KERO Bima ya Afya ya Jeshi(JWTZ) haitusaidii Wanajeshi na Familia zetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
JWTZ limeanzisha bima ya afya kwa ajili ya wanajeshi na familia zao ila bima hiyo imekuwa na msaada mdogo sana ukilinganisha na fedha ambazo tunachangia kwa mwezi kitoka katika mishahara yetu.

Masharti ya kunufaika katika bima hii ni mengi sana kiasi kwamba wanufaika wanashindwa kunufaika nayo:

1. Wanufaika wa bima hii wanalazimika kutibiwa katika hospitali za jeshi pekee. Ikihitajika kwenda hospitali za uraiani ni mpaka upewe rufaa toka hospitali za jeshi,kitu ambacho ni mara chache sana kupata, kwa kuwa hospitali za jeshi wanalazimisha kila kitu wafanye wao ili kupata fedha hizo za bima.

2-Matibabu ya kibingwa katika bima hii wananufaika wale wenye vyeo vya juu na familia yao pekee,wanajeshi wa vyeo vya chini na familia zao hawapati haki ya kupata matibabu ya kibingwa.

3. Familia za wanajeshi wanaoishi mbali na sehemu ambazo hospitali za jeshi zipo hawapati kabisa manufaa kutoka katika bima hii,kwa kuwa sharti lililowekwa ni lazima wakapate vibali vya kwenda hospitali za uraiani katika kambi za jeshi au ofisi za mshauri wa mgambo ambazo nazo zipo mbali hivyo huongeza ugumu zaidi.

Hivyo mfuko huu haujapunguza chochote kwenye changamoto za upatikanaji wa huduma za afya kwa wanajeshi na familia zao.
Inasikitisha sana.

Acha kulalamika ,onyesha uzalendo hata msipotibiwa na serikali toeni fedha mifukoni mwenu mkajitibie.
 
Ni vzr kukumbushana kuwa JWTZ ndio moyo wa nchi. Hakuna sovereignty bila jeshi. Kwa vyovyote vile, taarifa za Jeshi ndizo number one top secret za nchi.

Hii ndio sababu ya askari kutokutumia bima za kiraia. Hoja kubwa ilikuwa ni shirika litakalopewa kazi ya kutoa huduma za bima kwa askari lingekuwa na taarifa ya nchi ina askari wangapi kila wakati, na rekodi ya matibabu ya familia zao. Kiusalama hili halikubaliki kabisa.

Kwahiyo ni vyema mkazoea kukubaliana na hali halisi. Hata kama kunachangamoto maboresho myafanye kupitia mifumo ya ndani, siyo hii yetu ya kiraia
Hii hoja ina matundu sana, nchi zilizoendelea unapata takwimu za idadi ya Manpower waliyonayo jeshini, na hata baadhi ya aina ya silaha walizonazo. Ila huoni wakipokwa hiyo "sovereignty" unayosema.

Labda nikuulize swali, kitambulisho cha NHIF zinabeba taarifa zipi?
 
JWTZ limeanzisha bima ya afya kwa ajili ya wanajeshi na familia zao ila bima hiyo imekuwa na msaada mdogo sana ukilinganisha na fedha ambazo tunachangia kwa mwezi kitoka katika mishahara yetu.

Masharti ya kunufaika katika bima hii ni mengi sana kiasi kwamba wanufaika wanashindwa kunufaika nayo:

1. Wanufaika wa bima hii wanalazimika kutibiwa katika hospitali za jeshi pekee. Ikihitajika kwenda hospitali za uraiani ni mpaka upewe rufaa toka hospitali za jeshi,kitu ambacho ni mara chache sana kupata, kwa kuwa hospitali za jeshi wanalazimisha kila kitu wafanye wao ili kupata fedha hizo za bima.

2-Matibabu ya kibingwa katika bima hii wananufaika wale wenye vyeo vya juu na familia yao pekee,wanajeshi wa vyeo vya chini na familia zao hawapati haki ya kupata matibabu ya kibingwa.

3. Familia za wanajeshi wanaoishi mbali na sehemu ambazo hospitali za jeshi zipo hawapati kabisa manufaa kutoka katika bima hii,kwa kuwa sharti lililowekwa ni lazima wakapate vibali vya kwenda hospitali za uraiani katika kambi za jeshi au ofisi za mshauri wa mgambo ambazo nazo zipo mbali hivyo huongeza ugumu zaidi.

Hivyo mfuko huu haujapunguza chochote kwenye changamoto za upatikanaji wa huduma za afya kwa wanajeshi na familia zao.
Na nyie mnalalamika online?
 
Inasikitisha sana.

Acha kulalamika ,onyesha uzalendo hata msipotibiwa na serikali toeni fedha mifukoni mwenu mkajitibie.
Usipotoze utu wako kisa una ID fake, unaweza ukawa unawachukia askari (kwa sababu ya uelewa wako mdogo kuhusu wao au kwa sababu ya matendo ya askari wachache) ila usi-generalize mambo.

JF siyo Jukwaa la raia pekee, ni jukwaa la wote, yoyote mwenye jambo anaweza kutumia Jukwaa hili kuliwasilisha kwa imani kwamba waliopo kwenye nafasi za maumizi wanaweza kuiona na kuifanyia kazi.

Ukisoma mada iliyowasilishwa, unaona kabisa hiyo bima ilivyo ya hovyo, yaani Mtu atoke Ngarenanyuki aje Lugalo kutibiwa kisa tu bima ndo inamtaka aende hospitali za aina fulani?
 
Bima ya afya kwa wote itakuwaje kama ya jeshi haina msaada. Kwao .

Sasa hili halituhusu maana hatujakukatia bima sisi nenda ulipokatiwa bima tunakupa ushauri hapa sio nhif hapa ni jamiiforums.
Hivi kuna sehemu amesema amewaandikia "nyinyi", mtu katumia Jukwaa kuwasilisha hoja yake. Kama huusiki nayo, usiishadadie. Katafute zinazokuhusu.
 
Hivi kuna sehemu amesema amewaandiki "nyinyi", mtu katumia Jukwaa kuwasilisha hoja yake. Kama huusiki nayo, usiishadadie. Katafute zinazokuhusu.
Hasira ya nini eti angeandika kwa siri ila kama nimeona naongea kwani humu kuna kutawaliana humu sio kwenu jeshini mtutese humu tunaamua chakusema humu sio nhif .
 
Hii hoja ina matundu sana, nchi zilizoendelea unapata takwimu za idadi ya Manpower waliyonayo jeshini, na hata baadhi ya aina ya silaha walizonazo. Ila huoni wakipokwa hiyo "sovereignty" unayosema.

Labda nikuulize swali, kitambulisho cha NHIF zinabeba taarifa zipi?
Unakiapo chochote cha utii na uaminifu kwa JMT? Isije kuwa ww mwenyewe haupo kwenye chombo, ila unataka wenzako waje kichwakichwa wachangie kwenye haya mawazo yako halafu wapigwe shoti?
 
Maisha Yana Mengi Kuliko Unayoyajua
Ukimtazama Askofu, Padre, Mchungaji, Apostle, Sheikh Imamu

LKwa Nje Kama Wabakula Mema Ya Nchi Ila Ndani Msoto Mkali

Watu Hawapendani
jiulize Wenye Vyeo Vya Juu Wanatibiwa Chap Hawa Wa Chini Wanahaha
Halafu Wote Mnaumwa
Unajiuliza Elimu Kupitia Vyeti Hazijatusaidia Kabisa
 
Unakiapo chochote cha utii na uaminifu kwa JMT? Au unataka, wenzako waje wachangie kwenye haya mawazo yako halafu watumbukie shimoni?
Huna haja ya kutisha watu, ila mambo mengi unayotaka kuaminisha watu kuwa yanapaswa kuwa siri, hayana unyeti wowote. Hoja uliyotoa haina mashiko yoyote. Huwezi kuwaambia watu wazoee changamoto za kutengeneza.
 
Hasira ya nini eti angeandika kwa siri ila kama nimeona naongea kwani humu kuna kutawaliana humu sio kwenu jeshini mtutese humu tunaamua chakusema humu sio nhif .
Kwamba una mamlaka ya kuamua ni habari gani ichapishwe humu au stress za kutokuwa na mtu wa kuku chojosha ndo zinakufanya unadhurura mtandaoni kuvamia mada ambazo hazikuhusu.
 
JWTZ limeanzisha bima ya afya kwa ajili ya wanajeshi na familia zao ila bima hiyo imekuwa na msaada mdogo sana ukilinganisha na fedha ambazo tunachangia kwa mwezi kitoka katika mishahara yetu.

Masharti ya kunufaika katika bima hii ni mengi sana kiasi kwamba wanufaika wanashindwa kunufaika nayo:

1. Wanufaika wa bima hii wanalazimika kutibiwa katika hospitali za jeshi pekee. Ikihitajika kwenda hospitali za uraiani ni mpaka upewe rufaa toka hospitali za jeshi,kitu ambacho ni mara chache sana kupata, kwa kuwa hospitali za jeshi wanalazimisha kila kitu wafanye wao ili kupata fedha hizo za bima.

2-Matibabu ya kibingwa katika bima hii wananufaika wale wenye vyeo vya juu na familia yao pekee,wanajeshi wa vyeo vya chini na familia zao hawapati haki ya kupata matibabu ya kibingwa.

3. Familia za wanajeshi wanaoishi mbali na sehemu ambazo hospitali za jeshi zipo hawapati kabisa manufaa kutoka katika bima hii,kwa kuwa sharti lililowekwa ni lazima wakapate vibali vya kwenda hospitali za uraiani katika kambi za jeshi au ofisi za mshauri wa mgambo ambazo nazo zipo mbali hivyo huongeza ugumu zaidi.

Hivyo mfuko huu haujapunguza chochote kwenye changamoto za upatikanaji wa huduma za afya kwa wanajeshi na familia zao.
Hakuna aliyesalama chini ya uongozi wa CCM.
 
Huna haja ya kutisha watu, ila mambo mengi unayotaka kuaminisha watu kuwa yanapaswa kuwa siri, hayana unyeti wowote. Hoja uliyotoa haina mashiko yoyote. Huwezi kuwaambia watu wazoee changamoto za kutengeneza.
Msamehe Bure Watu Wanakatwa Pesa Watibiwe Halafu Huduma Zimeminywa Na Wachache Anaposema Wzhuni Wanasema Ni Siri

Jamaa Anayekupinga Jau Sana Sana
Mambo Sasa Yanakwenda Kasi
Tiba Ni Lazima
 
Nikiwa kama Mtumishi wa Afya na hata leo nimepokea wazee wawili hapa Kituoni wanahizi Form kwa uzoefu wangu mdogo wa miaka mi3 sasa kazini nikiri hii Bima wengi wanailalamikia sana

Nakupa hii scenario kwanza mkababa walioingia nao JwTZ ukiachana na vituo vyao vituo vilivyobaki vingi ni kuanzia RRH wengi hawana accsess ya kuona baadhi ya hospitali has zile za Private inampa usumbufu usio na sababu mgonjwa kuna mzee waliwahi toka Shelui akaja hadi kwa mshauri wa Mgambo Singida akapewa kibali afu akaenda Makiungu kufika huko akaambiwa hawapokei hiyo Bima mind you katoka shelui na kaambiwa Makiungu kuna huduma bora au kuna huduma yeye alitaka apate huko ikabidi arudi tena Singida Mjini akatibiwe Hospitali ya Mkoa ambako wanapokea
Huyo mzee hakufia njiani? Au Israel alikua buzzy hiyo siku?
 
Back
Top Bottom