Bima ya Afya, mnachokifanya mnajua madhara yake?

Kuhuisha taarifa! Maana ya matumizi ya mifumo ya kielekroniki ni ipi?
 
Ukipoteza kadi kuna utaratibu wake mfano unapopoteza kadi ya banki mbona hauji hapa kulalamika ebu tuacheni njia za mkato tufuateni utaratibu uliowekwa, NHIF ni taasisi kama ilivyo nyingine
Utaratibu wote unafuatwa, kuanzia police loss report, kujaza fomu ya NHIF ya kupoteza kadi, kupata mihuri ya mwajiri, kitambulisho cha Mchangiaji/Mkatwaji cha NIDA unawapa ila sasa Mtegemezi wanaanza kumletea mizengwe wakati ana dharura za kiafya.
 
Ahsante kwa maoni yako. Uhakiki wa wanachama wa mfuko kabla ya kupata huduma za matibabu ni jukumu la kila siku la mfuko lenye lengo la kuhakikisha wanufaika wanaostahili wanapata huduma kwa mujibu wa Sheria. Ujumbe mfupi wa kuhakiki taarifa unaotumwa kupitia simu za mkononi kwa baadhi ya wanachama ikiwemo wastaafu ni sehemu ya utaratibu wa kila siku wa kuwa na taarifa sahihi ili kuwaondolea usumbufu kabla hawajafika katika vituo vya kutolea huduma za matibabu. Kwa wanachama au wastaafu ambao hawawezi kufika kuhakiki taarifa zao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa, Mfuko kupitia waratibu wa NHIF katika kila halmashauri ya wilaya umeweka utaratibu wa kuwafikia na kusaidia kufanya uhakiki kwa urahisi . Aidha, uhakiki unaoendelea hauhusu kundi lote la wanachama wastaafu isipokuwa ni kwa wastaafu wachache ambao taarifa zao zimebainika kuwa na upungufu hivyo kama kuna mstaafu hajapokea ujumbe huo ajue taarifa zake zipo sawa. Vilevile, Mwanachama mwenye kuhitaji msaada anashauriwa kupiga simu ya bure ya kituo cha huduma kwa wateja no 199
 
Ahsante kwa Taarifa Sasa ni vizuri mkaboresha uduma zenu hasa Katika kutuma ujumbe mfupi tumieni lugha Nzuri inayoleta mantiki.
 
Hawawezi kufanya hayo kwa sababu hizo akili hawana wala huo ubunifu hawana.

Huku ni genge la ndugu wa VIONGOZI na watoto wao kupiga pesa.

Ubunifu wao ni kwenye kuiba pesa tuu na kulipana posho.

Pole sana mstaafu, hawana nia njema nawe.
Wizi ni mwingi tu kupitia mtandao wa kielektoniki. Mfano mgonjwa ametibiwa kituo fulani na hajasaini ktk tablet na wala akiweka saini hasomi gharama za matibabu. Pia cha ajabu hata usipOweka saini kwa kusahau kwenda kuchukua kadi ukiifuata kadi na kutaka kuwrka saini unaambiwa mtandao ulishafuta. NASHANGAA KUTIBIWA BURE MAANA WANAOSAHAU KADI NI WENGI BAADA YA KUCHOKA NA MIZUNGUKO YA HISPITALINI. NASHAURI ZIRUDISHENJ ZILE FOMU ZA KAWAIDA ZA KARATASI
 
Ujumbe unaotumwa na NHIF kwa mwanachama mhusika anayehitajika kuhuisha taarifa zake umejitosheleza na unaeleweka kama ifuatavyo

........Ndugu mwanachama mstaafu, tafadhali fika na mwenza wako katika Ofisi ya Mfuko iliyo karibu kwa ajili ya zoezi la uhakiki kabla ya tarehe 30/4/2023. Aidha, fika na namba yako ya NIDA na ya mwenza wako. Kwa ufafanuzi zaidi piga namba 199 bila malipo.

Ujumbe wa tofauti unaosambazwa ni wa upotoshaji na usizingatiwe.
 
Nadhani ufafanuzi wenu NHIF umejitosheleza na umeeleweka,mjadala ufungwe.Kama hujapata ujumbe jua uko salama,kama umepata ujumbe naenda halmashauri.
 
Uhakiki ni jambo la kawaida, wanataka kumuona anayetumia kitambulisho ni yeye na mwenzi wake, NSSF na mashirika mengine nayo huhakiki pia.
 
Uhakiki ni jambo la kawaida, wanataka kumuona anayetumia kitambulisho ni yeye na mwenzi wake, NSSF na mashirika mengine nayo huhakiki pia.
Hakuna hoja ya kupinga uhakiki.
Hoja ni mazingira, namna ya kuhakiki na hali ya unayemhakiki.
Sasa hivi kuna zoezi la uhakiki wa vyeti vya udereva. Fuatilia uone linavyoendeshwa kwa raha.
Halifanyiki mkoani.
Taarifa zinatolewa kwa namna nyingi.
Hata tusiohusika tuna taarifa ya huu uhakiki wa leseni.
Uhakiki ni siri?


Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Asante sana kwa maelezo yako mazuri mno.
Naomba:
1. Nisaidie kumfahamu Mratibu wa NHIF wa Ngara, ilipo Ofisi yake na mawasiliano yake.
2. Hili la wanaohusika na wasiohusika linafahamikaje kwa wasiohusika?
Kumbuka baadhi ya wateja wako hawawezi kuona na kusoma sms hiyo wala kupiga 199..
3. Uhakiki ufanyike, lakini kwa namna bora.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa jibu na maelezo mazuri sana.
Ujumbe huo ni wazi kabisa.
Unaeleweka.
Huu utaonwa/utasomwa na wachache mno.
Saidia uwafikie wadau wako.
Mwagize huyo Mratibu aliyeko Halmashauri awaombe Watendaji wa Kata na vijiji wawafahamishe wastaafu walioko kwenye maeneo yao.
Ukipenda tumia redio za jamii.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Kwanza pole lakini pili nilikua naomba kuuliza...

Je ukistaafu unapewa ela yako yote au unapewa kidogo?

Kama kidogokidogo je ni asilimia ngapi unapewa unapo staafu?
 
Kwanza pole lakini pili nilikua naomba kuuliza...

Je ukistaafu unapewa ela yako yote au unapewa kidogo?

Kama kidogokidogo je ni asilimia ngapi unapewa unapo staafu?
Asante sana.
Maswali haya yanahusianaje na hoja ya uhakiki?
Nadhani maswali haya yanafaa kuulizwa NSSF na PSSSF.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la bima ya afya kunabaadhi ya watu wanawapa ndugu zao wavitumie. Kuna ndugu wanaofanana huwa wanatumia kadi moja.
 
Asanteni sana Bima ya Afya kwa kuweka tangazo hili kwenye tovuti yenu.
Mmefanya jambo jema.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
‘TAARIFA KWA WASTAFU WOTE WA NGARA’

Mbunge wa Jimbo la Ngara Mh Ndaisaba George Ruhoro alipokea malalamiko ya wazee wasitafu ambao Taasisi ya BIMA YA AFYA NCHINI NHIF iliwataka kwenda Bukoba wakiambatana na wenza wao ili kuhakikiwa taarifa zao kabla ya 30.04.2023.

Kama ilovyo ada, Kazi ya Mbunge ni pamoja na utetezi. Mbunge wetu amefanikiwa kutetea kundi hili muhimu sana na sasa baadala ya uhakiki kufanyikia Bukoba sasa utafanyikia Wilayani Ngara kwenye Hospital ya Nyamiaga kuanzia saa tatu asubuhi tarehe 28.04.2023.

Naomba tusambaze taarifa hii kwa wazee wetu popote pale walipo.

Kwa taarifa zaidi, wastafu wanaweza kuwasiliana na Meneja wa NHIF wa Mkoa wa Kagera kupitia simu namba 0754394420.

Wenu katika ujenzi wa jamii yenye ustawi na maendeleo.

Yekonia Baliyendeza
KATIBU WA MBUNGE
JIMBO LA NGARA.
 
Nawashukuru sana Bima ya Afya kwa uamuzi huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…