Bima ya Afya, mnachokifanya mnajua madhara yake?

Na hii ishu ya BIMA ya Afya kuwanyima huduma za Dharura wanaopoteza vitambulisho eti mpaka waje na Vitambulisho vya NIDA ni mbaya sana. Huyu mtu wakati akishughulikia kupata hiyo namba ya NIDA akipata changamoto ya afya afanyeje sasa?.

Zamani mlikubali kuandikisha watu kwa kutumia vitambulisho vya mpiga kura, leo mtu ana dharura ya matibabu baada ta kupoteza kadi yake, kafuata procedure zote including Loss report ya polisi, kujaza fomu zenu upya, mihuri ya mwajiri kila kitu kipo halafu mnasema hamumpi nyaraka za dharura za matibabu mpaka aje na kadi ya NIDA, Huo ni Uchawi kuliko uchawi. Kwenye system zenu mtu mnamuona, ana shida ya dharura ya matibabu hamumpi, lakini kila mwezi bado mnakata hela ya mchangiaji. Huo kama siyo Udhalimu ni nini?

NHIF, acheni bureaucracy, Hudumieni watu, acheni kubadilibadili magoli wakati hela kila mwezi mnachukua.

Mimi au mtegemezi wangu akipata dharura kwa nyie kukataa kumpa matibabu kisa hana namba ya NIDA wakati kipindi najiandikisha mlitoa options kibao , sasa akidhurika nawashitaki!.
Inauma, inakera, inaumiza.
Kuna mengi mioyoni mwetu ila tuendelee kuwaomba wafahamu kuwa afya ni mali na pesa tumezipata kwa jasho.
 
Si ubinafsi rafiki.
Ni kutapatapa.
Nimewaza hivi kwa kuwa tunatakiwa twende mkoani ambako gharama ni kubwa mno.
Hatuimudu.
Heri nusu shari......
Sawa heri nusu shari....

Ila kiukweli Serikali hii inabidi ifanye mabadiliko makubwa kwenye recruitment ya viongozi wa Umma na taasisi zote vinginevyo hakutokuwa na mabadiliko.
 
Mioyo yetu imelemewa mengi.
 
Kuna watu tunatamani hata kupata hyo bima we umeambiwa kuhakiki tuu unaanza kulia lia, unataka wakufate?? Kuna vijana wanahangaika kufanya usaili Dodoma , too complicated , ukijua namna wengine wanavyosota kwenye hii nchi yaani kwa ahueni uliyo nayo kimya kimya ungeenda kuhakikiwa mkoani kwako
Kwakua una afya na nguvu unajona uko salama, siku yakikukuta ndio utajua mtoa mada anamaanisha nini.
 
Lengo ni wastaafu/wanachama wengi wasipate taarifa ya uhakiki kwa wakati mpaka muda wa uhakiki uishe wawasitishie huduma/uanachama.

Halafu wasote miezi kurudishiwa uanachama mfuko walau upumue kidogo.

Mfuko uko taabani huku wenyewe wakikopeshana michango ya wanachama wao hawajui FINCA,BAYPORT etc
 
Mimi ni mstaafu mwandamizi niliyepo wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera.

Nilipata tetesi za kuwapo kwa uhakiki wa wastaafu walio kwenye mfuko wa bima ya Afya tangu mwezi Machi mwaka huu. Kila aliyeniambia nilipomuuliza alikozipata taarifa, naye aliniambia ameambiwa na mwingine.
Hakukuwapo uthibitisho wa chanzo.

Nilihisi kuwa ni jumbe za kitapeli ambazo zinatumwa mara kwa mara. Jana, jamaa yangu akanitumia na kuniuliza iwapo nimepata ujumbe huu:

"NHIF 17.03.2023 SAA 03:11PM NDG. MWANACHAMA MSTAAFU,TAFADHALI FIKA NA MWENZAWAKO KTK. OFISI YA MFUKO ILIYO KARIBU KWA AJILI YA ZOEZI LA UHAKIKI KABLA YA 30.04.2023. AIDHA, FIKA NA NA. YAKO YA NIDA NA NA. MWENZA WAKO. KWA UFAFANUZI _ PIGANA. 199 BILA MALIPO. SENDER HENRY".

Naye alitumiwa na mstaafu mwenzetu. Sikuamini kuwa huo ni ujumbe halali. Mtindo/namna ya uandishi haikuniongoza kuamini kuwa umetumwa na taasisi hii kubwa. Kuna makosa mengi ya kiuandishi na hata ya kimantiki. Hilo tuliache.

Niliingia kwenye tovuti yao. Sikuona tangazo hilo. Niliwasiliana nao kupitia simu hiyo 199. Nilipata ushirikiano mkubwa kwa aliyenipokea. Niliambiwa yafuatayo:

1. Ni kweli uhakiki upo. Unahusisha wastaafu na walioko kazini. Wanataka mstaafu aende na mweza wake.

2. Kila mhusika alishaarifiwa kupitia simu yake na kila mmoja ana tarehe yake. Mimi na wastaafu sita niliowauliza hatuna ujumbe huu.

3. Uhakiki unafanyika makao makuu ya mkoa.

4. Mwisho wa uhakiki ni Mei 30.

Inaelekea bima ya afya hawafahamu kuwa Wastaafu (wateja wao):
i) Ni wazee
ii) Wengi ni wagonjwa
iii) Wengi wana pato duni mno ambalo huenda halitoshi hata gharama ya kwenda mkoani.
iv) Baadhi ni walemavu
v) Kuna ambao hawawezi kusoma jumbe hizo

Yaani wao kwenye simu zao wanafahamu kubonyeza kitufe kimoja tu. Cha kupokelea simu.
Hawa hawawezi kuweka vocha, kukata simu baada ya maongezi, kuongeza salio, kuunga kifurushi nk.
Sembuse kusoma au kuandika ujumbe!

Ushauri:
1. Uhakiki ufanywe jirani na wahusika. Ikiwezekana kwenye Kata. Kuwalazimisha kwenda mkoani kuachwe. Haya ni mateso. Mateso makubwa mno.

Mstaafu aliyepo kijiji cha Muganza wilayani Ngara, mkoa wa Kagera, uhakiki huu utamgharimu siku 5 (kwenda Bukoba na Kurudi). Baadhi ya wastaafu wanahitaji kusindikizwa/kupata wasaidizi. Mbali ya adha za safari, fikiria muda na gharama za safari. Mkifika kwenye kata zao ni vema zaidi.

2. Zoezi hili lifanyike kwa uwazi na kwa haki. Tangazeni kwenye vyombo vya habari. Wekeni kwenye tovuti yenu.
Wasilianeni vema na wateja/wadau wenu. Uduni wa taarifa hizi na hata uandishi wa sms ya wito tunautofautishaje na sms nyingine za kitapeli tunazotumiwa mara kwa mara.

3. Fungueni ofisi wilayani au muweke dawati lenu ama kwa Mkuu wa wilaya au Halmashauri. Mnataka wazee hawa wafe kwa ajali barabarani kwa safari? Mara uhakiki wa PSSSF mkoani na sasa uhakiki huu nao mkoani.
Magonjwa mengine yanatokana adha hizi.

Wazee mnaowasumbua na kuwatesa leo walitumikia nchi hii kwa bidii na uaminifu mkubwa. Msiwalipe mateso kwa kuwajaza majuto na kihoro.

KWA HALI HII, UZEE SI DHAHABU BALI NI ADHABU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Ummy Mwalimu na Naibu wako umemsikia huyu Mzee anavyotoa mapendekezo yake, alafu mda mwingine muwe mnaomba hata ushauri kutoka kwa wananchi basi kuliko kujiamulia tu kisa mnashinda kwenye viyoyozi mda wote, it's not fair
 
Asante sana kwa utetezi wako.
 
Kuna watu tunatamani hata kupata hyo bima we umeambiwa kuhakiki tuu unaanza kulia lia, unataka wakufate?? Kuna vijana wanahangaika kufanya usaili Dodoma , too complicated , ukijua namna wengine wanavyosota kwenye hii nchi yaani kwa ahueni uliyo nayo kimya kimya ungeenda kuhakikiwa mkoani kwako
Vitu vingine Viwapite
Mkajadili Kula tunda kimasihala
Sio Kuharibu Mada yawatu
 
Kwakua una afya na nguvu unajona uko salama, siku yakikukuta ndio utajua mtoa mada anamaanisha nini.
Nishashindwa kupata huduma za kibingwa kwa kukosa bima, na ikabd kukaa na ugonjwa zaidi ya miaka miwili now ndo nahangaika kujiweka sawa , na kila after two weeks nipo Regency medical center ..... kuhusu janga la kiafya hapa Tz nishaexperience badly chief ... Huyo mzee aende Bugando , KCMC na Mhimbili aone jinisi watu wanavyokata Moto kwa kukosa huduma kisa hawana bima na hawana cash , inashangaza yeye ameambiwa akahakiki tuu taarifa bima yake iende viral anaanza kulia lia..kimsingi anatakiwa akae Ulaya na sio hii Tz
 
Mimi ni mstaafu mwandamizi niliyepo wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera.

Nilipata tetesi za kuwapo kwa uhakiki wa wastaafu walio kwenye mfuko wa bima ya Afya tangu mwezi Machi mwaka huu. Kila aliyeniambia nilipomuuliza alikozipata taarifa, naye aliniambia ameambiwa na mwingine.
Hakukuwapo uthibitisho wa chanzo.

Nilihisi kuwa ni jumbe za kitapeli ambazo zinatumwa mara kwa mara. Jana, jamaa yangu akanitumia na kuniuliza iwapo nimepata ujumbe huu:

"NHIF 17.03.2023 SAA 03:11PM NDG. MWANACHAMA MSTAAFU,TAFADHALI FIKA NA MWENZAWAKO KTK. OFISI YA MFUKO ILIYO KARIBU KWA AJILI YA ZOEZI LA UHAKIKI KABLA YA 30.04.2023. AIDHA, FIKA NA NA. YAKO YA NIDA NA NA. MWENZA WAKO. KWA UFAFANUZI _ PIGANA. 199 BILA MALIPO. SENDER HENRY".

Naye alitumiwa na mstaafu mwenzetu. Sikuamini kuwa huo ni ujumbe halali. Mtindo/namna ya uandishi haikuniongoza kuamini kuwa umetumwa na taasisi hii kubwa. Kuna makosa mengi ya kiuandishi na hata ya kimantiki. Hilo tuliache.

Niliingia kwenye tovuti yao. Sikuona tangazo hilo. Niliwasiliana nao kupitia simu hiyo 199. Nilipata ushirikiano mkubwa kwa aliyenipokea. Niliambiwa yafuatayo:

1. Ni kweli uhakiki upo. Unahusisha wastaafu na walioko kazini. Wanataka mstaafu aende na mweza wake.

2. Kila mhusika alishaarifiwa kupitia simu yake na kila mmoja ana tarehe yake. Mimi na wastaafu sita niliowauliza hatuna ujumbe huu.

3. Uhakiki unafanyika makao makuu ya mkoa.

4. Mwisho wa uhakiki ni Mei 30.

Inaelekea bima ya afya hawafahamu kuwa Wastaafu (wateja wao):
i) Ni wazee
ii) Wengi ni wagonjwa
iii) Wengi wana pato duni mno ambalo huenda halitoshi hata gharama ya kwenda mkoani.
iv) Baadhi ni walemavu
v) Kuna ambao hawawezi kusoma jumbe hizo

Yaani wao kwenye simu zao wanafahamu kubonyeza kitufe kimoja tu. Cha kupokelea simu.
Hawa hawawezi kuweka vocha, kukata simu baada ya maongezi, kuongeza salio, kuunga kifurushi nk.
Sembuse kusoma au kuandika ujumbe!

Ushauri:
1. Uhakiki ufanywe jirani na wahusika. Ikiwezekana kwenye Kata. Kuwalazimisha kwenda mkoani kuachwe. Haya ni mateso. Mateso makubwa mno.

Mstaafu aliyepo kijiji cha Muganza wilayani Ngara, mkoa wa Kagera, uhakiki huu utamgharimu siku 5 (kwenda Bukoba na Kurudi). Baadhi ya wastaafu wanahitaji kusindikizwa/kupata wasaidizi. Mbali ya adha za safari, fikiria muda na gharama za safari. Mkifika kwenye kata zao ni vema zaidi.

2. Zoezi hili lifanyike kwa uwazi na kwa haki. Tangazeni kwenye vyombo vya habari. Wekeni kwenye tovuti yenu.
Wasilianeni vema na wateja/wadau wenu. Uduni wa taarifa hizi na hata uandishi wa sms ya wito tunautofautishaje na sms nyingine za kitapeli tunazotumiwa mara kwa mara.

3. Fungueni ofisi wilayani au muweke dawati lenu ama kwa Mkuu wa wilaya au Halmashauri. Mnataka wazee hawa wafe kwa ajali barabarani kwa safari? Mara uhakiki wa PSSSF mkoani na sasa uhakiki huu nao mkoani.
Magonjwa mengine yanatokana adha hizi.

Wazee mnaowasumbua na kuwatesa leo walitumikia nchi hii kwa bidii na uaminifu mkubwa. Msiwalipe mateso kwa kuwajaza majuto na kihoro.

KWA HALI HII, UZEE SI DHAHABU BALI NI ADHABU.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Pole sana , najihisi kuogopa sasa maana
 
Hizo nguvu za kuhakiki wangeziwekeza kwenye kuzuia wezi ingekuwa poa sana
 
Nishashindwa kupata huduma za kibingwa kwa kukosa bima, na ikabd kukaa na ugonjwa zaidi ya miaka miwili now ndo nahangaika kujiweka sawa , na kila after two weeks nipo Regency medical center ..... kuhusu janga la kiafya hapa Tz nishaexperience badly chief ... Huyo mzee aende Bugando , KCMC na Mhimbili aone jinisi watu wanavyokata Moto kwa kukosa huduma kisa hawana bima na hawana cash , inashangaza yeye ameambiwa akahakiki tuu taarifa bima yake iende viral anaanza kulia lia..kimsingi anatakiwa akae Ulaya na sio hii Tz
Asante sana kwa.maoni yako.
Nakuomba usome tena maelezo yangu.
Ukiwauliza wataalam, hata uzee ni aina.ya ugonjwa.
Hivi unapoona TRA, benki, NSSF, wapo kila wilaya unaona wamekosea?
Hao wanaopeleka huduma za kifedha hadi vijijini wanalenga nini?
Serikali inapojenga zahanati, vituo vya afya, shule, vyuo vya Ufundi, vituo vya polisi nk karibu na wananchi inakusudia nini?
 
Tutafute hela aisee maana huko mbeleni matibabu yatakuwa ghali sana
 
Nishashindwa kupata huduma za kibingwa kwa kukosa bima, na ikabd kukaa na ugonjwa zaidi ya miaka miwili now ndo nahangaika kujiweka sawa , na kila after two weeks nipo Regency medical center ..... kuhusu janga la kiafya hapa Tz nishaexperience badly chief ... Huyo mzee aende Bugando , KCMC na Mhimbili aone jinisi watu wanavyokata Moto kwa kukosa huduma kisa hawana bima na hawana cash , inashangaza yeye ameambiwa akahakiki tuu taarifa bima yake iende viral anaanza kulia lia..kimsingi anatakiwa akae Ulaya na sio hii Tz
Sikushangai wewe kwasababu unafikiri kila mtu anaishi mazingira kama ya dar ambapo mtu kwenda mkoani anapanda daladala ya Tsh. 500.
Kuna maeneo ndani ya nchi hii mtu kwenda mkoani ni safari ya siku nzima na nauli ni kubwa, bado gharana za malazi maana muda anaofika ofisi zineshafungwa
Kumwambia aende na mwenzi wake maana yake gharama zinaongezeka mara mbili. Wazee wetu hawa wanahoja za msingi acha kuwakebehi
 
Nishashindwa kupata huduma za kibingwa kwa kukosa bima, na ikabd kukaa na ugonjwa zaidi ya miaka miwili now ndo nahangaika kujiweka sawa , na kila after two weeks nipo Regency medical center ..... kuhusu janga la kiafya hapa Tz nishaexperience badly chief ... Huyo mzee aende Bugando , KCMC na Mhimbili aone jinisi watu wanavyokata Moto kwa kukosa huduma kisa hawana bima na hawana cash , inashangaza yeye ameambiwa akahakiki tuu taarifa bima yake iende viral anaanza kulia lia..kimsingi anatakiwa akae Ulaya na sio hii Tz
Watu huwa hawashindani kwa matatizo. Kama unapitia magumu usitake na mwenzako ayapitie
 
Back
Top Bottom