Baada ya kuwezesha suala la Elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha Sita na Mikopo ya Elimu ya Juu kwa wanaohitaji. Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inakwenda kuweka rekodi nyingine Barani Afrika.
Wananchi watakaotambuliwa kutokuwa na uwezo wataendelea kupatiwa huduma kwa utaratibu utakaowekwa na Serikali kwa kila mtu kuwa na kadi yake ya bima ya afya.
Suala hili la BIMA ya Afya kwa wote ni matokeo ya ushirikishwaji wa wadau wote. Ni mpango bora unaotekelezwa na serikali ya awamu ya sita ikiwa ni sehemu ya ahadi za Mhe. Rais kumuwezesha kila Mwananchi kupata huduma ya Afya.
Wenye uwezo wa kuchangia (Wasio na familia) watachangia TZS 84,000 kwa Mwaka, sawa na TZS 7000 Kwa Mwezi. Huku kaya ya watu 6 pendekezo likiwa ni TZS 340,000 kwa Mwaka. Mpaka sasa mapendekezo haya yanaonekana kuwa ya chini zaidi Barani Afrika.
Kupitia mfumo wa bima ya afya kwa wote, mfumo wa rufaa wa matibabu utatumika, ambapo wananchi watapata matibabu kuanzia ngazi ya zahanati hadi Taifa itakapohitajika bila shida au adha ya aina yoyote.
Rais Samia Suluhu anahakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za afya zenye gharama nafuu.