KERO Bima ya Afya ya Jeshi(JWTZ) haitusaidii Wanajeshi na Familia zetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
JWTZ limeanzisha bima ya afya kwa ajili ya wanajeshi na familia zao ila bima hiyo imekuwa na msaada mdogo sana ukilinganisha na fedha ambazo tunachangia kwa mwezi kitoka katika mishahara yetu.

Masharti ya kunufaika katika bima hii ni mengi sana kiasi kwamba wanufaika wanashindwa kunufaika nayo:

1. Wanufaika wa bima hii wanalazimika kutibiwa katika hospitali za jeshi pekee. Ikihitajika kwenda hospitali za uraiani ni mpaka upewe rufaa toka hospitali za jeshi,kitu ambacho ni mara chache sana kupata, kwa kuwa hospitali za jeshi wanalazimisha kila kitu wafanye wao ili kupata fedha hizo za bima.

2-Matibabu ya kibingwa katika bima hii wananufaika wale wenye vyeo vya juu na familia yao pekee,wanajeshi wa vyeo vya chini na familia zao hawapati haki ya kupata matibabu ya kibingwa.

3. Familia za wanajeshi wanaoishi mbali na sehemu ambazo hospitali za jeshi zipo hawapati kabisa manufaa kutoka katika bima hii,kwa kuwa sharti lililowekwa ni lazima wakapate vibali vya kwenda hospitali za uraiani katika kambi za jeshi au ofisi za mshauri wa mgambo ambazo nazo zipo mbali hivyo huongeza ugumu zaidi.

Hivyo mfuko huu haujapunguza chochote kwenye changamoto za upatikanaji wa huduma za afya kwa wanajeshi na familia zao.
Mlibaki kuua raia kutetea wadhalimu. Mkome.
 
Mmeshaanza kutoa milio ehh..nyie si mahodari, watu wakitaka kuandana kupinga mifumo mibovu mnatoana makambini kufanya usafi ili mtishe raia na bunduki zenu..yani ikiwezekana hata hizo bima zenyewe mnyimwe tuu..ili tuelewane
 
Nashauri wakatibiwe hospitali za polisi au magereza kuna mabingwa kule. Sikuizi polisi wameendelea kuliko wajeda
 
Polisi na hao Magereza wanajitafuta mkuu hao Polisi ndio kwanza wanataka wapande hadhi ya RRH kule Kilwa Road na kutafuta specialist wakutosha Magereza kule Ukonga ndio wanaongeza huduma taratibu zile za msingi yule MOI yule mama SSP ni Physician nafikiri ndio mwenyewe ana Elimu kubwa Pale
 
Mtoa maada yuko sahihi.

Kwa ninavyojua ukiwa askari wa kawaida sidhani kama(sjui) kama kuna nafasi ya kutoa maoni jeshini. Mtu aliyekuzidi cheo anakuona kama nini sjui utamshauri nini akuskilize, labda wakubwa kwa wakubwa.
 
Changamoto za Bima siyo jeshini tu! Hata sekta nyingine za umma.
Labda hapo kwenye huduma za kibingwa ndiyo najiuliza mnafanyaje kama wakubwa ndiyo pekee yao wanapata?
 
Back
Top Bottom