KERO Bima ya Afya ya Jeshi(JWTZ) haitusaidii Wanajeshi na Familia zetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Changamoto yangu inahusu huduma za Bima ya Afya ya Jeshi (MHIF), ambayo imekuwa kero kwa wanachama na wategemezi wao.

Kwa mujibu wa malalamiko haya, mwanajeshi mwanachama hukatwa takribani Shilingi 51,000 kila mwezi kwa ajili ya bima hiyo. Hata hivyo, matumizi ya bima hiyo yamekuwa na changamoto, kwani hospitali zinazotambuliwa ni chache, hasa zile za Serikali.

Mara nyingi, ili mwanachama kupata huduma katika hospitali nyingine, anatakiwa kuanza katika kituo cha afya cha Jeshi na kupata barua ya rufaa (referral). Hata hivyo, kuna nyakati ambapo daktari huamua kutompatia rufaa mara moja na kumtaka mgonjwa kusubiri au kuendelea na matibabu katika kituo hicho.

Hali hii inazua maswali kadhaa: Kwa nini bima ya afya ya wanajeshi imetengwa na mfumo wa bima unaotumiwa na watumishi wengine wa Serikali? Kwa nini mwanachama analazimika kupewa hospitali maalumu za kwenda badala ya kuwa na uhuru wa kupata huduma katika hospitali zilizo ndani ya mtandao wa bima? Kwa nini hata wategemezi nao wanapaswa kufuata utaratibu huo wa kupata rufaa?

Aidha, changamoto nyingine ni upatikanaji mdogo wa madaktari bingwa katika baadhi ya hospitali za Jeshi, hali inayoweza kuwaathiri wanachama wanaohitaji huduma za kibingwa.

Tunaomba mamlaka husika zifanyie kazi changamoto hizi na kutoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa MHIF, ikiwemo sababu za kuwepo kwa taratibu hizi na hatua zinazochukuliwa kuboresha huduma kwa wanachama na wategemezi wao.

Wanajeshi na familia zao wanastahili kupata huduma bora za afya kwa wakati, bila kukumbana na urasimu usio wa lazima katika kupata matibabu.
Na bado kilio ni endelevu. Tukutane wakati ujao wa uchaguzii.
Safi sanaa. Mnyooshwe hivyo hivyo, kila mtu atafikiwa kwa wakati wake.
 
Usipotoze utu wako kisa una ID fake, unaweza ukawa unawachukia askari (kwa sababu ya uelewa wako mdogo kuhusu wao au kwa sababu ya matendo ya askari wachache) ila usi-generalize mambo.

JF siyo Jukwaa la raia pekee, ni jukwaa la wote, yoyote mwenye jambo anaweza kutumia Jukwaa hili kuliwasilisha kwa imani kwamba waliopo kwenye nafasi za maumizi wanaweza kuiona na kuifanyia kazi.

Ukisoma mada iliyowasilishwa, unaona kabisa hiyo bima ilivyo ya hovyo, yaani Mtu atoke Ngarenanyuki aje Lugalo kutibiwa kisa tu bima ndo inamtaka aende hospitali za aina fulani?
Si ndio utaratibu wa bima yao ya jeshi au? Unataka iweje? Hebu wewe toa suggestions za hili suala.
 
JWTZ limeanzisha bima ya afya kwa ajili ya wanajeshi na familia zao ila bima hiyo imekuwa na msaada mdogo sana ukilinganisha na fedha ambazo tunachangia kwa mwezi kitoka katika mishahara yetu.

Masharti ya kunufaika katika bima hii ni mengi sana kiasi kwamba wanufaika wanashindwa kunufaika nayo:

1. Wanufaika wa bima hii wanalazimika kutibiwa katika hospitali za jeshi pekee. Ikihitajika kwenda hospitali za uraiani ni mpaka upewe rufaa toka hospitali za jeshi,kitu ambacho ni mara chache sana kupata, kwa kuwa hospitali za jeshi wanalazimisha kila kitu wafanye wao ili kupata fedha hizo za bima.

2-Matibabu ya kibingwa katika bima hii wananufaika wale wenye vyeo vya juu na familia yao pekee,wanajeshi wa vyeo vya chini na familia zao hawapati haki ya kupata matibabu ya kibingwa.

3. Familia za wanajeshi wanaoishi mbali na sehemu ambazo hospitali za jeshi zipo hawapati kabisa manufaa kutoka katika bima hii,kwa kuwa sharti lililowekwa ni lazima wakapate vibali vya kwenda hospitali za uraiani katika kambi za jeshi au ofisi za mshauri wa mgambo ambazo nazo zipo mbali hivyo huongeza ugumu zaidi.

Hivyo mfuko huu haujapunguza chochote kwenye changamoto za upatikanaji wa huduma za afya kwa wanajeshi na familia zao.
Mtulie ..nyie si ndio mlikuwa mnaamisha silaha makambini na kuwapa wale wauawaji ... Mtulie...
 
Kumbe na nyinyi mnaisoma namba?
Acheni kutumika kisiasa tupambanie katiba mpya na tume huru
 
Hahhha
 
Bima ya afya kwa wote itakuwaje kama ya jeshi haina msaada. Kwao .

Sasa hili halituhusu maana hatujakukatia bima sisi nenda ulipokatiwa bima tunakupa ushauri hapa sio nhif hapa ni jamiiforums.
Hahahaa haya Tate Mkuu jibu hili shitaka
Analeta mambo gani tena huyu? Umempa ushauri mzuri! Ameishia kukushambulia na kufikiri eti hayupo wa kuku chojosha! Ni kwamba mimi ni mzee sana siwezi kusimamia ukucha!!!
 
Kwamba una mamlaka ya kuamua ni habari gani ichapishwe humu au stress za kutokuwa na mtu wa kuku chojosha ndo zinakufanya unadhurura mtandaoni kuvamia mada ambazo hazikuhusu.
Mjomba kuwa makini. Ukimshambulia SweetyCandy umenishambulia mimi. Mimi ndiye ninaye mchojosha, na humu JamiiForums tunazurula wote kwa raha zetu.
 
Usipotoze utu wako kisa una ID fake, unaweza ukawa unawachukia askari (kwa sababu ya uelewa wako mdogo kuhusu wao au kwa sababu ya matendo ya askari wachache) ila usi-generalize mambo.

JF siyo Jukwaa la raia pekee, ni jukwaa la wote, yoyote mwenye jambo anaweza kutumia Jukwaa hili kuliwasilisha kwa imani kwamba waliopo kwenye nafasi za maumizi wanaweza kuiona na kuifanyia kazi.

Ukisoma mada iliyowasilishwa, unaona kabisa hiyo bima ilivyo ya hovyo, yaani Mtu atoke Ngarenanyuki aje Lugalo kutibiwa kisa tu bima ndo inamtaka aende hospitali za aina fulani?
Hayo ni mawazo yangu ,sijatoa wazo lolote baya ,wao ni askari wameajiriwa ,wanamishahara ,kulalamika kwa vitu vidogo vya bima ni upuuzi ,kama bima yao inataka hivyo kwanini alijuiunga? Kama walilazimishwa basi ni MANYUMBU....Afya kwanza kama BIMA mbovu aipotezee atafute BIMA nyingine private.
 
Back
Top Bottom