Bima ya Afya kwa wote Tanzania is impossible

Kwa lugha rahisi itakuwa KIZUNGUMKUTI!
 
halafu hiyo ipo Sana, vipi anaendeleaje mgonjwa mkuu, poleni sana
 
Ondoa negative energy yako katika maendeleo ya nchi yetu walahi [emoji2959]
Nafumba mdomo wako na chochote utakacho nena au kuwaza kisitokee kabisa shindwa na ulegee walahi!
Penda kujifunza kutokana na makosa ya wengine sio kwa makosa yako. Fanya home work yako vizuri. Walahi lengo kuu hapa sio afya ya watanzania bali hela ya watanzania. Mazingira na miundombinu ya kutoa bima ya afya kwa wote hatuna na hatunayo Leo Wala kesho. Binadamu anahitaji kwanza hewa, maji na chakula kabla ya kuhitaji matibabu (safety, free from pain). Hivyo, Kama hewa safi, maji safi na chakula safi kwa wote hakuna haitawezekana kabisa kwa bima kwa wote. Hii haihitaji rocket science.
 
Kuweka kumbukumbu kwenye computer Nako kunahitaji internet ya uhakika, umeme wa uhakika kila Kijiji na wataam wa uhakika kila zahanati na hospital, tunavyo? Hadi Leo Kuna maeneo hata mawasiliano kwa simu za mkononi hazifiki
 
Malengo ya Serikali ya Tanzania katika suala la bima ya afya kwa wote sio Huduma! Ila wanaforce wapate hela za kusimamisha tena NHIF ili wawe wanajikopesha vizur na kula vizur hela za wananchi, kuhusu huduma ya afya tutajua wenyewe

Kuna watu watakua wanapata commission kutoka kwa makampuni ya Bima. Viongozi wetu hawajawahi kukazia kitu kisicho na maslahi kwao.
 
Kaka na maskini huwa wanaugua kila siku ya Mungu. Mara utasikia mtoto kaungua na uji, mara mtoto kameza hela, mara kapigana na mwenzake, mara oh kaumwa na mbwa, kasukumwa na ng'ombe, ameumwa na nyoka, ana minyoo, ana mimba. Maskini ni mtu ambae halali kwenye chandarua, hanawi mikono, haogi, hafui hali matunda mara kwa mara ndio maana kipindupindu ni kawaida kutoka kwenye mitaa ya watu maskini zaidi kuliko huko masaki, mikocheni, oyster bay, mbezi beach, nk. Hii inamaana kuwa watachangia kidogo sana lakini watatibiwa sana. Wafanyakazi wa afya, vifaatiba, wodi, na maslahi ya watumishi tunavyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…