Bima ya Afya, mnachokifanya mnajua madhara yake?

Asante sana kwa hoja nzuri.
Heri yake anaongea kukosa
"Huduma za kibingwa".

Mioyo yetu ina mengi.
 
DENAMWE ahsante sana jwa taarifa muhimu kwa wastaafu. Wengi hatuna habari ya UHAKIKI wa kadi za bima za afya kwa wastaafu. UBARIKIWE SANA.

Ushauri wako uzingatiwe. Kijana wa leo ni mzee wa kesho. NHIF wekeni utaratibu mzuri wa bima ya afya kwa wastaafu ili nanyi mkifika uzeeni mfaidike na mipango mizuri mliyoisisi.
 
Ishu serious kama hii kuna litanzania linaandika ujumbe wa kukejeli ama kweli kuna wachawi wako wazi sana. Poleni sana sana Mungu awasimamie.
 
Nakushukuru sana Alibaaliyo.
Tuendelee kusaidiana.
 
Ishu serious kama hii kuna litanzania linaandika ujumbe wa kukejeli ama kweli kuna wachawi wako wazi sana. Poleni sana sana Mungu awasimamie.
Ni ajabu sana.
Huenda anafaidika kwa adha tunazozipata.
 
Huu mwandiko sio wa mzee
 
Uhakiki
Uhakiki sio suala gani hapa nchini Taasisi nyingi zimekuwa zikifanya uhakiki katika maeneo yake hivyo kama hauna tatizo kwa nini uje kulalamika hapa?
 
Ukipoteza kadi kuna utaratibu wake mfano unapopoteza kadi ya banki mbona hauji hapa kulalamika ebu tuacheni njia za mkato tufuateni utaratibu uliowekwa, NHIF ni taasisi kama ilivyo nyingine
 
Uhakiki ni watu ni mchakato wa kawaida sana msipende shortcut
 
Hata mfuko wao unapumulia mashine sababu ya ufisadi wakifanya ivyo wakahakiki wote itakula kwao. Tatizo limeanzia mbali.
Tuache kuibua mambo ambayo hayapo, uhakiki ni utaratibu tu katika huduma nyingi
 
Asante kwa maoni yako. Uhakiki wa wanachama ni suala la msingi na hufanyika mara kwa mara katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. NHIF inaendelea na uhakiki wa wanachama wake na ili taarifa ifike kwa walengwa ujumbe maalum wa wito unatumwa kwa mhusika. Dhumuni ni kuhuisha taarifa za uanachama na endapo kuna changamoto yoyote mwanachama asisite kuwasiliana na Mfuko kupitia namba ya bure ya huduma kwa wateja 199.
 
Mbona kwenye ujumbe wa NHIF wanasema ofisi ya
Nashindwa kuelewa mbona tangazo la ujumbe mfupi linasema ofisi iliyo karibu na wewe unasema makao makuu ya mkoa?
NHIF wana ofisi hadi ngazi mkoa. In that context ukiambiwa ofisi iliyo karibu nawe maana yake nini? Jumbe za kitapeli zinazoficha ukweli wa jambo kuwatapeli wajinga; ujumbe na zoezi lenyewe ni siasa halafu tunaona sawa. Kama unadhani wanajali pole!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…