Bilioni 650 za DP World Zamkuna Makala. Zaongeza Ufanisi wa Bandari ya Dar kutoka Makasha 7,000 Hadi Makasha 20,000

Bilioni 650 za DP World Zamkuna Makala. Zaongeza Ufanisi wa Bandari ya Dar kutoka Makasha 7,000 Hadi Makasha 20,000

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
My Take
Wale wa Samia ameuza Mali zao za Urithi mnaitwa kuja kumwaga povu jingine.

Kwa taarifa yenu sio tuu shehena ya mzigo imeongezeka Bali muda wa kusubiria meli umetoka siku 14 Hadi siku 3.

Hongera sana Rais Samia Kwa Mageuzi haya yenye Tija Kwa Nchi na kuleta ushindani mzuri wa Bandari ya Dar.

Pia soma hapa DP World kuokoa Sh1.6 trilioni hadi Desemba



View: https://youtu.be/o3wT4BwqifA?si=TXvSwhowSbEj_FlY

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) imesema uwekezaji uliofanywa na Kampuni ya DP World katika bandari ya Dar es Salaam katika kipindi cha miezi mitatu umeonesha mafanikioa makubwa kwa shehena ya makasha kuongezeka kutoka 7,151 Aprili 2024 hadi kufikia 20,151 kufikia Julai 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Uwekezaji huo wenye thamani ya takriban dola milioni 250 (Sh bilioni 675) kwa ajili ya uendeshaji wa magati 0-7 bandarini hapo umeleta manufaa makubwa kwa ni ongezeko la shehena ya makasha hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 182.

Hayo yamebainishwa jana jijini Dar es Salaam na Meneja wa Shughuli na Uratibu wa TPA, Josephat Lukindo wakati akiwasilisha ripoti fupi ya utendaji wa bandari hiyo baada ya uwekezaji huo kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makala aliyefanya ziara yake badarini hapo.

Alisema pesa hizo imetumika kuboresha utendaji wa bandari hiyo katika maeneo matatu baada ya kukabidhiwa na mamlaka ya bandari Aprili 15, 2024.

“Kwa uzoefu tulionao katika uendeshaji wa bandari, tuliamua kuanza na uboreshaji wa maeneo matatu muhimu ili kuongeza ufanisi zaidi,” alisema Lukindo.

Amesema sehemu ya kwanza kabla ya kufanya kitu chochote kampuni ya DP World kupitia kampuni tanzu ya DP World Dar es Salaam iliyoanzishwa kusimamia bandari hiyo ilifanya manunuzi ya mitambo ya kisasa yenye thamani ya takriban bilioni 215.

Alisema pili ilifanya ukarabati wa mitambo mibovu iliyokuwa ikitumika bandarini hapo na kufanya manunuzi ya vifaa vipya yakiwemo matrekta ya kubebea mizigo 20 pamoja na matela 31, jenerela saba zenye ukubwa wa Kv 10,000 kila moja kwa ajili ya kuendeshea mitambo ikitokea umeme umekatika na vifaa vya kubebea mizigo mizito (cranes).

“Tatu, DP World ilifanya usimikaji wa mifumo ya kisasa ya TEHAMA kwa ajili ya uendeshaji wa bandari hiyo. Hapo awali, tulikuta mifumo ambayo imepitwa na wakati na kuamua kuweka mifumo ya kisasa kuendana na maendeleo ya teknolojia,” alisema.

Hivyo, alisema uwekezaji huo umeleta manufaa makubwa ndani ya kipindi cha miezi mitatu iliyochangia ongezeko la shehena ya makasha ikiwa sawa na ongezeko la asilimia 182.

Mwanahalisi
 
20240829_072729.jpg
 
Nani amefanya ubaya ?
Father Kitima na wengine kwenye ngazi ya kanisa letu Katoliki walidhani wanamkomoa Samia kumbe wanapoteza muda na wameishia kujipatia aibu ya mwaka baada ya Adani kupewa aendeshe magati namba 8 mpaka 11.

Yale yale ya Mwabukusi anayelaumu IGA bila ya kuwa na uelewa wowote wa sheria za kimataifa. IGA ipo na makampuni mengine yanaruhusiwa kufanya biashara ya uendeshaji wa bandari zetu.
 
Father Kitima na wengine kwenye ngazi ya kanisa letu Katoliki walidhani wanamkomoa Samia kumbe wanapoteza muda na wameishia kujipatia aibu ya mwaka baada ya Adani kupewa aendeshe magati namba 8 mpaka 11.

Yale yale ya Mwabukusi anayelaumu IGA bila ya kuwa na uelewa wowote wa sheria za kimataifa. IGA ipo na makampuni mengine yanaruhusiwa kufanya biashara ya uendeshaji wa bandari zetu.
Maajabu ya layman kumfundisha sheria mwanasheria!.

Wewe ni layman kwasababu hata ile IGA hukuwahi kuiona, kama ungeiona kwa kuisoma na kuielewa usingeandika hizi pumba zako hapa.
 
Back
Top Bottom