Bima ya Afya kwa wote Tanzania is impossible

Hayo ni mawazo yako ya duni


Point ya msingi ungesema ni watz wangapi watalipa hiyo 84k ili wapate bima ya NHIF !?

Mimi nachojua Serikali jinsi inavyo wakomodate wanafunzi wa shule za Serikali ndo itafanya katika bima Huduma zitakuepo lakini in poor quality condition
 
Lengo la hiyo Bima kwa wote ni kuiongezea NHIF wachangiaji wapya ili isife.

Nyie mtachanga halafu huduma nyingi bado mtaendelea kujilipia tu.

Haohao viongozi walioshindwa huku NHIF ikiwa na wanachama wachache,watafanya maajabu gani unafikiri?

NB: NHIF iko hoi kiuchumi kwa sasa.
 
Uko sahihi kabisa
 
Ngoja tuone... Mambo ya kuelekea kwenye uchaguzi mkuu...
 
Hizi point zako za mwisho ni kichekesho. Kwa hiyo ugonjwa mdogo haustahili kutibiwa hospital? Maskini kuugua kila siku hayo ni makisio yako tu ama chuki kwao lakini pia kama wanalipia bima nini ubaya wakitibiwa, si ndio kiini hasa cha bima? Kwani unakata bima ili usiugue? Acheni wivu, bima ni kwa wote maskini ama tajiri
 
Malengo ya Serikali ya Tanzania katika suala la bima ya afya kwa wote sio Huduma! Ila wanaforce wapate hela za kusimamisha tena NHIF ili wawe wanajikopesha vizur na kula vizur hela za wananchi, kuhusu huduma ya afya tutajua wenyewe
Walichukua hela za mifuko yote ya huduma za kijamii kuanzia hifadhi ya jamii, NSSF, NHC, LAPF, NHIF, PPF, nk kwenda kuendeshea serikali hadi mifuko ikafa. Hata taasisi kama muhimbili ililazimishwa kwa nguvu watoe gawio kwa serikali wakati wagonjwa hawana hata shuka za kujifunika Wala dawa.

Mtu ana wake 2 na watoto 9 bima gani ya afya itaruhusu kuhudumia wake 2 na watoto 9? Je, watumishi wa afya wa kuhudumia wagonjwa wapo? Posho zao zipo? Idadi Yao inatosha?

Mtu Hana chakula Cha kula Leo unategemea atalipa hela ya kutibiwa kama siku ataumwa?
 
Kutumia vitu kama kupata leseni, line ya simu au passport lazima uwe na bima ya afya haitakuwa effective kwakuwa bima ya afya inalipiwa kila mwezi au kila mwaka wakati leseni ya udereva ni kila baada ya miaka 5, Ina maana utakuwa na wanachama wengi lakini ambao hawalipi michango Yao kwenye bima.

Dawa pekee ya serikali kuwasaidia wananchi wake kupata maisha mazuri ni kwa
1. Kuboresha kilimo, ufungaji na uvuvi
2. Kuwa na mashamba makubwa ya mazao na mifugo ambako watu wengi wataajiliwa.
3. Kuboresha kazi za wamachinga zitoe faida.
4. Kutafuta masoko ya uhakika mazao, mifugo, samaki na bidhaa nyingine
5. Kupunguza riba kwenye mabenki
6. Kuwa na Kodi zinazolipika
7. Kufundisha elimu ya bima ya afya mashuleni kuanzia elimu ya msingi ili ufahamu wa watu ubadilishe culture yao ya kuoa, kuzaa na kujiunga na bima.

Tusijidanganye sisi wenyewe, bima kwa wote ni mfupa mgumu sana kuutafuna.
 
Hivyo unatoa maoni gani?

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Unamwambia mama yako anaeumwa kijijini kuwa nenda hospitali katibiwe SI una bima wewe? Pale kwenye zahanati anakuta foleni ndeeefu ya wagonjwa, hakuna watumishi wa kutosha na hakuna dawa. Anashinda hapo kutwa nzima na kuishia kuandikiwa cheti akanunue dawa maduka binafsi, na wagonjwa wengine wanafia kwenye foleni akisubiri zamu yake ifike. Mhudumu mwenyewe Yuko peke yake na ana madai kibao hajalipwa.
 
Majibu ya mkurugenzi ylinikatisha tamaa alipoulizwa atawezaje kutoa vitambulisho vya bima kwa watanzania wapatao mil 70, ikiwa NIDA kutoa vitambulisho mil 10 tu walishindwa mwaka wa 8 huu.

Naamini ummy Mwalimu atafanya jambo kabla serikali yetu haijapata lawama
 
Sijui sisi wa Tz tunakwama wapi!? Hivi sasa nipo Oman na nimetembelea supermarket maarufu kama Lulu, Carrefour etc. Unakuta matunda kama Avocado kutoka Kenya na Uganda na wanauza kilo si chini ya Tzs 8,000/=, za Tz hazionekani. Huu ni mfano tuu, ili wananchi waweze kujikwamua kimaisha, na waweze kumudu kitu kama “Bima ya afya” lazima serikali kupitia wizara ya biashara iangalie mambo kama haya kwa karibu. Lazima kuwepo na Economic Intelligence. Mnapigwa bao na Kenya na Uganda.
 
Ngoja tuone huenda tukafaulu.
 
Bima ya afya kwa wote lazima iwepo, nyie wakosoaji na wajinga wachache hamuwezi kukwamisha, mnataka watu waendelee kufa kwa marelia kwa kukosa fedha za matibabu
Juzi nilimpeleka mgonjwa KCMC saa 4 usiku. Hana bima ya afya, hivyo ikabidi kulipia gharama. Hadi saa 7 usiku alikuwa ameshafanyiwa vipimo karibu vyote.

Kuna bwana mmoja alimfikisha mgonjwa wake toka saa 11 jioni. Huyu mgonjwa Ana bima ya afya. Hadi saa 7 usiku alikuwa hajapata huduma kutokana na tatizo la mtandao.

Sasa hivi wenye bima ya afya ni wachache; lakini wanachelewa kupata huduma kutokana na kutoaminika kwa mtandao! Je, kama Watanzania wote wakiwa na bima za afya hali itakuwaje?!
 
wakinilazimisha bima ya afya nitakuwa naenda hospital check kila wiki hospital tofauti mpaka bima yangu iishe
 
Jiongeze ndugu. Kinachotafutwa sio ubora wa afya ya mchangiaji bali hela ya mchangiaji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…