Mkuu Hawa jamaa wako smart sana walifanikiwa kwenye DINI ambapo hofu ya Kitu kisichojulikana ndo imetawala na Sasa wameenda hatua ya mbele zaidi
Hii ndiyo njia itakayoshindwa vibaya kuwahi kutokea, sina shaka na hili. Dini ilikufa kitambo sana kipindi cha akina Karl Max aliposema " religion is an opium of the masses" 1800's inapapatika tu ila tayari.
Dini pamoja na kujificha chini ya ukasimishwaji wa mamlaka ya mtu kwa nguvu kubwa iliyopewa jina Mungu. Watu waliweza mapema sana kuishiku na kuipinga vikali tena katika mwanzo wake mpaka sasa. Jaribio hili lilishashindwa kitambo sana na mamlaka ya mtu ni mtu ndiyo maana leo baadhi ya madhehemu Ulaya ni kumbi za starehe leo. Afrika na Tanzania kwa upekee kutokana na athari za ukoloni imechelewa sana lakini paso na shaka hali inaonesha kabisa kuwa watu wameanza kuona.
Asili inaonesha kuwa mtu ni mtawala "God like" hakuna njia rahisi ya kumtawala mtawala ndiyo maana unaona njia nyingi zinazotumika kwa kiasi kikubwa zinapanda hofu ya kukiondoa kiti cha utawala cha mtu.
We must think critically, nani ni AI, nini nguvu iliyopo nyuma ya teknolojia hiyo, Kuna maslahi gani " vested interest" ya AI katika AI, kama AI itafanya kazi za watu suala la muhimu siyo hofu inayosukumwa kuwa watu watakosa cha kufanya ila ni watu kutawala zaidi. Tatizo ni ukweli kuwa Kuna watu wanasukuma ajenda ya kutawala zaidi kwa kuhakikisha uwezo wa mtu kibinadamu unatwezwa.
Teknolojia imekuja kama zana ya mtu kutawala zaidi mazungira yake na siyo kumtawala mtu mwingine. Suala la mtu kutaka kumtawala mtu mwingine siyo suala la asili ila ni zao la tamaa, uchu na mawanda ya chini ya nishati za kiumbaji.
Hili lipo wazi kwa AI haina nafasi ya kutoa mawazo yake katika chanzo anachotolea mtu mawazo yake pamoja na kuipamba kwa mapambo mbalimbali juu ya uwezo wa teknolojia hiyo. Naungana na hoja kuwa hii ni njia ya kupanda hofu kwa kasi kama zilivyowahi kutumia njia nyingine Ili kulinda maslahi fulani ya kikundi fulani "hegemony protection"
Ni kundi lenye ,lengo uleule wa kutawala utu Duniani linalotumia mwavuli wa teknolojia kuhakikisha akili za wanadamu zinaghilibiwa kiasi cha kuikabidhi madaraka yake ya asili kwenye mifumo ya kiteknolojia.
Tunaona kila dalili ya watu wachache kutumia ukwasi mkubwa walionao katika harakati za makusudi za kuutweza utu kwa kuhakikisha binadamu anaushusha uwezo wake wa asili wa kufikiri kwa kiwango dhalili mno.