Bima ya Afya kwa wote Tanzania is impossible

Bima ya Afya kwa wote Tanzania is impossible

Juzi nilimpeleka mgonjwa KCMC saa 4 usiku. Hana bima ya afya, hivyo ikabidi kulipia gharama. Hadi saa 7 usiku alikuwa ameshafanyiwa vipimo karibu vyote.

Kuna bwana mmoja alimfikisha mgonjwa wake toka saa 11 jioni. Huyu mgonjwa Ana bima ya afya. Hadi saa 7 usiku alikuwa hajapata huduma kutokana na tatizo la mtandao.

Sasa hivi wenye bima ya afya ni wachache; lakini wanachelewa kupata huduma kutokana na kutoaminika kwa mtandao! Je, kama Watanzania wote wakiwa na bima za afya hali itakuwaje?!
Kwa lugha rahisi itakuwa KIZUNGUMKUTI!
 
Juzi nilimpeleka mgonjwa KCMC saa 4 usiku. Hana bima ya afya, hivyo ikabidi kulipia gharama. Hadi saa 7 usiku alikuwa ameshafanyiwa vipimo karibu vyote.

Kuna bwana mmoja alimfikisha mgonjwa wake toka saa 11 jioni. Huyu mgonjwa Ana bima ya afya. Hadi saa 7 usiku alikuwa hajapata huduma kutokana na tatizo la mtandao.

Sasa hivi wenye bima ya afya ni wachache; lakini wanachelewa kupata huduma kutokana na kutoaminika kwa mtandao! Je, kama Watanzania wote wakiwa na bima za afya hali itakuwaje?!
halafu hiyo ipo Sana, vipi anaendeleaje mgonjwa mkuu, poleni sana
 
Ondoa negative energy yako katika maendeleo ya nchi yetu walahi [emoji2959]
Nafumba mdomo wako na chochote utakacho nena au kuwaza kisitokee kabisa shindwa na ulegee walahi!
Penda kujifunza kutokana na makosa ya wengine sio kwa makosa yako. Fanya home work yako vizuri. Walahi lengo kuu hapa sio afya ya watanzania bali hela ya watanzania. Mazingira na miundombinu ya kutoa bima ya afya kwa wote hatuna na hatunayo Leo Wala kesho. Binadamu anahitaji kwanza hewa, maji na chakula kabla ya kuhitaji matibabu (safety, free from pain). Hivyo, Kama hewa safi, maji safi na chakula safi kwa wote hakuna haitawezekana kabisa kwa bima kwa wote. Hii haihitaji rocket science.
 
Kavulata! Naungana na wewe!

Kama maswali ya muhimu Kwa jamii kama maji, Shule Hospitali zilizopo zenyewe dawa unaandikiwa hadi upate kitumia siku zinaenda! Hii ni kitendawili kulifanikisha.

Na isitoshe bado hatuna uke utaalamu wa kuweka kumbukumbu kimtandao.

Hii tabia ya kuweka kumbukumbu kwenye makaratasi zaidi nayo shida. Hiki ni kipindi Hospitali zote nchini ziwe na uwekaji kumbukumbu kwenye computer.

Mpangilio wa kuwaona wagonjwa nao uboreshwe sio wanakusanyika Hospitali kutwa mzima.

MaDr. Naonwaelewe kazi zao kwani nao ni tatizo.
Kuweka kumbukumbu kwenye computer Nako kunahitaji internet ya uhakika, umeme wa uhakika kila Kijiji na wataam wa uhakika kila zahanati na hospital, tunavyo? Hadi Leo Kuna maeneo hata mawasiliano kwa simu za mkononi hazifiki
 
Malengo ya Serikali ya Tanzania katika suala la bima ya afya kwa wote sio Huduma! Ila wanaforce wapate hela za kusimamisha tena NHIF ili wawe wanajikopesha vizur na kula vizur hela za wananchi, kuhusu huduma ya afya tutajua wenyewe

Kuna watu watakua wanapata commission kutoka kwa makampuni ya Bima. Viongozi wetu hawajawahi kukazia kitu kisicho na maslahi kwao.
 
Hili haliwezekani. Na ndicho anachokiongelea mleta mada.

Ongezeko la pesa linaenda sambamba na ongezeko la wanufaika. Kama wameshindwa kutoa huduma bora za bima ya afya kwa wachangiaji wachache wenye uhakika wa vipato (watumishi wa umma), hawataweza kabisa endapo maskini wakianza kuchangia
Kaka na maskini huwa wanaugua kila siku ya Mungu. Mara utasikia mtoto kaungua na uji, mara mtoto kameza hela, mara kapigana na mwenzake, mara oh kaumwa na mbwa, kasukumwa na ng'ombe, ameumwa na nyoka, ana minyoo, ana mimba. Maskini ni mtu ambae halali kwenye chandarua, hanawi mikono, haogi, hafui hali matunda mara kwa mara ndio maana kipindupindu ni kawaida kutoka kwenye mitaa ya watu maskini zaidi kuliko huko masaki, mikocheni, oyster bay, mbezi beach, nk. Hii inamaana kuwa watachangia kidogo sana lakini watatibiwa sana. Wafanyakazi wa afya, vifaatiba, wodi, na maslahi ya watumishi tunavyo?
 
Back
Top Bottom