A
Anonymous
Guest
JWTZ limeanzisha bima ya afya kwa ajili ya wanajeshi na familia zao ila bima hiyo imekuwa na msaada mdogo sana ukilinganisha na fedha ambazo tunachangia kwa mwezi kitoka katika mishahara yetu.
Masharti ya kunufaika katika bima hii ni mengi sana kiasi kwamba wanufaika wanashindwa kunufaika nayo:
1. Wanufaika wa bima hii wanalazimika kutibiwa katika hospitali za jeshi pekee. Ikihitajika kwenda hospitali za uraiani ni mpaka upewe rufaa toka hospitali za jeshi,kitu ambacho ni mara chache sana kupata, kwa kuwa hospitali za jeshi wanalazimisha kila kitu wafanye wao ili kupata fedha hizo za bima.
2-Matibabu ya kibingwa katika bima hii wananufaika wale wenye vyeo vya juu na familia yao pekee,wanajeshi wa vyeo vya chini na familia zao hawapati haki ya kupata matibabu ya kibingwa.
3. Familia za wanajeshi wanaoishi mbali na sehemu ambazo hospitali za jeshi zipo hawapati kabisa manufaa kutoka katika bima hii,kwa kuwa sharti lililowekwa ni lazima wakapate vibali vya kwenda hospitali za uraiani katika kambi za jeshi au ofisi za mshauri wa mgambo ambazo nazo zipo mbali hivyo huongeza ugumu zaidi.
Hivyo mfuko huu haujapunguza chochote kwenye changamoto za upatikanaji wa huduma za afya kwa wanajeshi na familia zao.