Binadamu ana majibu ya maswali yote! Wachache wanaujua huu ukweli

Binadamu ana majibu ya maswali yote! Wachache wanaujua huu ukweli

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
5,315
Reaction score
13,269
Ukiniuliza swali nikupe majibu, majibu nitakayokupa mimi ni yangu binafsi sio yako.

Majibu yangu nitakayokupa yatatokana na experience yangu na sio yako.

Wewe una experience yako, mimi nina experience yangu. Kama swali lako ni la ki proffesional na mimi ni proffesional basi majibu yangu yatakufaa yatakusaidia

Ila kama swali lako ni kuhusu maisha yako mfano ufanye biashara gani au unaniuliza ukasomee vitu gani au nikupe ushauri kuhusu ndoa yako! Majibu nitakayo kupa mimi ni yangu wala sio yako sababu wewe umenisaidia mimi kujiuliza swali kisha nikajijibu mwenyewe


Majibu yangu hayatakusaidia sababu ni yangu na sio yako, experience yangu na yako ni tofauti.

Ukiwa na swali kuhusu maisha yako tafuta majibu yako wewe mwenyewe ktk akili yako na sio ktk akili ya mtu mwingine

Kwwnini uiamini akili ya mtu mwingine na usiiamini akili yako?


Usiku ukilala na mawazo ya kulogwa basi utaota wachawi wote nchi hii wanakuroga sababu umeuliza swali la kurogwa na majibu yake ndio hayo

Ukibanwa mkojo usingizini hili litakuwa swali indirect! Akili itaanza kutafuta majibu na itayapata itakuonyesha choo kilipo na utakojoa kweli hapo hapo kitandani ila ktk akili yako majibu ni choo au kichaka ndio sehemu sahihi ya kukojoa


Ukilala na mawazo ya uzinzi hili ni swali indirect! Utaota unafanya mapenzi na mwanamke mrembo na utapiga bao kweli!


Kwanini uulize maswali ya kipuuzi ktk akili yako yenye madini ya thamani? Kichwani kuna mgodi wa dhahabu, kuna majibu yote ila wengi hatujui kama tunayo


Tuna changamoto nyingi za kimaisha, tunamaswali mengi ya msingi haya maswali tuyaulize usiku wakati wa kulala majibu yatajitokeza ktk namna ambayo huwezi kuitarajia yatakuja ktk mfumo wa ndoto

Watu mashuhuri wanaujua huu ukweli
 
..Maisha ni magumu.
Kuna muda uwezo wa kufikilia ..unapungua kutokana na stress na uchovu wa akili
..Kuuliza ni muhimu pia ili upate uzoefu wa mtu mwingine
 
Back
Top Bottom