Bima ya gari imekuwa anasa!

Bora ajichange akate ya Mwaka ili asahau Mwaka mzima,Mambo siku hizi ni mengi miezi 6 hii hapa fumba fumbua!!
Kuna kampuni ilikua inaitwa 'REAL INSURANCE' ilikua unalipia mwezi kwa mwezi
 
Watz tumezidi sana kulalamika jamani!

Yani mtu anaona 118,000 kwa mwaka ni nyingi mpaka anaifungulia uzi sasa huyu amemiriki gari ya nini?
Mtu kama huna uwezo wa kumiriki gari bora uache tu aisee
Hujajua maisha wewe. Watu ipo siku unabaki na 5,000/= mfukoni. Huku familia yote inakutizama. Sembuse 118,000/=?
 
Kumbe kuna Comprehensive full cover na nyingine isiyo full cover?
 
Hahaha yange Yange wa Sirro ni hatari bora ulipe tu hiyo 118k.
Hahah ni noma, nimeona wale wanaovalia jezi za bahasha wakiwa wanamshusha dereva flani wa roli kama gunia la mkaa kwenye clip flani halafu mara naskia mkuu wa mkoa wa Mbeya anakiri jamaa amevuta ila anaanda tume kwa ajili ya kuchunguza kifo chake.
 
Nadhani bima ingekuwa inakatwa miaka mitano.

Hii ya kila mwaka inazingua kinoma.

Hujakaa sawa mwaka umeshaisha, unahitaji kulipa tena.
 
Unakuta bima imeisha kipindi una ukataa. Mwaka jana nilataka nimalize mwaka mzima bila kulipia bima kabisa coz nnilikutana na viajari vingi ila bima haikuwa msaada hata kidogo.

Nilikomaa miezi 6 ninapenyeza mjini bila bima mpaka ndugu yangu mmoja alikuwa na vipesa akaamua kunilipia. Yani na angenipa cash nisingelipa.
 
Bima ni jambo jema sana lakini kwa hapa kwetu doh nadhani bima ingetakiwa iwe ni moja wapo ya taasisi inayoshikiliwa na serekali maana inapokea in HUGE na kujitahidi kutoa KIDUCHU mno by hook and crooks ni ukweli ukizuba tu hulipwi hata senti tano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…