lakini bado wengine wanaendelea kwa kutumia mbinu mbalimbali. Kwa mfano tunazuia watu wasibakwe, lakini wanabakwa, hii yote inaonyesha umuhimu wa watu kuwa makini," alifafanua DCI Manumba.

Gavana wa Benki Kuu (BoT) Profesa Benno Ndulu, alipoulizwa kuhusu sakata hilo alisema yuko nje ya nchi kikazi.

"Niko Sweden kikazi, halafu hapa siwezi kukusikia vizuri wala kuzungumza vema kwani kuna shughuli ambayo nimehudhuria," alisema Profesa Ndulu, ambaye taasisi kuu ya fedha ya nchi ina wajibu wa kusimamia benki na taasisi zote za fedha nchini.

Baadhi ya maofisa wa benki hizo ambazo majina yake tunayahifadhi, wamethibitisha kukumbwa na uhalifu huo mkubwa na kwamba wameacha suala hilo mikononi mwa vyombo vya dola.

"Ni kweli kuna vitenfo vya kughushi vimetokea katika benki yetu, lakini hilo hatuwezi kulizungumzia kwa kina kwasababu liko mikononi mwa vyombo vya dola. Polisi wanaweza kulizungumzia hilo," alifafanua ofisa kutoka moja ya benki iliyoibiwa kiasi kikubwa cha fedha karibu Sh100 bilioni.

Wakati DCI Kamishna Manumba, Gavana Ndulu na maofisa wa benki wakizungumzia hayo, uchunguzi wa Mwananchi umebaini kwamba, fedha hizo ziliibwa mwishoni mwa mwaka jana na mwanzoni kabisa mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, hadi sasa taarifa za awali zinaonyesha mpango huo mchafu umeanzia ndani ya benki kwa kuhusisha baadhi ya watu ambao ni wanamtandao na wezi wenzao nje ya nchi.

Mwananchi imebaini kwamba, hadi sasa Idara ya Interpol Tanzania kwa kushirikiana na wenzao wa nje wanafanya uchunguzi huo wa kina katika nchi za Hong Kong, Uingereza na Marekani ambako taarifa za awali zinaonyesha fedha hizo zilikwenda.

Katika uchunguzi huo, Mwananchi imebaini kwamba baada ya mpango huo kufanywa nchini fedha hizo zinaonyesha zilihamishwa kwa njia hiyo ya kughushi kwenda nchi hizo.

Vyanzo hivyo vya habari za kiuchunguzi, zilifafanua kwamba baadhi ya watu katika mabenki hayo ambao wanafahamu mzunguko wa fedha ikiwemo malipo ya ndani na nje, wamepanga njama hizo na kughushi malipo kwa kushirikiana na mtandao mkubwa wa wezi wenzao wa nje ya mabenki ndani na nje.

Habari hizo za kiuchunguzi, zinaonyesha kwamba wizi huo umetikisa mabenki hayo kiuchumi huku duru za kiusalama zikisema vyombo vya usalama vimekuwa makini kuangalia fedha hizo zimeingia mikononi mwa watu gani.

Mwananchi imebaini kwamba, kiasi hicho kikubwa cha fedha kinaweza kuweka usalama wa taifa hatarini endapo kitakuwa kimeingia kwenye mikono ya watu ambao wana nia mbaya na nchi.

"Ni kiasi kikubwa cha fedha, kama kitakuwa kimeingia kwenye mikono ya watu hatari wanaweza kuhatarisha usalama wa nchi, bilioni 300 si kitu kidogo," kilisema chanzo kimoja kutoka moja ya vyombo vya usalama.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, kitisho kingine kinachoangaliwa hadi sasa ni iwapo fedha hizo zimeibwa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba kwa ajili ya kundi fulani ikiwemo mafisadi kutaka kuzitumia kutimiza malengo yao.

"Tunaangalia pia, maana inawezekana ni mafisadi wakubwa ambao wanajua mzunguko wa fedha ndiyo wamekula njama na kutaka kuhujumu nchi kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu," kilifafanua chanzo hicho.

Ingawa haijathibitika, lakini kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kuliibuka ufisadi mkubwa katika BoT ambao zaidi ya Sh 133 bilioni ziliibwa.
 
Mambo ya uchaguzi. Why mihela kibawa inaibiwa uchaguzi ukikaribia? Tisuburi mapilau, laki 5, fulana, kofia na kanga bin vitenge. Kaazi Kwer Kwer Kwer
 
WAKATI habari za wizi wa kimafia wa Sh300 bilioni zikiwa zimeistua serikali, watu kumi wamekamatwa kwa tuhuma za wizi mwingine wa aina hiyo uliohusisha Sh360 milioni za benki moja nchini.

Kukamatwa kwa watu hao kumetokea siku moja baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti wizi huo mkubwa unaotumia teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta ambao ulifanyika kwenye benki nne kubwa nchini, taarifa iliyofanya Mamlaka ya Mapato (TRA) kuanza uchunguzi.

Mbali na taarifa za kukamatwa kwa watu hao, vyombo vya habari pia vimeripoti kukamatwa kwa mfanyabiashara mmoja aliyekuwa akifanya jaribio la kuiba kimafia Sh221 milioni kutoka benki ya NBC.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ambazo zilithibitishwa na msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Abdallah Msika zinasema watu hao walikamatwa kati ya Februari na Machi, katika msako wa jeshi hilo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Shinyanga na Zanzibar.

Kukamatwa kwa watu hao kumetokea wakati benki zimekuwa zikihaha kubadili na kuboresha mifumo yake ya kuchukua na kutoa fedha kwa njia ya elektroniki kwa lengo la kukabiliana na uhalifu uliokithiri unaofanywa na watu walio ndani na nje ya nchi.

Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao, Mssika alisema watano kati yao ni wafanyakazi wa benki hiyo (jina tunalo kwa sababu za kimaadili) na wengine ni kutoka nje ya benki hiyo na kuongeza: "Hadi sasa uchunguzi bado unaendelea.

"Wote wanatuhumiwa kwa wizi huohuo wa mtandao... baada ya kufanyika uchunguzi walibainika kuwa ni sehemu ya mtandao ambaon inatuhumiwa unahusika kwenye wizi huo."

Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizothibitishwa na Mssika, wizi huo ulifanyika katika kipindi cha kuanzia Januari lakini ulibainika kati ya Februari na ndipo uchunguzi ukaanza.

Msika alifafanua kuwa baada ya kufanyika uchunguzi ilibainika kiasi hicho cha fedha kilihamishwa kutoka tawi moja jijini Dar es Salaam na kupelekwa tawi jingine la mkoani Shinyanga.

Alisema baada ya kuhamishiwa tawi la Shinyanga, fedha hizo zilianza kuingizwa kwenye akaunti mbalimbali za wahusika ndipo baadhi yao waliponaswa.

"Fedha zilitoka tawi la Dar es Salaam na kupelekwa tawi la Shinyanga, baada ya kufika Shinyanga zilianza kuingizwa kwenye akaunti mbalimbali za watuhumiwa... tayari hao kumi wamekamatwa kuhusika na tukio hilo," alifafanua msemaji huyo wa polisi.

Kuhusu kiasi cha fedha, alisema hadi sasa zimepatikana Sh319.5 milioni kati ya Sh360 milioni zilizoibwa na kwamba juhudi za kusaka nyingine na watuhumiwa zinaendelea.

Mssika aliongeza kwamba baada ya watuhumiwa wengine kukamatwa, watajumuishwa katika kesi inayowakabili watu hao kumi walio mikononi mwa polisi.

Katika hatua nyingine, Mssika alisema Jeshi la Polisi limetaka benki yoyote ambayo imekumbwa na tuhuma za wizi huo wa mtandao ziwasilishe taarifa zao polisi.

Mssika, ambaye alilirudia kauli ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba kuhusu taarifa za wizi mkubwa katika mabenki matatu, alisema hadi sasa hawajapata taarifa hizo kuhusu kiwango kilichoibwa na benki husika.

Wizi wa mtandao umekuwa ukikua kwa kasi nchini kutokana na matukio yaliyozikumba benki na tayari kuna kesi mbalimbali zinazohusisha wafanyabiashara wa Morogoro, walioba zaidi ya Sh1 bilioni katika moja ya benki nchini.

Lakini vyombo vya usalama ikiwemo polisi na mamlaka za serikali zimekuwa zikijaribu kufunika uhalifu huo.

Juzi wataalamu wa kubaini uhalifu wa kughushi kutoka Afrika Kusini walikuwa jijini Dar es Salaam kuangalia wizi mkubwa katika moja ya benki kati ya tatu zilizokumbwa na wizi huo wa kimafia wa Sh300 bilioni.

Benki hiyo ambayo inatajwa kuwa iliibiwa kiasi hicho kikubwa cha fedha, kwa sasa imeanza kurekebisha mfumo wake wa usalama wa fedha, hali ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa kwa wateja wake kwa takriban wiki nne sasa.

Tayari maafisa wadogo wanne wa benki hiyo wameshaondolewa katika nafasi zao kwa ajili ya kupisha uchunguzi zaidi kubaini uhalifu huo na mtandao wake.

Uchunguzi wa wizi huo unahusisha pia maafisa waandamizi ambao wanatuhumiwa kuwa wanaweza kushirikiana na mtandao wa wahalifu wa kughushi kufanikisha wizi huo wa kimafia.

Mwaka 2005/2006 Benki Kuu (BoT) iliibiwa zaidi ya Sh133 bilioni katika akaunti moja ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) baada ya watu kughushi nyaraka zilizoonyesha kuwa walirithishwa madeni na makampuni ya nne na hivyo kujivunia mabilioni ya fedha.

Hadi sasa, wafanyabiashara kadhaa pamoja na wafanyakazi wa BoT wameshafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kula njama na kuiba fedha hizo,

Hata hivyo, baadhi ya walioiba hawakufikishwa mahakamani baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa msamaha kwa wale ambao wangezirudisha kabla ya Novemba mosi mwaka 2008.
Mbali na waliorejesha kiasi cha Sh70 bilioni, waliokwapua kiasi cha Sh40 bilioni pia hawajafikishwa mahakamani kutokana na wizi huo kuhusisha makampuni mengine yaliyo nje ya nchi na hivyo uchunguzi kuhitaji nguvu kubwa zaidi kuweza kuwabaini wahusika.

SOURCE: MWANANCHI
 
ukweli wa mambo mi siami kama ni wezi tu hizo pesa zitakuwa zauchaguzi,why kila uchaguzi ukikaribia pesa nyingi sana zinapotea,kwa mtindo huu hii nchi kuendelea itakuwa ndoto
 
ukweli wa mambo mi siami kama ni wezi tu hizo pesa zitakuwa zauchaguzi,why kila uchaguzi ukikaribia pesa nyingi sana zinapotea,kwa mtindo huu hii nchi kuendelea itakuwa ndoto
Mi SIJASEMA MWENZIO 😕
 
wakati habari za wizi wa kimafia wa sh300 bilioni zikiwa zimeistua serikali, watu kumi wamekamatwa kwa tuhuma za wizi mwingine wa aina hiyo uliohusisha sh360 milioni za benki moja nchini.

Kukamatwa kwa watu hao kumetokea siku moja baada ya gazeti la mwananchi kuripoti wizi huo mkubwa unaotumia teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta ambao ulifanyika kwenye benki nne kubwa nchini, taarifa iliyofanya mamlaka ya mapato (tra) kuanza uchunguzi.

Mbali na taarifa za kukamatwa kwa watu hao, vyombo vya habari pia vimeripoti kukamatwa kwa mfanyabiashara mmoja aliyekuwa akifanya jaribio la kuiba kimafia sh221 milioni kutoka benki ya nbc.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali vya habari ambazo zilithibitishwa na msemaji wa jeshi la polisi, kamishna msaidizi abdallah msika zinasema watu hao walikamatwa kati ya februari na machi, katika msako wa jeshi hilo kwenye mikoa ya dar es salaam, shinyanga na zanzibar.

Kukamatwa kwa watu hao kumetokea wakati benki zimekuwa zikihaha kubadili na kuboresha mifumo yake ya kuchukua na kutoa fedha kwa njia ya elektroniki kwa lengo la kukabiliana na uhalifu uliokithiri unaofanywa na watu walio ndani na nje ya nchi.

Akithibitisha kukamatwa kwa watu hao, mssika alisema watano kati yao ni wafanyakazi wa benki hiyo (jina tunalo kwa sababu za kimaadili) na wengine ni kutoka nje ya benki hiyo na kuongeza: "hadi sasa uchunguzi bado unaendelea.

"wote wanatuhumiwa kwa wizi huohuo wa mtandao... Baada ya kufanyika uchunguzi walibainika kuwa ni sehemu ya mtandao ambaon inatuhumiwa unahusika kwenye wizi huo."

kwa mujibu wa taarifa hizo zilizothibitishwa na mssika, wizi huo ulifanyika katika kipindi cha kuanzia januari lakini ulibainika kati ya februari na ndipo uchunguzi ukaanza.

Msika alifafanua kuwa baada ya kufanyika uchunguzi ilibainika kiasi hicho cha fedha kilihamishwa kutoka tawi moja jijini dar es salaam na kupelekwa tawi jingine la mkoani shinyanga.

Alisema baada ya kuhamishiwa tawi la shinyanga, fedha hizo zilianza kuingizwa kwenye akaunti mbalimbali za wahusika ndipo baadhi yao waliponaswa.

"fedha zilitoka tawi la dar es salaam na kupelekwa tawi la shinyanga, baada ya kufika shinyanga zilianza kuingizwa kwenye akaunti mbalimbali za watuhumiwa... Tayari hao kumi wamekamatwa kuhusika na tukio hilo," alifafanua msemaji huyo wa polisi.

Kuhusu kiasi cha fedha, alisema hadi sasa zimepatikana sh319.5 milioni kati ya sh360 milioni zilizoibwa na kwamba juhudi za kusaka nyingine na watuhumiwa zinaendelea.

Mssika aliongeza kwamba baada ya watuhumiwa wengine kukamatwa, watajumuishwa katika kesi inayowakabili watu hao kumi walio mikononi mwa polisi.

Katika hatua nyingine, mssika alisema jeshi la polisi limetaka benki yoyote ambayo imekumbwa na tuhuma za wizi huo wa mtandao ziwasilishe taarifa zao polisi.

Mssika, ambaye alilirudia kauli ya mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai (dci), kamishna robert manumba kuhusu taarifa za wizi mkubwa katika mabenki matatu, alisema hadi sasa hawajapata taarifa hizo kuhusu kiwango kilichoibwa na benki husika.

Wizi wa mtandao umekuwa ukikua kwa kasi nchini kutokana na matukio yaliyozikumba benki na tayari kuna kesi mbalimbali zinazohusisha wafanyabiashara wa morogoro, walioba zaidi ya sh1 bilioni katika moja ya benki nchini.

Lakini vyombo vya usalama ikiwemo polisi na mamlaka za serikali zimekuwa zikijaribu kufunika uhalifu huo.

Juzi wataalamu wa kubaini uhalifu wa kughushi kutoka afrika kusini walikuwa jijini dar es salaam kuangalia wizi mkubwa katika moja ya benki kati ya tatu zilizokumbwa na wizi huo wa kimafia wa sh300 bilioni.

Benki hiyo ambayo inatajwa kuwa iliibiwa kiasi hicho kikubwa cha fedha, kwa sasa imeanza kurekebisha mfumo wake wa usalama wa fedha, hali ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu mkubwa kwa wateja wake kwa takriban wiki nne sasa.

Tayari maafisa wadogo wanne wa benki hiyo wameshaondolewa katika nafasi zao kwa ajili ya kupisha uchunguzi zaidi kubaini uhalifu huo na mtandao wake.

Uchunguzi wa wizi huo unahusisha pia maafisa waandamizi ambao wanatuhumiwa kuwa wanaweza kushirikiana na mtandao wa wahalifu wa kughushi kufanikisha wizi huo wa kimafia.

Mwaka 2005/2006 benki kuu (bot) iliibiwa zaidi ya sh133 bilioni katika akaunti moja ya malipo ya madeni ya nje (epa) baada ya watu kughushi nyaraka zilizoonyesha kuwa walirithishwa madeni na makampuni ya nne na hivyo kujivunia mabilioni ya fedha.

Hadi sasa, wafanyabiashara kadhaa pamoja na wafanyakazi wa bot wameshafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kula njama na kuiba fedha hizo,

hata hivyo, baadhi ya walioiba hawakufikishwa mahakamani baada ya rais jakaya kikwete kutoa msamaha kwa wale ambao wangezirudisha kabla ya novemba mosi mwaka 2008.
Mbali na waliorejesha kiasi cha sh70 bilioni, waliokwapua kiasi cha sh40 bilioni pia hawajafikishwa mahakamani kutokana na wizi huo kuhusisha makampuni mengine yaliyo nje ya nchi na hivyo uchunguzi kuhitaji nguvu kubwa zaidi kuweza kuwabaini wahusika.

Source: Mwananchi

tanzania imekuwa mapango ya majizi ,
uchumi wa hii nchi utaporomoka sana mpaka kufikia kipindi kifupi kijacho itakuwa nchi masiki kuliko zote duniani!
Majizi yatazidi kununua magari ya kifahari foleni zitazidi mikocheni nk.
Majizi yatazidi kununua magorofa masaki,mbezi,mikocheni nk
mwisho kutakuwa hakuna amani ktk nchi hii maana kutakuwa na matabaka ya matajiri mijizi na masikini mijizi !
 
Kwa kweli huwa inanishangaza baadhi ya vijana umri wa kati (35-50) huwa nawaona kila siku wana magari na nyumba nzuri pamoja na vitega uchumi vya ghafla ghafla ila kila ukitaka kuchunguza upate shughuli yake halali huioni!!!! Yaani utasikia nafanyia shughuli zangu mjini, na kweli kila siku anaenda mjini. Sasa ukitaka kuulizia ofisi ndiyo kabisa "dumb". Tatizo kubwa ni kwamba usalama wa taifa umelala fofo fofo, naweza kusema wamedundwa nusu kaputi wanasubiri operation!!!!

Nchi za wenzetu huwa kila nyendo ya binadamu inafuatiliwa!!!! Hapa kwetu population yetu ni kubwa kuliko wao na tunashindwa kuwafuatilia watu wachache au tuseme wanaopewa mamlaka ya kufuatilia basi engine zonapoozwa njiani??? Mwenye feza Tanzania ni rafiki wa vyombo vya dola na mamlaka, hakamatiki!!! Hukuona hata wale wa EPA kiongozi wa heshima alisema "watu hawa ni hatari sana, wana hela si rahisi kupambana nao". Sasa kama wewe chief unasema hivyo, je wale walio chini ya himaya yako watasemaje?? Tuwe serious!!
 
Back
Top Bottom