Emmission standards zimebadilika tofauti na zamani. za miaka ya 90 zio za miaka ya 2000. Za zamani huwezi ku import Europe sasa ivi kwa sababu hazimeet hizo standards. Ndio maana Toyota akawa na engines mpya ambazo zinatumika Euro na hasa kwa kutumia brand ya Lexus, engine hizo hizo tunaziona kwenye toyota saiv na bado toyota hauzi Europe.
2jzgte ni engine moja babkubwa kwa perfomance, lakini sababu ya kwanini toyota hawakuiweka kwenye Supra mpya, sio kwamba emmissions (ingawa haikuwa certified tangu mwanzo kukubalika in Europe) bali ni engine ya zamani mno, Toyota wameachana na Inline 6 engines na wamehamia kwa v6, kwao kuanza development upya ya kuweka 2jzgte sio cost efficient (inabidi waanze from scratch wakati assembly ya hio engine imeshauliwa) na ndio wakaamua kwenda na BMW engine, in short wamechukua BMW wakaibandika badge ya Supra the same wamefanya kwa FT86 ambayo ni subaru.
Sensors za emmission zina collect data ku make sure gari ina run kwenye standards zilizowekwa, sioni vipi zinachangia katika ubovu wa chombo zaidi ya kukwambia tu kama gari yako ita fail emmission test n.k Mfano Oxygen sensor, ina collect data ECU inapewa taarifa mafuta iongeze au ipunguze, lakini o2 sensor kama o2 sensor hai control physicial device. Sasa general rule ni kwamba ukiongeza vitu manake unaongeza more things to fail, lakini sio in a sense kwamba its not reliable. Umeongeza tu idadi ya vitu ofcourse uta repair vingi kuliko alokuwa na vichache.
Nakubaliana na wewe kuwa toyota ana vitu basic, Haziendani kabisa na wengine, wapo nyuma na wamejiekea nyuma makusudi. Wao kama kitu kinafanya kazi vizuri kwanini wafanye njia nyengine? wanaona bora wakiache ivo ivo. Sasa wenzao wanakwenda na technology, kama wanaweza kuweka bluetooth brakes (jokes) kwanini wasiweke?
Tutizame Air suspension vs Coil Springs, chances za ku fail air suspension ni high kuliko coil springs, sasa toyota hapo anaona ah wacha niweke coil springs, RR na wenzake wacha tuweke Air Suspension for ride comfort anaenunua RR ana uwezo wa kununua Air suspension nyengine tu.