Bimmer na Landcruiser V8

Sure.. Ila sio tech zote unaweza tumia za zamani.. Ukiitazama reviews za LC300.. Wanaongelea vitu vyake kufanana na 80 Series..!
Ishu ni kwenye engine sasa.. Standard ya emissions imekuwa juu.. Kwahiyo Toyota ili kuuza Ulaya inabidi engines zao zimeet European standards za emission.. Hapo ndio huwezi kutumia tech ya zamani.. Na Toyota hapo ana struggle..
Magari ya zamani ya Toyota ni reliable zaidi kuliko ya siku hizi..!
Toyota reliability aliijenga zamani..
Gari za Toyota za siku hizi nazo zina sensors kibao.. Not simple as kipindi hicho..!
 
Hili suala la speed ya gari ndogo kutofautiana na ya gari kubwa mfano zote zikiwa 100km/h linakera sijui kwanini wanalazimisha utofauti wakati zote zinasomeka kilomita kwa saa!nilibishana na watu wote wakinipinga nikawaacha na kujisemea bakini na ujinga wenu.
 
View attachment 2023217
Hizo ndio engine na speed za G wagon benz miaka hio! Ukizungumzia wakumzidi mjapani sidhani kama kuna zaidi ya hao akina benz! Ila kwa speed hizo Land Cruiser mkonga still alikuwa mwamba.
Mbona tdi alikuwa anammudu tu huyo hz tena milimani ndio kabisaa,mjapani alipoleta 12h-t akaiondolea unyonge hz[emoji3]
 
I mean tech ya zamani kwenye toyota sio kwenye engines. Engines zao kitambo tu zina sensors za emmissions. Ujue Lexus zina share same engines na toyota na zinauzwa Europe, Toyota ni maamuzi tu wamefanya kwamba model hii tutauza wapi na wapi. Wanajua kuwa huwezi kupeleka LC300 Europe ukauza same price na RR. Watu watachukua RR tu na sio kwamba ana struggle kumeet izo emmission standards.

Tech ya zamani mfano kwenye suspensions watatumia zile zile za zamani wakati wenzake kina RR unakuta wanatumia Air Suspension. Sunroof utakuta hio hio unayoiona kwenye crown inatumika kwenye v8 zao wakati wenzake RR wana panoramic roof. Ukija interiors ndo usiseme, layout ya dashboard na vitu vyake ni kama zamani tu. If it doesnt break dont fix it, ndio toyota hao. Crown ya 2010 haifui dafu kwa BMW 7 series 2002 in terms of features na uluxury na ndio crown unaambiwa flagship.

Most of snesors sio kwamba ni for emmissions, nyengine ni za kucheki uzima wa gari, suspension, gearbox. n.k

Nikasema kuwa toyota kwenye kushindana na german cars kamwachia Lexus
 
200hp halafu wanalinganisha na hz yenye 129 hp kweli!japo rover ilikuwa ni v8,hivi hawa team toyota wanajua kuwa hiyo hz haifui dafu mbele ya prado L150?
 
Kuna tajiri wa zamani mbeya alikuwa na mabasi yanaitwa obamka japo sijabahatika kuyaona yakiwa road ila yaliyoharibika niliyaona,alikuwa na ka-benzi milango miwili(convertible)ka 1965 kwenye dashboard kalikuwa na 220km/h kako juu ya mawe!
 
Ok sawa.. Hapo nilichokuwa na maanisha ni hiki..
Euro Emissions zinapanda siku baada ya siku.. European cars wameshakuwa na technology kubwa zaidi kabla ya Toyota.. Kwao kumeet hizo standards sio ishu sana.. Euro emission 5 ilifanya DPF kuwa mandatory kwenye diesel cars.. Toyota wakati huo gari flagship ni LC150 na LC200.. Sasa angalia early models za hizo gari jinsi zilivyopata shida na vumbi kwenye engine.. Diesel chafu.. Actually mpaka hivi karibuni Toyota ame recall baadhi ya gari HiLux ili kufix hiyo ishu..Engine ikipita kwenye vumbi kuna sensor zinapata shida..new model HiLux sio kama HiLux ilipojenga jina enzi hizo..

Toyota Supra iv.. Engine yake 2jz Gte.. Bonge la engine na sifa zake zinajulikana kote.. Umeona new Supra.. Engine B58 kutoka kwa Bimmer.. Why hawajaweka their legendary engine wahangaike kusource mpya!!kwa standards za leo za emissions ni ngumu sana 2jz Gte kumeet..!

Kwenye sensors.. Toyota Landcruiser ya 1990 haina sensors kama Landcruiser ya 2010.. Kwahiyo sio kwamba hawakuwa na sensors.. Zilikuwepo.. Chache sana.. Ila sasa hivi engines za Toyota unakuta zina sensors nyingi.. Yote hii ni kuhakikisha gari zinakuwa na clean emission hazichafui mazingira.. Ukishaanza kuwa na vitu vingi kwenye gari.. Unaongeza chance ya kitu kimoja kuzingua.. Kwahiyo hata Toyota magari yao sio reliable kama ya zamani..!

Kwahiyo tangu zamani gari ya mzungu ilikuwa imetengenezwa kwa technology kubwa.. Halitaki vitu chini ya standard.. Toyota aliinvest vitu basic..
Sasa game inachange na Toyota anaanza kuonyesha weakness zake ikija mambo ya technology..!
 
Sema Toyota anatumia global diesel tech. Kumeet emissions GD6
 
Sahivi LC300 haiendi Europe wala North America. Inakuja Africa, Middle East, Asia, South America na Australia.

LC 200 ilistruggle sana kuuza N.A na EU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samsung zinadondoka thamani haraka sana kulinaganisha na iPhone
Ujue mkuu siku zote Samsung yeye anatengeneza simu kwa ajili ya wateja wa hali zote kiuchumi. Ana simu za high range, mid range, na low range ili mteja anunue simu kulingana na uwezo wake.

Tofauti na iPhone ambaye yeye simu zake ni high range tu hanaga longolongo hauwezi nunua tafuta brand nyingine au subiri zishuke bei. Sasa kwa bongo wateja wengi wa Samsung wananunua hizi mid na low.

Wengi hawana uwezo wa kununua high ambazo bei na ubora wake zinalingana na iPhone tena na nyingine zimezidi. So ukweli ni kwamba zinazowahi kudondoka thamani haraka ni hizi mid na low siyo high.
 
Yes nakubaliana.. Kila mmoja ana strength zake.. Ila usiseme hawawezi kufananishwa..!
Ukifananisha nguvu..luxury.. Mjerumani..!
Ukija kwenye uimara.. Practical kwa hapa nyumbani TZ.. Mjapani..!
Bora wewe umenielewa kidogo mkuu. Sisi hatuzipondi Bimmer binafsi katika gari zote za mjerumani mimi Bimmer nimeinyanyulia mikono kina MB na VW na mwanaye Audi wote hawaikuti ila penye ukweli inabidi tuambiane tu.
 
Kwamba BMW isifananishwe na Land Cruiser kisa tu Land Cruiser ni Toyota? Ndicho wabongo wengi wanachoponda hiki!
 
Anachowazidi LC hao wengine ni reliability tu. Hamna kingine. Luxury, speed, handling, ride quality muonekano etc LC hawagusi wajerumani. Labda kwa entry model zao.
Muonekano? Teh BMW show ya mbele kwenye most cars ni mbaya bana na zile vents kama pua za nyati! [emoji23][emoji23]

Hapo kwenye muonekano hasa wa nje hebu muacheni Land Cruiser aisee bila kusahau mlio wa engine! Kwa muonekano BMW kazidiwa hadi na Mercedes Benz kuanzia body hadi interior designs!

By the way hivyo vitu kama muonekano na mlio wa engine ni subjective tu
 
Mkuu, leo unaweza nunua Samsung ya daraja la juu kabisa, na iPhone pia kwa wati mmoja, chukua iPhone ya 2.5 million na Samsung ya 2.5 million, mje muuze mwakani ndio utajua Samsung zinavyo poromoka thamani haraka ukilinganisha na iPhone. Sio napondea Samsung nimezitumia na inatumia ila ikija kwenye value iPhone kamkata gape mbali
 
BMW ana mionekano tofauti tofauti mbele inategemea unataka muonekano upi, kuhusu milio inategemea mkuu wangu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…